Post hii inahusu zaidi huduma kwa mama ambaye mimba inataka kutoka, mimba za aina hiyo kwa kitaalamu huitwa inevitable pregnant ni lazima itoke tu hata kama kuna juhudi mbalimbali za wataalamu mimba hii utoka kabisa.
Huduma kwa mama mwenye mimba inayotaka kutoka.
1. Kwanza kabisa napenda kuwakumbushia kwamba aina ya mimba hii huwa na dalili zote za mimba kutoka ambazo ni pamoja na kutokwa kwa damu nyingi ambayo uandamana na maumivu makali ya tumbo hasa tumbo la chini.kama mama ataangaliwa na wataalamu wa afya mimba uonekane kwenye mlango wa kizazi na mara nyingi kichanga kinakuwa kimeshakufa tayari kwa hiyo mama ufanyiwa uangalizi wa karibu ili kuhakikisha kwamba mimba inatoka kwa utaratibu bila kuasili maisha ya mama.
2. Kama mimba iko chini ya miezi mitatu au wiki kumi na mbili kusafishwa kunapaswa kufanyika kwa kutumia njia ya kitaalam ambayo inaitwa manual vacuum evacuation, kwa hiyo ni vizuri kabisa akina Mama kuelewa siku zao za mimba ili kuweza kupata huduma inayofaa endapo matatizo kama haya yakitokea.
3 . Kama mimba ipo zaidi ya miezi minne au zaidi ya wiki kumi na mbili mama anapaswa kupewa dawa za kuanzisha uchungu ili kuweza kujifungua kawaida dawa hizo huitwa oxtocini na siku zote upitishwa kwenye mirija ya damu, mama anapaswa kupewa taarifa zote hatua kwa hatua na pia aambiwe lengo la kupewa dawa za kuanzisha uchungu.
4. Pia mama anapaswa kutiwa moyo na kumhakikishia usalama na kumwambia kwamba ni hali ambayo utokea akina Mama wengi na pia urudia hali ya kawaida.
5. Pia jamii na watu wa karibu wa mama wanapaswa kumtia moyo mama na kuachana na mila na desturi za kwamba mimba kutoka ni aibu kwa ukoo kwa hiyo wasimtenge mama bali na wenyewe wapewe elimu kuhusu namna ya kumsaidia na kumtunza mama pale atakaporudi kwa hali ya kawaida.
6. Pia mama anapaswa kuambiwa wazi wazi siku za kubeba mimba nyingine na afahamu kwamba baada ya mimba kutoka ndani ya siku ishirini na moja anaweza kubeba mimba nyingine kwa hiyo anapaswa kutumia uzazi wa mpango ili kuepuka kubeba mimba nyingine kabla ya viungo havijawa na nguvu kuweza kutunza mimba, kwa hiyo mama akitoa mimba anapaswa kubeba mimba nyingine baada ya miezi sita.
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetuUmeionaje Makala hii.. ?
Vyakula hivi hapasi kuvila mwanamke mwenye ujauzito kwa kiasi kikubwa, hasa yule mwenye mimba chaga
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi njia mbalimbali za kuongeza uwezo wa kuzaa au kuzalisha kwa sababu kuna familia nyingi zinakosa watoto sio kwa sababu ni tasa ila kuna njia mbalimbali za kuongeza uwezo wa kuzaa kama ifuatavyo.
Soma Zaidi...Yai lililopikwa ni chanzo kizuri cha protini, vitamini, na madini muhimu kwa mama mjamzito. Husaidia katika ukuaji wa mtoto tumboni, afya ya mama, na kuimarisha kinga ya mwili.
Soma Zaidi...PEP Ni dawa ambazo utumiwa na watu wanaojamiiana na watu wenye virus vya ukimwi ila wenyewe hawawezi kupata kwa sababu ya kutumia dawa hizo.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi dalili ambazo zinaweza kutokea iwapo Kuna upungufu wa homoni ya progesterone.
Soma Zaidi...Je ungependa kuijuwa Njia ya kuzuia mimba wakati wa tendo la ndoa?. Posti hii itakwenda kukufundisha ujanja huu.
Soma Zaidi...Kama na wewe unasumbuliwa na hali ya kupitiliza siku zako post hii itakusaidia.
Soma Zaidi...Somo Hili linakwenda kukueleza kuhusu sababu za maumivu ya tumbo wakati wa tendo la ndoa
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi mabadiliko kwenye uke wa Mama pale anapobeba tu mimba, Mama anapobeba mimba Kuna mabadiliko Katika uke wa Mama kama ifuayavyo.
Soma Zaidi...