HUDUMA YA KWANZA KWA ALIYEPATWA NA SHAMBULIO LA MOYO


hii ni hali ghafla inayopelekea moyo kutofanya kazi vyema ama kukimama kabisa. Hali hii ikitokea inaweza kupelekea ukosefu wa hewa ya oksijeni mwilini na hatimaye kuanza kuathiri ubongo. Ukikutana na mtu wa namna hii utambue kuwa anahitaji msaada wa haraka sana.Hakikisha unaomba msada wa kuwaishwa mgonjwa kituo cha afya. Mpunguzie nguo ili aweze kupata baridi. Muangalie vyema kama anaweza kupumua, kama hapumui ama anapata shida kupumua ana za kumfanyia huduma ya kwa nza ya CPR.1.mlaze mgonjwa kichalichali juu ya sehemu iliyo ngumu, isiwe sehemu inayobonyea kama kitandani


2.Punguza nguo zilizopo kifuani kwake, na kama ni mwanaume unaweza kumvua shati kabisa.


3.Bidua kidogo kichwa cake


4.Weke mkono wako wa mmoja juu ya mwengine, kisha iweka katikati ya chuchu za mgonjwa.


5.Anza kumbonyeza kifua chake kwa wastani wa mibonyezo 100 paka 120 kwa dakika moja. Yaani karibia mibonyezo miwili kwa dakika.


6.Hakikisha unabonyeza kwa nguvu mpaka uone kifua cha mgonjwa kinapanda na kuchuka kutokana na mibonyezo yako.


7.Usizidishe nguvu kupitiliza ukavunja mifupa ya mgonjwa.


8.Enelea kufanya hivi mpaka utakapoona mgonjwa anweza kupumua.


9.Muwahishe mgonjwa kituo cha afya baada ya kuanza kupumua.