Njia za kupunguza uzito na kitambi

Posti hii inahusu zaidi njia mbalimbali ambazo zinaweza kutumika ili kuweza kupunguza tatizo la kuwepo kwa uzito mkubwa pamoja na kitambi

Njia za kupunguza uzito mkubwa pamoja na kitambi.

1. Tunapaswa kufahamu kwamba mara nyingi tatizo la kuwepo kwa uzito mkubwa na kitambi ni mtindo wa maisha ambapo kwa walio wengi ujiachiaa kabisa katika maisha na vyakula, kwa mfano unaweza kuona mtu anatoka nyumbani kwenda kazini kwa kutumia gari na akifika kazini ni kukaa tu na jioni akitoka kazini ni kupiga bia na nyama yoyote ile na pengine anaongezea chips akitoka hapo anafika nyumbani ni kuangalia movies na kusubiria chakula, watu wanaishi hivyo hata bila ya mazoezi hatimaye kuota kitambi na unene kupita kiasi.

 

2. Kwa hiyo watu wanapaswa kubadilika na kufuata yafuatayo ili kuweza kuepuka na tatizo la kuwepo kwa vitambi kwa kubadilisha mtindo wa maisha kwa kupiga mazoezi mara kwa mara walau mara tatu kwa  wiki pamoja na kutumia maji ya uvuguvugu ili kupunguza vitambi na unene uliopitiliza.

 

3. Epuka matumizi ya vyakula vya wanga.

Kwa kawaida kitu kikubwa ambacho kipo kwenye vyakula vya wanga ni starch na ndiyo inayosababisha kuwepo kwa unene uliopitiliza.

 

4. Epuka matumizi ya vyakula vyenye sukari nyingi.

Kwa kawaida tunajua kazi ya sukari ikiwa nyingi mwilini usababisha kuwepo kwa mwongezeko wa mwili pamoja na uzito kwa hiyo ni vizuri kutumia sukari kidogo kwenye vinywaji.

 

5. Kufunga ili kuweza kuchoma calories ambazo zimo mwilini ambazo utokana na ulaji wa vyakula vyenye wanga na sukari.

 

6. Tumia vyakula vyenye wingi wa protini na gari kwa kiasi kidogo na pia tumia uchache wa unga na sukari.

 

7. Katika kupunguza uzito ni vizuri kabisa kufahamu kwamba matumizi ya vyakula vya wanga mara kwa mara hata kama unafanya mazoezi sio rahisi kupunguza tatizo kwa hiyo punguza matumizi ya vyakula vyenye wanga.

 

Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 1970-01-01 03:33:44 Topic: Huduma Main: Afya File: Download PDF Views 1974

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
👉1 kitabu cha Simulizi    👉2 Simulizi za Hadithi Audio    👉3 Kitabu cha Afya    👉4 Dua za Mitume na Manabii    👉5 Tafasiri ya Riyadh Swalihina    👉6 web hosting   

Post zinazofanana:

Kazi za vitamin B na makundi yake

Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu kazi za vitamin B na makundi take

Soma Zaidi...
HUDUMA YA KWANZA KWA ALIYEANGUKA KIFAFA

Kifafa kinaweza kumpata mtu muda wowte.

Soma Zaidi...
Njia za kujilinda dhidi ya mapunye

Somo Hili linakwenda kukueleza kuhusu njia za kujilinda dhidi ya mapunye

Soma Zaidi...
Utaratibu wa lishe kwa vijana

Somo Hili linakwenda kukueleza kuhusu utaratibu wa lishe kwa vijana

Soma Zaidi...
Vyakula vya kuongeza nguvu za kiume

Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu baadhi ya vyakula vinavyoongeza nguvu za kiume

Soma Zaidi...
Mbinu za kupunguza magonjwa yanayohusiana na figo

Posti hii inahusu zaidi ugonjwa wa figo. Ni ugonjwa unaotokana pale figo linaposhindwa kufanya kazi, tuone mbinu za kufanya Ili kuepuka na tatizo hilo.

Soma Zaidi...
Huduma ya Kwanza kwa mtu aliyekunywa sumu

Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu huduma ya Kwanza kwa mtu aliyekunywa sumu

Soma Zaidi...
Yanayoathiri afya

Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu mambo yanayoathiri afya

Soma Zaidi...
Utaratibu wa maisha kwa aliye athirika

Somo hili linakwenda kukuletea utaratibu wa maisha kwa aliye athirika

Soma Zaidi...
Mzunguko wa mwezi kwa mwanamke

Posti hii inahusu zaidi mzunguko wa mwezi kwa mwanamke, ni mzunguko ambao huchukua siku ishilini na nane kwa kawaida Ila lla ubadilika kulingana na mtu, Ila ngoja tuangalie siku ishilini na nane tu.

Soma Zaidi...