Kazi za MalaikaMalaika wamepewa kazi ya kumtumikia Allah(SW) kwa kumtukuza na kumtakasa, kama wanavyosema wenyewe:Hakuna yoyote miongoni mwetu ila anapo mahali pake mahususi. Na kwa yakini katika sisi wapo wajipangao safu. Na wako katika sisi wamtukuzao(Mwenyezi Mungu)(3 7:1 64-1 66)
Malaika pia hushughulikia mambo ya wanadamu katika maisha ya duniani na Akhera. Miongoni mwa mambo hayo ni:(1) Kuleta ujumbe kwa wanaadamu kutoka kwa Allah (s.a.w.).
Kazi ya kwanza ya malaika ni kuleta ujumbe wa Allah(SW) kwa wanadamu. Ujumbe huo huweza kuwa ni mwongozo wa maisha(Wahy) au habari juu ya jambo fulani. Malaika hupeleka ujumbe wa Allah(SW) kwa mitume au watu wa kawaida.


Huteremka Malaika na wahy kwa amri yake juu ya anaowataka katika waja wake kuwa “onyeni kuwa hakuna wa kuabudiwa isipokuwa Mimi, basi niogopeni” (16:2)
Jibril, ambaye ndiye mkuu wa Malaika, ndiye mjumbe mkuu aliyekuwa akiwaletea Mitume wote Wahyi. Yeye ni mwalimu mkuu aliyeteuliwa na Allah(SW) kuwafunza mitume namna ya kuwalingania watu Uislamu kwa maneno na matendo.Hakika hii Quran ni neno lililoletwa na mjumbe mtukufu, malaika mwenye nguvu na hadhi kubwa kwa Mw enyezi Mungu. (81:19-20)(2)Kuandika amali za wanaadamu njema na mbaya.
Kila mtu ana malaika waandishi wawili, kulia na kushoto kwake. Unaposema au kutenda jema au baya hadharani au umejificha peke yako, malaika hawa wanakuona na kurekodi jambo hilo.Wanapopokea w apokeaji w awili, anayekaa kuliani na anayekaa kushotoni. Hatoi (mtu)kauli yoyote isipokuw a karibu naye yupo mngojeaji(malaika) tayari (kuandika.) (5 0:1 7-18).(3)Kuwalinda wanaadamu. Qur’an inatufahamisha
Kazi ya tatu ya malaika ni kumchunga na kumlinda kila mtu na vitu vya hatari vilivyo nje ya uwezo wake.Ana (kila mtu) kundi (la malaika) mbele yake na nyuma yake. Wanamlinda kwa amri ya Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu habadili yaliyoko nafsini mwa watu mpaka wabadili wao yaliyomo katika nafsi zao. Na Mw enyezi Mungu anapowatakia w atu adhabu, hakuna cha kuzuia wala hawana mlinzi yeyote badala yake Mwenyezi Mungu (13:11)
Kwa ulinzi huu wa malaika utokao kwa Allah(SW), mtu hata kama atachukiwa na dunia nzima na kwahiyo wakafanya njama za kutaka kumdhuru, hawataweza mpaka Allah(SW) aondoe ulinzi wake.Vivyo hivyo, kama Allah(SW)atauondoa ulinzi wake huu kwa mtu, hakuna wa kumkinga na shari hata kama atalindwa na mitambo madhubuti ya kisasa pamoja na wataalamu wa ulinzi wa ulimwengu mzima.(4) Kuwaombea waumini msamaha kwa Allah (s.w.)
Malaika pia wana kazi ya kumwomba Allah(SW) awasamehe wale watu wanaotubia na kufuatisha vitendo vyema.Humwomba Allah(SW) awasamehe, afute makosa yao, awarehemu kwa kuwalipa pepo na kuwaepusha na adhabu ya Moto.
