Post hii inahusu zaidi dawa ya furosemide ni mojawapo ya dawa ambayo ipo kwenye kundi la diuretics na kwa jina linguine huitwa lasix
Ifahamu dawa ya furosemide.
1. Kama tulivyoona hapo mwanzoni dawa ya furosemide ni mojawapo ya dawa ambayo imo kwenye kundi la diuretics, dawa hii ni maarufu kwa kuzalisha mkojo na kusababisha sumu kuondoka kwenye mwili na kusababisha moyo kufanya kazi yake kawaida, na pengine dawa hii utolewa kwa wagonjwa hata wasio na tatizo la moyo kabla ya kuwawekea damu, kwa hiyo ni dawa inayosaidia Sana kwenye matibabu.
2. Dawa hii pia ufanya Kazi haraka inapotolewa kwa kupitia kwenye mishipa ya damu na ndani ya saa moja inakuwa imeshaanza kufanya kazi kwenye mwili wa binadamu. Tunafahamu kabisa kwamba kama Kuna kiwango kikubwa cha chumvi kwenye damu usababisha matatizo mbalimbali hasa kwa wagonjwa wa moyo, kwa hiyo kwa matumizi ya furosemide uhakikisha chumvi hiyo inatolewa kwenye moyo kwa kuhakikisha kwamba mgonjwa anakojoa ,kwa hiyo dawa hii ufanya Kazi kupitia kwenye Figo, na kwa kupitia katika hali ya kutoa mkojo usababisha sumu kutolewa mwilini.
3. Vile vile dawa hii huwa na maudhi madogo madogo wakati wa kutumia ,na sio maudhi tu dawa hii upunguza kiwango cha madini mwilini,na vile kuongeza kiwango cha sukari mwilini kwa hiyo kwa watumiaji wa dawa hii wanapaswa kuwa makini hasa wale wenye tatizo la sukari kupanda, na pia wale wenye tabia ya kupungukiwa na madini wanapaswa kuwa makini pindi watumiapo dawa hii, au kama Kuna tatizo kubwa kwa wagonjwa wa sukari na wenye upungufu wa madini ni vizuri kabisa kutumia dawa chini ya uangalizi maalumu.
4. Kwa hiyo dawa hii inawezekana kutumiwa na watu mbalimbali ila wale wenye tatizo la sukari ya kupanda na wenye tatizo la upungufu wa madini wanapaswa kuitumia kwa utaratibu wa wataalamu wa afya, na vile dawa hii haipaswi kutumiwa kiholela Bali utumika kulingana na wataalamu wa afya.
Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.
Download NowUmeionaje Makala hii.. ?
Post hii inahusu zaidi dawa ya sulphonamide ni mojawapo ya dawa ambayo usaidia kutibu magonjwa mbalimbali yanayosababishwa na bakteria ni dawa au antibiotics ya mda mrefu na pia matumizi yake sio makubwa sana kwa sababu ya kuwepo kwa antibiotics zenye ngu
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi kundi la diuretics,ni kundi mojawapo kati ya makundi ya dawa zinazosaidia katika matibabu ya magonjwa ya moyo.
Soma Zaidi...PID ni mashambulizi ya bakteria kwenye mfumo wa uzazi kwa wanawake. Hapa nitakujulisha dawa
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi dawa ya epinephrine kwa kutuliza aleji ni dawa ambayo imependekezwa kutuliza aleji kama dawa ya hydrocortisone, Prednisone hazipo au zimeshindwa kufanya kazi.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi dawa ya amoxline .jinsi inavyofanya kazi mwilini.pamoja na matumizi yake.
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi aina mojawapo ya dawa ya penicillin ambayo ufanya kazi kwa mda mrefu, dawa hii kwa kitaamu huiitwa procaine benzyl penicillin.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi dawa ya Albendazole katika kutibu Minyoo, ni Aina mojawapo ya dawa ambayo usaidia kutibu Minyoo inayosababishwa na bakteria mbalimbali.
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi dawa ya propranolol katika matibabu ya magonjwa ya moyo, dawa hii ipo kwenye kundi la beta blockers na ufanya Kazi mbalimbali hasa kwa wagonjwa wa moyo.
Soma Zaidi...