Hizi ni Dua ambazo unatakiwa uziombe wakati wa shida na taabu
DUA ZA WAKATI WA SHIDA
1.Dua ya wakati wa taabu
“LAA ILAAHA ILLA-LLAHUL-’ADHIMUL-HALIIMU. LAA ILAAHA ILLA LLAHU RABBULS-SAMAAWATI WARABBUL-ARDHI WARABBUL-’ARSHIL-’KARIIM” (Bukhari)
2.Dua pindi uonaposhetani au unapotishwa na shetani
Ikitokea Mtu ameona shetani au ametishwa na shetani anatakiwa kuleta isti’adha na asema “A’UDHU BILLAHI MINKA” mara tatu kisha aseme “AL’ANUKA BILA’ANATIL-LLAHI TAAMMAH” mara tatu. Hakika shetani anakimbia ukisema maneno hayo. Hatika mapokezi ukimuona shetani akikutisha au hakukutisha soma adhana hakika shetani hukimbia adhana. Katika hadithi alopokea muslim mtume (s.a.w) amesema “hakika shetani hukimbia pindi adhana ya swala inaposomwa”
3.pindi muislamu anapokutana na jambo ambalo halitaki.
Pindi Muislamu anapoutana na jambo ambalo halitaki au jambo baya litakalomuhuzunisha anatakiwa aseme: “QADDARALLAHU WAMAA SHAA-A FA’ALA” na katu asiseme lau.… Yaani lau nisingelifanya hivi lisingenikuta au mifano kama haya. Kwani kusema hivi hufungua milango ya shetani (Muslim na Nisai)
4.pindi muislamu anapopatwa na shaka
Itakapotokea Mtu anashaka katika nafsi yake juu ya jambo anatakiwa aseme: “HUWAL-AWALU WAL-AKHIRU WADHAHIRU WAL BAATWINU WAHUWA BIKULLI SHAY-IN ‘ALIIM” (Abu Daud amepokea adithi hii na sanadi yake ni sahihi)
5.anapopata Muislamu msiba
Msiba ni katika mambo yanayohuzunisha moyo. Msiba sio pekeake kifo hata ukipotelewa na kitu pia ni msiba. Hivyo inapotokea hali kama hii ya kuhuzunisha moyo useme:”INNAA LILLAHI WA INNAA ILAYHIR-RAJI’UUN” Allah amesema kuwa “wape habari njema za furaha wenye subira, ambao wanapopata msiba husema ”INNAA LILLAHI WA INNAA ILAYHIR-RAJI’UUN”
6.Dua pindi unapokasirika.
Mtume (s.a.w) amekataza sana kuwa na tabia ya kukasirika na ni katika usia alokuwa akiwaba masahaba zake. Pindi mtu anapokasirika Mtume amesema anatakiwa aseme: “A’UDHU BILLAHI MINASH-SHAITWAANIR-RAJIIM” hadithi hii ni sahihi.(Bukhari na Muslim).
7.Dua unapokutana na adui
Pindi unapokutana na adui wako kama kwenye vita ama sehemu nyingine iwe usiku ama mchana unatakiwa useme: “ALLAAHUMMA MUNZILAL-KITAABI WA MUJRISAHAABI WAHAAZIMAL-AHZAABI IHZIMHUM WANSUUNAA ‘ALAYHIM” hii dua aliiomba mtume alipokutana na Maadui zake kwenye vita vya Ahzab (Bukhari na Muslim)
8.Dua pindi unapohofia kiongozi
Ikitokea mtu anajambo na anataka kukutana na kiongozi, au amewekwa chini ya ulinzi na kiongozi jabari, muovu ama kwa namna ingine na akawa anahofu kukabiliana na kiongozi huyo anatakiwa aseme: “LAA ILAAHA ILLAAHUWAL-HALIIMUL-KARIIM,,SUBHAANALLAHI RABBIA-SAMAAWATIS-SAB-’I WARABBIL-’ARSHIL-’ADHIIMI. LAA ILAAHA ILLAA ANTA, ‘AZZA JAARUKA WAJALLA THANAAUKA” amesimulia hadithi hii Ibn “Umar.
Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.
Download NowJe umeipenda post hii ?
Post hii itakueleza ni dua gani unatakiwa uzisome wakati unapokiwa na hasira ama pale unapokasirika.
Soma Zaidi...Sunnah na hadithi (EDK form 3: dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...DUA Kwa ufupi dua ni kumuomba Allah akuondoshee lililobaya, ama linalo kuudhi ama akupe jambo fulani.
Soma Zaidi...Post hii itakufundisha maana ya neno sunnah katika Uislamu. Pia utajifunza maana ya neno hadithi katika uislamu
Soma Zaidi...عَنْ أَبِي مَسْعُودٍ عُقْبَةَ بْنِ عَمْرٍو الْأَنْصَارِيِّ الْبَدْرِيِّ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عل?...
Soma Zaidi...Soma dua mbalimbali za kila siku ambazo unatakiwa uzijuwe. Dua 120 ambazo muislamu anatakiwa kuzijua
Soma Zaidi...