HUDUMA YA KWANZ AKWA ALIYEPALIWA AMA KUSAKAMWA NA KUTU KOONI
Mtu aliyepaliwa ama kukwamwa na kitu kooni huwa anashindwa kuzungumza ama kupumua. Hali hii ikiendelea kwa muda inaweza kumsababishi amadhara makubwa hata kifo. Ubongo unaweza kufa ndani ya dakika chache sana kama ukikosa hewa ya oksijeni. Kama ukimkuta mtu amepaliwa ama kukamwa na kitu kooni na anashindwa kupumua unatakiwa umpe huduma ya kwanza:
Mtu anaweza kukwamwa ama kupaliwa na chakula, ama kitu kigumu kama kumeza pesa, jiwe barafu na kadhalika. Pia anaweza kupaliwa na maji, asali ama kimiminika chochote na kuzuia njia ya hewa. Hivyo kuathiri mfumo wa upumuaji.
Kama kupaliwa ni kwa kawaida amnapo mtu atakuwa na uwezo wa kukohoa, kulia, kuzungumza na kuhema, tambua kuwa anaweza kurudi katika hali ya kawaida hata bila ya kupata huduma ya kwanza. Ili kumsaidia mtu huyu kurudi haraka katika hali ya kawaida
1.Mwambie aendelee kuhohoa zaidi hii itasaidia kuondoa kilichokwama
2.Mwambe ajaribu kutema kicho kilichomkaba ama kilicho mkwama ama kusababisha kupaliwa
3.Katu usuthubutu kuingiza vidole vyeko kwenye koo lake eti kujaribu kukitoa kilicho mkaba
Kupaliwa kwa namna nyingine iliyo mbaya ni pale mtu anaposhindwa kusema, kukohoa, kulia ama kuhema. Bila ya huduma ya kwanza mtu huyu anaweza kuzimia na hatimaye kupoteza maisha. Huduma ya kwanza kwa mtu huyu ni:-
1.Muinamiche kifua chake kwa mbele, hii itasaidia kitu kilichomkaba kisiende ndani sana
2.Simama nyuma yake pembeni kidogo, weka mkono wako mmoja kwenye kifua chake na mgono wako mwingine anza kumpiga ngumi kwenye mgongo wake kati ya bega na bega, usawa na kifua kwa nyuma.
3.Angalia kama kilichomkaba kimeondoka
4.Kama hakijaondoka mpige tena kwa nguvu mapigo matano kama ni mtoto mminye kwa nguvu kwenye tumbo lake fanya hivi mara tano. Usifanye hivi kwa mtoto mdogo.
5.Kama hali inaendelea umpeleke kituo cha afya cha karibu.
Umeionaje Makala hii.. ?
Posti hii inahusu zaidi Aina ya mkojo usiokuwaa wa kawaida uwa na vitu vifuatavyo, ukiona dalili kama hizo wahi mapema hospitalini Ili upatiwe huduma.
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za vyakula vya madini mwilini
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi tatizo la kupungukiwa damu mwilini, ni ugonjwa unaotokana sana hasa kwa watoto wadogo chini ya miaka mitano ingawa na kwa watu wazima.
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi jinsi moyo unavyosukuma damu, moyo ni ogani ambayo usukuma damu kwenye sehemu mbalimbali za mwili.
Soma Zaidi...Post inaenda kuzungumzia kuhusiana na upungufu wa damu mwilini ambapo tutaona SABABU na dalili zake lakin upungufu wa damu mwilini hujulikana Kama ANEMIA.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi madhara ambayo yanaweza kutokea kwa mtu mwenye uzito mkubwa,kwa kawaida ili mtu aweze kuwa na uzito wa kawaida ni vizuri na kiafya kupima urefu ukilinganisha na uzito wa mtu.
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi umuhimu wa makundi manne ya damu na jinsi yanavyotumika, Ni magroup manne ya damu ambayo husaidia kuongeza damu kwa mtu ambaye amepungukiwa damu
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu huduma ya Kwanza kwa mtu aliyepatwa na kwikwi
Soma Zaidi...Posti hii inaelezea kuhusiana na upungufu wa maji mwilini
Soma Zaidi...