image

Nafasi ya Elimu na wenye elimu katika Uislamu

Nafasi ya elimu na mwenye elimu katika uislamu inaonkana katika maeneo yafuatayo: Kwanza, Elimu ndio takrima ya kwanza aliyokirimiwa mwanaadamu na Mola wake.

Nafasi ya Elimu na wenye elimu katika Uislamu

Nafasi ya Elimu na wenye elimu katika Uislamu



Nafasi ya elimu na mwenye elimu katika uislamu inaonkana katika maeneo yafuatayo:
Kwanza, Elimu ndio takrima ya kwanza aliyokirimiwa mwanaadamu na Mola wake.Tunajifunza katika Qur-an kuwa jambo la kwanza alilotunukiwa Adam (a.s) mara tu baada ya kuumbwa kwake ni kupewa elimu.


“Na (Mwenyezi Mungu) akamfundisha Adam majina ya vitu vyote...” (2:3 1)
“Majina ya vitu vyote” katika aya hii inaashiria fani zote za elimu ambazo anahitajia mwanaadamu hapa duniani ili afikie kwa ufanisi lengo la kuumbwa kwake. Pia tunajifunza katika Quran kuwa mwenye elimu na hekima amepewa kheri nyingi.


(Mungu ) humpa hikma amtakaye, na aliyepewa hikma bila shaka amepewa kheri nyingi. Na hawakumbuki ila wenye akili. (2.269).
Kutafuta elimu (kusoma) ni amri ya kwanza kwa mwanaadamu. Tunajifunza kutokana na historia ya kushushwa Qur-an kuwa Wahay wa kwanza kumshukia Mtume (s.a.w) ambao ndio ulimtawazisha rasmi kuwa mtume ni ule unaopatikana katika aya tano za mwanzo za Suratul-’Alaq:


“Soma kwa jina la Mola wako aliyeumba.Ambaye amemuumba mwanaadamu kwa ‘Alaq (kitu chenye kuning’inia). Soma na Mola wako ni karimu sana. Ambaye amemfundisha mwanaadamu kwa kalamu. Amemfundisha mwanaadamu (chungu ya) mambo aliyokuwa hayajui”.(96:1-5)
Kutokana na aya hizi, kwa muhtasari, tunajifunza yafu atayo:



1. Kusoma kwa ajili ya Mwenyezi Mungu ni jambo la kwanza waliloamrishwa wanaadamu na Mola wao.



2. Kusoma kwa jina la Mola wako ni kusoma kwa ajili ya kutafuta radhi za Mwenyezi Mungu au ili kuweza kumwabudu Allah(s.w) inavyostahiki na kusimamisha Uislamu katika jamii.



3. Radhi za Mwenyezi Mungu zitapatikana pale mwanaadamu atakapoweza kufikia lengo la maisha yake la kumuabudu Allah (s.w) kwa kuzingatia maamrisho na mipaka ya Mwenyezi Mungu katika kila kipengele cha maisha.



4. Amri hii ya kusoma hailengi fani maalum tu ya elimu; bali kila fani itakayomuwezesha mwanaadamu kufikia lengo la maisha yake kwaufanisi.



5. Chanzo au chimbuko la fani zote za elimu ni Allah (s.w). Hivyo kwa Muislam mlango wa kwanza wa elimu ni kusoma kwa mazingatio Qur-an na hadithi sahihi za Mtume (s.a.w) na kusoma maarifa ya Uislamu kwa ujumla kutokana na vyanzo hivi viwili.




                   






           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 904


Sponsored links
👉1 Kitabu cha Afya     👉2 kitabu cha Simulizi     👉3 Madrasa kiganjani     👉4 Kitau cha Fiqh    

Post zifazofanana:-

kuwa muaminifu na kuchunga Amana
Uaminifu ni uchungaji wa amana. Soma Zaidi...

Dua sehemu 03
Zijuwe njia ambazo Allah hujibu Dua yako. Tambua kama umejibiwa dua yako au bodo, soma darsa za dua hapa. Soma Zaidi...

DUA 120
Soma Zaidi...

DUA 61 - 84
61. Soma Zaidi...

DUA DHIDI YA WASIWASI, UCHAWI NA MASHETANI
DUA ZA KUONDOA WASIWASI, SIHIRI NA UCHAWI 1. Soma Zaidi...

Al-Arba'uwn An-Nawawiyyah hadithi ya 1: Nia
huu ni mwanzo wa kitabu hiki cha Matn arbaina Naway Soma Zaidi...

HUU NDIO USIA WA MTUME KWA WAISLAMU
عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ أَنَّ رَجُلًا قَالَ لِلنَّبِيِّ صلى الله عليه و سلم أَوْصِنِي. Soma Zaidi...

Maana ya dua na fadhila zake
Dua ni moja ya Ibada ambazo tunatakiwa kuziganya kila siku. Kuna fadhila nyingi sana za kuomba dua. Post hiibitakwenda kukujuza fadhila za kuomba dua. Soma Zaidi...

DUA 41 - 50
41. Soma Zaidi...

DUA 51 - 60
51. Soma Zaidi...

KUKUSANYIKA KATIKA DUA
KUKUSANYIKA KATIKA DUA. Soma Zaidi...

UHAKIKI WA HADITHI
Uhakiki wa Hadith za Mtume (s. Soma Zaidi...