image

Nafsi ya mwanaadamu

Nafsi ya mwanaadamu

Nafsi ya mwanaadamu


“Na katika ardhi zipo (alama namna kwa namna za kuonyesha kuwepo Allah (s.w) kwa wenye akili. Na katika nafsi zenu (pia zimo ishara hizo)Je, hamuoni?” (51:20-21)
Ukimtafakari mwanaadamu utapata dalili nyingi zinazothibitisha kuwepo kwa Allah (s.w). Maeneo ya kutafakari ni pamoja na:(i) Chanzo na mwisho wa uhai wa mwanaadamu“Vipi mnamkanusha Allah (s.w) na hali mlikuwa wafu, akakuhuisheni, kisha atakufisheni, kisha atakurudisheni (tena) kisha kwake mtarejeshwa” (2:28)“Basi mbona (roho) ifikapo kooni, na nyinyi wakati ule mnamtazama. (56:83-84)Nasi tunakaribiana naye zaidi (huyo anayetoka roho) kuliko nyinyi, wala nyinyi hamuoni. (56:85)Kama nyinyi hamumo katika mamlaka (yangu), kwanini hamuirudishi (hiyo roho) ikiwa mnasema kweli?” (56:86-8 7).(ii)Asili ya mwanaadamu “Na katika ishara zake (za kuonyesha kuwepo kwake) ni huku kukuumbeni kwa udongo kisha mnakuwa watu mnaoenea (kila mahali).” (30:20)(iii)Kuumbwa Wanaume na Wanawake “Je! Anafikiri binaadamu kuwa ataachwa bure (asipewa amri za Mwenyezi Mungu wala makatazo yake)? Je, hakuwa tone la manii lililotonwa? (75:36-37).Kisha akawa kidonge cha damu, kisha akamuumba na akamsawazisha, kisha akamfanya namna mbili, mwanamume na mwanamke.(75:38-39).Je! Hakuwa huyo ni muweza wa kuhuisha wafu?” (75:40). “Na katika ishara zake ni kuwa amekuumbieni wake zenu katika jinsi yenu ili mpate utulivu kwao, naye amejaalia mapenzi na huruma baina yenu. Bila shaka katika haya ziko alama (za kuwepo Allah) kwa watu wanaofikiri” (30:21)(iv) Tofauti ya Lugha, Rangi, Makabila, Mataifa “Na katika ishara zake (za kuonyesha kuwepo kwake na uwezo wake) ni kuumba mbingu na ardhi na kuhitalifiana lugha zenu na rangi zenu. Kwa yakini katika haya zimo ishara kwa wenye ujuzi” (30:22). “Enyi w atu! Kwa hakika tumekuumbeni (nyote) kw a (yule) mw anamume (mmoja Adam) na (yule) mwanamke (mmoja Hawwa). Na tumekufanyeni mataifa na makabila (mbali mbali) ili mjuane (tu basi). Hakika aheshimiwaye sana miongoni mw enu mbele ya Allah ni yule amchaye Allah zaidi katika nyinyi. Kwa yakini Allah ni Mjuzi Mwenye habari (za mambo yote).” (49:13)(v) Umbo na Sura “Ewe mwanaadamu! Nini kikudanganyacho na Mola wako Mtukufu (hata ukamkanusha). Aliyekuumba na akakutengeneza, kisha akakulinganisha sawasawa. Katika sura yoyote aliyoipenda amekutengeneza ”. “Na katika umbo lenu na katika viumbe alivyovitawanya zimo alama kwa watu wenye yakini.” (45:4)(vi)Chakula cha Mwanaadamu “Hebu mwanaadam na atazame chakula chake. Hakika Sisi tumemimina maji kwa nguvu (kutoka maw inguni).Tena tukaipasuapasua ardhi.Kisha Tukaotesha humo (vyakula vilivyo) chembe chembe. Na mizabibu na mboga. Na mizeituni na mitende.Na mabustani, (mashamba) yenye miti iliyosongamana barabara.Na matunda na malisho.Kwa ajili ya kukustarehesheni nyinyi na wanyama wenu. (80:24-32)(vii)Ufanyaji kazi wa viungo vya ndani na nje ya mwili wa Mwanaadamu


