Post hii inahusu zaidi kundi la diuretics,ni kundi mojawapo kati ya makundi ya dawa zinazosaidia katika matibabu ya magonjwa ya moyo.
Fahamu kuhusu kundi la diuretics.
1. Diuretics ni mojawapo ya kundi kwenye dawa za kutibu magonjwa ya moyo,kundi hili pia Lina dawa mbalimbali ambazo utumika kwenye matibabu, kundi hili la dawa ni kuzalisha mkojo Ili kuweza kutoa sumu mwilini ambazo ni chanzo cha kusababisha kuwepo au kuongezeka kwa tatizo kwenye moyo.
2. Dawa hizi ambazo zipo kwenye Kundi hili la diuretics zikitumika uweza kufanya kazi kupitia kwenye Figo na baadae kuongeza kiwango cha kuzalishwa kwa mkojo , kwa hiyo baada ya kutolewa mkojo nje uweza kusababisha moyo kuendelea na kazi yake kama kawaida,kwa sababu sumu utoka nje kupitia kwenye mkojo.
3. Dawa hizi kwenye kundi la diuretics ni pamoja na furosemide, bendofurothiazide, potassium sparing diuretics- spirolactone na amiloride hizi dawa ni kutokana na kundi Moja la diuretics lakini ufanya Kazi tofauti tofauti kutegemea na tatizo la mgonjwa.
4. Vili vile dawa hizi huwa na maudhi madogo madogo katika matumizi na maudhi hayo ni pamoja na kukojoa sana au pengine kizunguzungu na kutapika hasa kwa watumiaji ambayo wanaaoanza kutumia dawa,pia dawa hizi zina tabia ya kupandisha sukari juu ,kwa hiyo wenye tatizo la ugonjwa wa kisukari hasa ya kupanda wanapaswa kuwa makini katika matumizi ya dawa hii.
5. Vili vile kwa sababu dawa hii Inafanya mtu akojoe sana Ina tabia vile vile ya kupunguza madini mwilini kwa sababu madini mengi upitia kwenye mkojo na kutolewa nje, kwa hiyo ni vizuri na kuwa makini kwa wale wenye tatizo la upungufu wa madini mwilini.
6. Vile vile dawa hizi zinapaswa kutumiwa kadri ya wataalamu wa afya sio kuzitumia kiholela na pia watu wenye tatizo la kisukari hasa ya kupanda na wale wenye tatizo la upungufu wa madini mwilini wanapaswa kuwa macho katika matumizi.
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetuUmeionaje Makala hii.. ?
Posti hii inahusu zaidi faida za dawa za NMN maana yake ni Nicotinamide mononucleotide ni dawa ambazo usaidia kutibu magonjwa mbalimbali kama vile.
Soma Zaidi...Nini kinasababisha maumivu ya tumbo chini ya kitovu?
Soma Zaidi...Post hii inahusu dawa za kifua kikuu ni dawa ambazo utumika kutibu kifua kikuu, kwanza kabisa kabla ya kuanza kufahamu dawa hizo ni vizuri kabisa kufahamu kifua kikuu nini hili kuweza pia kufahamu dawa zake.
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi dawa ya Rifampin kama dawa mojawapo ya kutibu kifua kikuu.
Soma Zaidi...PoPosti hii inahusu zaidi vyakula ambavyo unaweza kutumia iwapo umepata tatizo la kiungulia
Soma Zaidi...Post hii inahusu dawa ya kupambana na bakteria, hili kundi la fluoroquinolones lina dawa kuu mbili ambazo ni ciprofloxin na ofloxacin.
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi dawa ya kutibu au kutuliza maumivu, kwa majina huiitwa indomethacin ni dawa inayotumika kutuliza maumivu ya Kawaida.
Soma Zaidi...Nitakujuza dalili za UTI na dawa za kutibu UTI. Pia tutaona njia za kujikinga na UTI pamoja na dalili za UTI
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi dawa ya pyrantel pamoate ni dawa ambayo usaidia kutibu minyoo ambayo kwa kawaida ukaa kwenye utumbo mdogo.
Soma Zaidi...