Kwanini Uislamu umeipa Elimu nafasi ya kwanza?

Kwanini Uislamu umeipa Elimu nafasi ya kwanza?

Kwanini Uislamu umeipa Elimu nafasi ya kwanza?


Elimu imepewa nafasi ya kwanza katika Uislam kwa sababu zifu atazo:
Kwanza, elimu ndio nyenzo pekee inayomuwezesha mwanaadamu kumtambua Mola wake vilivyo na kumuabudu ipasavyo kwa unyenyekevu kama Qur-an inavyothibitisha:



โ€œ... Kwa hakika wanaomuogopa Mwenyezi Mungu miongoni mwa waja wake ni wale wataalam (waliozama katika fani mbali mbali)โ€ (35:28).


Pili, elimu iliyosomwa kwa mrengo wa Qur-an ndio nyenzo pekee inayomuwezesha mwanaadamu kuwa Khalifa wa Allah (s.w) hapa Ulimwenguni. Khalifa ni mja anayetawala ulimwengu kwa niaba ya Allah (s.w) kwa kufuata kanuni na sheria zake. Nabii Adam (a.s) aliwathibitishia Malaika kuwa ana uwezo wa kuutawala ulimwengu kwa niaba ya Allah (s.w) baada ya kuelimishwa fani zote za elimu (majina ya vitu vyote) na kuahidiwa mwongozo kutoka kwa Allah (s.w).



Tatu, kutafuta elimu ni Ibada maalumu ya hali ya juu kuliko Ibada zote. Kwa mujibu wa Qur-an Swala ni Ibada maalumu ya hali ya juu na ni dhikri kubwa au zingatio kubwa juu ya Allah (s.w)


โ€œโ€ฆ Hakika swala humzuilia (mja) na mambo machafu na maovu na ni dhikri kubwa kwa Allah (s.w)โ€ (29:45).



Pia katika Hadith Mtume (s.a.w) amesisitiza: โ€œNguzo kubwa ya Dini (Uislamu) ni swala, mwenye kusimamisha swala kasimamisha Dini na mwenye kuacha sw ala kavunja Dini.โ€
Hivyo kwa mujibu wa Qur-an na Hadith sahihi za Mtume (s.a.w), swala ni Ibada yenye hadhi ya juu kuliko Ibada zote mbele ya Allah (s.w); lakini bado Ibada ya kutafuta elimu inachukuwa nafasi ya juu zaidi kuliko swala kwani swala haiwezi kusimama bila ya kuwa na ujuzi stahiki.
Nne, mwenye elimu ananafasi bora ya kumuabudu Mola wake inavyostahiki katika kila kipengele cha maisha yake kama inavyosisitizwa katika Qur-an:


โ€œ... Kwa hakika wanaomuogopa Mwenyezi Mungu miongoni mwa waja wake ni wale wataalamuโ€ฆโ€ (35:28)
Pia Qur-an inasisitiza juu ya umuhimu wa elimu kwa kuuliza:


โ€œโ€ฆ Je, waweza kuwa sawa wale wanaojua na wale wasiojua? Wanaotanabahi ni wale wenye akili tu.โ€ (39:9)
Kimsingi wanaojua wanatarajiwa wafanye mambo kwa ufanisi zaidi kuliko wasiojua. Kwa msingi huu Allah (s.w) anasisitiza tena katika aya ifuatayo:



โ€œMwenyezi Mungu ataw ainua (daraja) w ale w alioamini miongoni mwenu, na waliopewa elimu watapata daraja zaidi. Na Mwenyezi Mungu anazo habari za mnayoyatenda yoteโ€ฆโ€ (58:11)
Hivyo, kutokana na aya hizi (35:28, 39:9 na 58:11) tunajifunza kuwa waumini wenye elimu wana daraja zaidi kuliko waumini wengine kwa sababu wanao uwezo zaidi wa kuona dalili za kuwepo Allah (s.w) na utukufu wake kwa undani zaidi, jambo ambalo huwapelekea kumuogopa Mola wao na kumuabudu inavyostahiki katika kukiendea kila kipengele cha maisha yao kama inavyobainika katika aya zifuatazo:


โ€œKatika kuumbwa mbingu na ardhi na mfuatano wa usiku na mchana, ziko hoja (za kuonesha kuw epo Allah (s.w) kwa wenye akili. (3:190)


Ambao humkumbuka Mw enyezi Mungu w akiwa wima, wakiwa wamekaa na wakiwa wamelala. Na hufikiri (tena) umbo la mbingu na ardhi (wakasema) Mola wetu! Hukuviumba hivi burebure tu. Utukufu ni wako. Basi tuepushe na adhabu ya moto.โ€ (3:190).
Pia kutokana na aya hizo tunajifunza kuwa waumini wenye elimu wanao uwezo mkubwa wa kufanya mambo kwa ufanisi jambo litakalowapelekea kusimamisha ukhalifa wa Allah (s.w) katika jamii.




                   


Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 1970-01-01 03:33:44 Topic: Tawhid Main: Dini File: Download PDF Views 1950

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
๐Ÿ‘‰1 Kitabu cha Afya    ๐Ÿ‘‰2 Bongolite - Game zone - Play free game    ๐Ÿ‘‰3 kitabu cha Simulizi    ๐Ÿ‘‰4 Madrasa kiganjani    ๐Ÿ‘‰5 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)    ๐Ÿ‘‰6 Kitau cha Fiqh   

Post zinazofanana:

Kuwa wenye shukurani mbele ya Allah (s.w)

Mwanaadamu ametunukiwa neema mbali mbali na Mola wake kuliko viumbe wengine wote kama tuanvyojifunza katika aya mbali mbali za Qur'an.

Soma Zaidi...
Mtazamo wa uislamu juu ya dini

Kwenye kipengele hichi tutajifunza mitazamo ya kikafiri juu ya dini.

Soma Zaidi...
ALAMA YA MUUMINI WA UKWELI KATIKA UISLAMU

ุนูŽู†ู’ ุฃูŽุจููŠ ู‡ูุฑูŽูŠู’ุฑูŽุฉูŽ ุฑูŽุถููŠูŽ ุงู„ู„ู‡ู ุนูŽู†ู’ู‡ู ุฃูŽู†ูŽู‘ ุฑูŽุณููˆู„ูŽ ุงู„ู„ูŽู‘ู‡ู ุตู„ู‰ ุงู„ู„ู‡ ุนู„ูŠู‡ ูˆ ุณู„ู… ู‚ูŽุงู„ูŽ: "ู…ูŽู†ู’ ูƒูŽุงู†ูŽ ูŠูุคู’ู…ูู†ู ุจูุงูŽู„ู„ูŽู‘ู‡ู ูˆูŽุงู„ู’ูŠูŽูˆู’ู…ู...

Soma Zaidi...
Ni nini maana ya Ilhamu katika uislamu?

Ilhamu ni moja katika njia ambazo Allah huwasiliana na wanadamu na kuwafundisha mambo mablimbali.

Soma Zaidi...
Kujiepusha na kukaribia zinaa

Si zinaa tu iliyoharamishwa bali hata yale yote yanayotengeneza mazingira na kuchochea kufanyika kwa zinaa nayo pia yameharamishwa.

Soma Zaidi...
Nafsi ya mwanadamu inavyothinitisha uwepo wa Allah

Mwanadamu ukifikiria vyema. Kuhusu nafsi yako, hakika utapatabfikra yabuwepp wa Mwenyezi Mungu

Soma Zaidi...
Jifunze ni kwa namna gani Malaika waliweza kuwasiliana ana manabii Malimbali

Wakatibmeingibe Allah anapotaka kuwasiliana na wanadamu hutuma Malaika wake.

Soma Zaidi...
mitume

Labda itaulizwa: Kwanini Mtume Muhammad (s.

Soma Zaidi...
Ni lipi lengo la Elimu katika yislamu?

Ni lipi lengo kuu la Elimu katika uislamu (Edk form 1 Dhanaya Elimu)

Soma Zaidi...