“Basi uelekeze uso wako katika dini iliyo sawasawa - ndilo umbile Mwenyezi Mungu alilowaumbia watu; (yaani dini hii ya Kiislamu inawafikiana barabara na umbo la binaadamu).Hakuna mabadiliko katika maumbile ya viumbe vya Mw enyezi Mungu. Hiyo ndiyo dini iliyo haki, lakini w atu w engi haw ajui.” (30:30) “Na katika ishara zake ni kulala kwenu usiku na kuamka mchana na kutafuta fadhila Yake. Hakika katika hayo zimo ishara kwa wenye kusikia.(30:23)
Mwanadamu japo analala kila siku, hajui chanzo cha usingizi. Mtu anapokuwa usingizini hajui chochote kinachoendelea, Je! ni nani anayeleta usingizi na kuuondoa?(ix) Mwanadamu kumkumbuka Allah (s.w) wakati wa matatizo“Sema: Ni nani anayekuokoeni katika viza (taabu) vya bara na baharini? Mnamuomba kwa unyenyekevu na kwa sauti ndogo (mnasema): Kama akituokoa katika (baa) hii bila shaka tutakuwa miongoni mwa wanaoshukuru (6:63)
Hata Fir’auni, aliyetakabari sana kiasi cha kudai kuwa yeye ni mkubwa kuliko Allah, alimkumbuka Mola wake pale alipokabiliwa barabara na matatizo.“Na tukawapitisha wana wa Israel katika bahari, na Firauni na majeshi yake wakawafuata kwa dhulma na jeuri. Hata kulipomfikia Fir’aun kuzama alisema, “Naamini kwamba hakuna aabudiw aye kwa haki ila yule wanayemuamini wana wa Israel na mimi ni miongoni mwa wanaotii”. (10:90)
                   
           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2018-08-01     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 328


Download our Apps
👉1 Madrasa kiganjani     👉2 Kitau cha Fiqh     👉3 kitabu cha Simulizi     👉4 Kitabu cha Afya    

Post zifazofanana:-

KAZI ZA MALAIKA
Malaika wamepewa kazi ya kumtumikia Allah(SW) kwa kumtukuza na kumtakasa, kama wanavyosema wenyewe:Hakuna yoyote miongoni mwetu ila anapo mahali pake mahususi. Soma Zaidi...

Uovu wa kumzulia Muumini Uzinifu na Maovu mengine na Hukumu dhidi ya Wazuaji
Kumzulia mtu mtwahirifu kuwa amefanya tendo la zinaa pasina kuleta ushahidi stahiki ni tendo ovu mno mbele ya Allah (s. Soma Zaidi...

Ni Ipi Elimu yenye manufaa
Elimu inaweza kugawanyika katika makundibmrngine mawili ambayo ni elimu yenye manufaa na elimubisiyi na manufaa Soma Zaidi...

Udhaifu wa mtazamo wa makafiri juu ya dini dhidi ya mtazamo wa uislamu
Somo Hili linaeleza kuhusu mtazamo wa uislamu juu ya dini (EDK form2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

Mgawanyiko wa Elimu katika mtazamo wa Uislamu
Katika Uislamu elimu imegawanyika katika Elimu ya muongozo na elimu ya mazingira. Soma Zaidi...

Kwanini Uislamu Ndio Dini Pekee Inayostahiki Kufuatwa na Watu?
Soma Zaidi...

Kujielimisha kwa Ajili ya Allah (s.w).
Elimu ndiyo zana aliyotunukiwa mwanadamu ili aitumie kutekeleza majukumu yake kama Khalifa wa Allah (s. Soma Zaidi...

jamii muongozo
Haja ya Mwongozo kutoka kwa Allah (s. Soma Zaidi...

KUAMINI MALAIKA WA ALLAH (S.W.)
Soma Zaidi...

Sifa za waumini zilizotajwa katika surat ash-Shuura
“Basi vyote hivi mlivyopewa ni starehe ya maisha ya dunia tu, lakini kilicho kwa Mwenyezi Mungu ni bora na cha kudumu (milele). Soma Zaidi...

NGUZO ZA IMAN
Jifunze tawhid yaani kumpwekesha Allah subhaanah wata'aala Soma Zaidi...

Dalili Kubwa za kukaribia Siku ya kiama
Soma Zaidi...