image

NGUZO ZA IMANI

Tunajifunza katika Qur-an na hadithi sahihi kuwa Imani ya Kiislamu imejengwa juu ya nguzo sita zifuatazo:1 Kumuamini Allah (s.

NGUZO ZA IMANI

NGUZO ZA IMANI


Tunajifunza katika Qur-an na hadithi sahihi kuwa Imani ya Kiislamu imejengwa juu ya nguzo sita zifuatazo:
1 Kumuamini Allah (s.w).2 Kuamini Malaika wake.3 Kuamini Vitabu vyake.4 Kuamini Mitume wake.5 Kuamini Siku ya mwisho.6 Kuamini Qadar yake.
Hawi Muumini wa Kiislam yule ambaye amekanusha angalau moja ya nguzo hizi kama inavyobainika katika Qur-an:
“... Na mwenye kumkanusha Allah (s.w) na Ma la ika wake na Vitabu vyake na Mitume wake na siku ya mwisho., basi bila shaka amepotea upotofu ulio mbali (kabisa)” (4:136)Mtu hatakuwa Muumini kwa kutamka tu hizi nguzo sita, bali pale atakapozijua kwa undani na kuendesha maisha yake yote kwa misingi ya nguzo hizi.Tunazifahamu nguzo hizi sita kutokana na Hadith ya Mtume (s.a.w) iliyosimuliwa na Umar (r.a) kama ifuatavyo:Siku moja tulipokuwa tumeketi pamoja na Mtume (s.aw.) alitutokea mtu mmoja ambaye nguo zake zilikuwa nyeupe kama theluji na nywele zake nyeusi sana, hakuwa na dalili zozote za msafiri, ingawa alikuwa mgeni kwetu sote.


Halafu alikaa mbele ya Mtume (s.a.w) hali magoti yake yakikabiliana na yale ya Mtume na akaweka mikono yake katika mapaja ya Mtume na akasema:”Ewe Muhammad nifahamishe juu ya Uislamu ” na Mtume akasema ; “Ni kushuhudia ya kuwa hakuna apasaye kuabudiwa kwa haki ila Allah, Kusimamisha swalaa, kutoa Zakat, Kufunga Mwezi wa Ramadhani, Kuhiji Makkat kwa mwenye kuweza” Halafu yule mgeni akasema “umesema kweli”. Tukastaajabu kwa nini aliuliza halafu akasadikisha.


Halafu akasema; “Nifa ham ishe juu ya Iman ”. Mtume akasema : “Ni kumuamini Mwenyezimungu na, Ma la ika wake , Vitabu vyake, Mitume wake, Siku ya Mwisho na Qadar, Kheri na shari yake.


Kisha akasema nifahamishe juu ya Ihsaan” Akasema “Ni Kumuabudu Allah kama kwamba unamuona, ikiwa wewe humuoni yeye anakuona ” Halafu akasema nifahamishe juu ya Kiyama ” Akasema: “Hajui mwenye kuulizwa juu ya hilo zaidi ya mwenye kuuliza.


Akasema “Nifahamishe dalili zake. Mtume akasema: “Ni wakati ambapo mjakazi atamzaa bibi yake, na utakapowaona wachungaji masikini wanaposhindana kujenga maghorofa. “Yule mgeni alipoondoka, Mtume alikaa kimya kwa muda kisha akasema: “eweUmar, unamfahamu muulizaji?’ Sote tukamjibu kuwa Allah na Mtume wake wanajua zaidi. Mtume akasema “Huyo ni Jibriil amekuja kuwafundisheni dini yenu” (MUSLIM)
                   
           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2018-08-01     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 938


Download our Apps
👉1 Madrasa kiganjani     👉2 kitabu cha Simulizi     👉3 Kitau cha Fiqh     👉4 Kitabu cha Afya    

Post zifazofanana:-

Mafundisho ya Mitume
Mafundisho ya mitume ni eneo lingine linalo thibitisha kuwepo Allah (s. Soma Zaidi...

Sifa za waumini zilizotajwa katika surat Al-Anfal (8:2-4) na Al-Hujurat
"Hakika wanaoamini kweli ni wale ambao anapotajwa Allah nyoyo zao hujaa khofu; na wanaposomewa aya zake huwazidishia imani na wanamtegemea Mola wao tu basi. Soma Zaidi...

KUAMINI SIKU YA MALIPO
Soma Zaidi...

Maisha ya Mitume
Soma Zaidi...

Maana ya muislamu.
Kwenye kipengele hichi tutajifunza ni nani muislamu. Soma Zaidi...

Kutopupia dunia
"Ewe mwanangu! Soma Zaidi...

Historia ya Mwanadamu
Soma Zaidi...

Elimu Yenye Manufaa
Kwenye kipengele hiki tutajifunza elimu yenye manufaa kwenye jamii na pia tutajifunza sifa za elimu yenye manufaa. Soma Zaidi...

Kuongea na Allah (s.w) nyuma ya Pazia
Hii ni njia ambayo mwanaadamu huongeleshwa moja kwa moja na Allah (s. Soma Zaidi...

Kwanini mwanadamu hawezi kuishi bila ya dini?
Mtazamo wa uislamu juu ya dini (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

Sifa za waumini zilizotajwa katika surat ash-Shuura
“Basi vyote hivi mlivyopewa ni starehe ya maisha ya dunia tu, lakini kilicho kwa Mwenyezi Mungu ni bora na cha kudumu (milele). Soma Zaidi...

Kumuamini malaika wa mwenyezi Mungu
Nguzo za Imani (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...