Fahamu kuhusu dawa ya griseofulvin

Post hii inahusu zaidi dawa ya griseofulvin ni dawa inayotumika kutibu fangasi za kwenye ngozi ambazo usababisha mabaka mabaka kwenye ngozi.

Fahamu kuhusu dawa ya griseofulvin .

1. Kama tulivyoona hapo mbele kuhusu dawa ya griseofulvin ni dawa inayotumika kutibu ugonjwa wa fangasi za kwenye ngozi, kwa kawaida kwenye ngozi kunakuwepo na maambukizi ya aina mbalimbali za fungasi kwa hiyo ni vizuri kabisa kutumia dawa hii kwa usahihi kabisa kadri ya wataalamu wa afya.

 

2. Kwa kawaida dawa hii utumika kwenye ngozi na kiwango cha kufanya kazi ni kikubwa kwa hiyo uzuia maambukizi kwenye ngozi, kwa hiyo kuanzia mda ulioanza kutumia na matokeo ya kupona yanaweza kuonekana kuanzia wiki ya pili mpaka wiki ya sita kwa upande wa ngozi, pia kwa upande wa ngozi ya kichwa na penyewe dawa hizi utumika na pia kupona utegemeza kuanzia wiki ya pili mpaka wiki ya sita hivi.

 

3. Pia dawa hii ya griseofulvin haitumiki kwenye ngozi ya kawaida na kwenye nywele tu bali usaidia pia kwenye kwenye maambukizi ya kucha na kwa hiyo kama kucha zimeharibiwa na wadudu usaidia kuua wadudu hao na kufanya kucha kutwa nzuri na za kuvutia, kwa wenye shida ya matatizo ya kwenye kucha tiba yake uenda kwa utaratibu na hatimaye kucha zinajirudia na kuwa kawaida.

 

4. Dawa hii ufanya kazi kwa kuzuia kazi ya enzyeme ambayo kwa kitaalamu huitwa cytochrome p450 ni enzyeme ya mdudu ambaye usababisha kuwepo kwa fangasi kwenye ngozi na kwenye kucha, kwa hiyo dawa ya griseofulvin uenda kuharibu kazi ya mdudu huyu na kusababisha kupona kwa mgonjwa.na pia dawa hii uzuia kutengenezwa kwa polymerization of nucleic acids ambayo usababishwa na mdudu anayesababisha fangasi kwenye ngozi na kwenye kucha.

 

5. Kwa hiyo dawa hii haipaswi kutumiwa na wale wenye aleji na griseofulvin na pia kutumia dawa hii ni vizuri kutumia kwa ushauri wa wataalamu wa afya hairuhusiwi kutumika kiholela hohlela.

 

6. Pia dawa ina maudhi ambayo yanaweza kutokea kwa watumiaji ambayo ni pamoja na maumivu ya kichwa ya mara kwa mara wakati wa kutumia, hali hiyo ni kawaida ila maumivu yalizidi onana na wataalamu wa afya.Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2022/12/15/Thursday - 01:05:47 pm     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 1889


Download our Apps
👉1 Madrasa kiganjani     👉2 Kitabu cha Afya     👉3 Kitau cha Fiqh     👉4 kitabu cha Simulizi    

Post zifazofanana:-