“Wale wanaokichukua kiti cha enzi(cha Mwenyezi Mungu) na wale wanaokizunguka, wanamtukuza Mola wao na kumsifu na wanamuamini na wanawaombea msamaha waliaomini. (Wanasema): “Mola wetu! Umekienea kila kitu kwa rehema na Elimu. Basi wasamehe waliotubu na kufuata njia yako na waepushe na adhabu ya Jahannam ”(40:8)Na Mwenyezi Mungu anaahidi kuwa wale wanaotubu kwa kujuta juu ya maovu waliyofanya, wakamuamini Yeye ipasavyo, kwa kujizuia kuyaendea maovu na badala yake wakashikamana na mwenendo mwema; Atabadilisha maovu yao kuwa mema! Qur’an inathibitisha hili katika aya ifuatayo, inasema:Ila yule atakayetubia na kuamini na kufanya vitendo vizuri; basi hao ndio Mwenyezi Mungu ataw abadilishia maovu yao kuwa mema, na mwenyezi Mungu ni mwingi wa kusamehe na Mwingi wa kurehemu.(25:70)(5)Kuwasaidia waumini vitani katika kupambana na madhalimu
Miongoni mwa kazi tukufu za malaika ni kuwasaidia waislamu kupambana na maadui wenye nguvu kubwa kijeshi katika vita. Qur’an inatueleza kuwa:Naam. Kama mtasubiri na kujilinda na makatazo yake(Allah) na maadui wakakufikieni kwa ghafla, hapo Mola wenu atakusaidieni kwa Malaika elfu tano washambuliao kwa nguvu (3 :125)(6)Kuwaangamiza watu waovu waliopindukia mipaka
Malaika pia wana kazi ya kuwaangamiza watu waovu waliokubuhu na kupindukia mipaka. Watu wa nabii Lut waliangamizwa na Malaika baada ya kubobea katika maovu nakukataa kwao kujirekebisha. Tunafahamishwa hili pale malaika walipomjibu nabii Ibrahiimu(as).Wakasema: “Hakika sisi tumetumwa kwa wale watu w akosa(tuw aangam ize). Isipokuw a w aliomfuata Lut. Bila shaka sisi tutawaokoa wote hao(15:58-59)(7)Kutoa roho za watu.Kuna malaika wengi wanaohusika na utoaji wa roho za wanadamu wakati muda wao wa kuishi duniani unapokamilika. Malaika mkuu wa kazi hii ni Malakul-mauti.Atakufisheni Malaika wa mauti aliyewakilishwa kwenu, kisha mtarejeshwa kwa Mola wenu(32:11)
(8)Kuwaliwaza na kuwakaribisha watu wema peponi
Kabla ya kutolewa roho, kila mtu aliyetenda mema na kutofanya maovu atashukiwa na malaika wa kumliwaza. Watamwambia Ewe nafsi yenye kutulia! Rudi kwa Mola wako hali ya kuw a utaridhika Naye amekuridhia. Basi ingia katika kundi la waja (wazuri) uingie katika pepo yangu. (89:2 7-30)Na siku ya Kiama watawapokea na kuwakaribisha kwenye pepo ya Allah(SW) yenye neema za kudumu. Watawaambia:Amani juu yenu, furahini, na ingieni humu mkae mile le (39:73)(9) Kuwaadhibu watu waovu motoni
Watu wanaotenda maovu watakuwa katika adhabu kali kwenye Moto wa Jahannam. Mwenyezi Mungu amewaweka malaika maalumu kwa ajili ya kuwaadhibu watu waovu wasiotaka kutubia, kujirekebisha wala kutenda mema. Allah(SW) anamtangazia kila mtu mwenya tabia hizi kuwa:Karibuni hivi nitamtia katika Moto. Na ni nini kitakachokujulisha Moto huo? Haubakizi w ala hausazi, unababua ngozi mara moja.Juu yake wako malaika(walinzi) kumi na tisa.(74:26-30).
Mkuu wa malaika hawa wa adhabu katika Jahannam ni Malik. Kutokana na machungu ya adhabu watakayopata, watu waovu watalia na kutamani mauti, watamtaka Malik amwombe Allah(SW) awafishe kuliko hiyo adhabu inayowakabili.Nao watapiga kelele: watasema: “Ewe Malik! Na atufishe Mola wako!” (Maliki) atasema: “Kwa hakika mtakaa humu humu ”(43:77)Na Mwenyezi Mungu anasifu kuwa adhabu watakayotoa 158malaika hao kutokana na uwezo aliowapa haitakuwa na mfano wake katika adhabu hizi za duniani.


Siku hiyo mwanadamu atakumbuka, lakini kukumbuka huko kutamfaa nini. Atasema: “Laiti ningalitanguliza(wema) kw a ajili ya uhai wangu (huu wa leo). Basi adhabu ya(Allah) siku hiyo, haitolingana na adhabu aitoayo yeyote (katika wanadamu). Wala hatafunga yeyote jinsi ya kifungo chake (Allah)
(89:23-26).