Njia za kuzuia damu isiendelee kuvuja

Posti hii inahusu zaidi njia za kuzuia damu isiendelee kuvuja, ni njia ambazo utumika ikiwa kuna damu inavuja kwenye sehemu yoyote ya mwili,kwa hiyo tunaweza kutumia njia hizi ili kuepuka kuendelea kuvuja kwa damu.

Njia za kuzuia damu uendelea kuvuja.

1.Tumia nguvu nyingi kukandamiza sehemu ambayo inavuja, unaweza kutumia ngumi kama ni sehemu kubwa au kidole kama ni sehemu ambayo umechomwa na kitu chenye ncha kali.

 

2.Amsha sehemu iliyotumia, unapaswa kuinua juu ili kuweza kuuweka vizuri sehemu iliyovunjika.

 

3.Mpe matumaini mgonjwa na zungumza naye kila wakati ili mgonjwa asiweze kuzimia kwa sababu kitendo cha kuvuja damu kwa mda mrefu usababisha kuishiwa kwa damu na maji

 

4.Funika sehemu ambayo ina kidonda kama kimetokea ili kuweza kuzuia maambukizi kwenye kidonda hicho 

 

5.Hakikisha inamfanyia mgonjwa usafi ili kuzuia kuendelea kwa Maambukizi na kumfanya mgonjwa aendelee kuwa na matatizo mengine.

 

6.Ondoa tisu (nyamanyama, ama ngozingozi) ambazo zimeharibika (kupondeka, kukatikakatika) kwenye kidonda ili kuweza kuruhusu tisu nyingine ziweze kuingia na kupona kutakuwa rahisi kw hiyo hakikisha kila siku tisu zilizoharibika zinaondolewa.

 

7.Funga vizuri sehemu iliyoariabika ili kuweza kufanya uponyaji kuwa wa haraka.

 

8. Mpatie mgonjwa dawa ya kutuliza maumivu kama vile panadol, asprin na dawa nyingine za maumivu kutokana na hali ya mgonjwa

 

9. Mpatie mgonjwa antibiotics ili kuweza kuepuka Maambukizi ambayo yanaweza kutokea ua kusaidia kutibu maambukizi na dawa hizi zinapaswa kutolewa kwa ruhusa ya wataalamu wa afya.

 

10.Kama sehemu yenye matatizo kuna nywele jaribu kuzing'oa ili kuondoa njia ya kupata Maambukizi.

 

11.Mpatie Mgonjwa elimu kama patatokea shida yoyote kama vile maji maji na kuendelea kuvuja damu atoe taarifa.

 

12.Mpatie Mgonjwa Mda wa kuja kutolewa nyuzi kama sehemu iliyokuwa inavuja imeshomwa



Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2022/02/23/Wednesday - 07:56:38 am     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 731


Download our Apps
👉1 Kitau cha Fiqh     👉2 Madrasa kiganjani     👉3 Kitabu cha Afya     👉4 kitabu cha Simulizi    

Post zifazofanana:-