Kondo la nyuma kuwa mbele ya mlango wa kizazi
Posti hii inahusu zaidi sababu za kondo la nyuma kuwa mbele ya mlango wa kizazi, kwa kawaida kondo la nyuma huwa nyuma ya mlango wa kizazi ila Kuna wakati kondo la nyuma ujishikisha mbele ya mlango wa kizazi.
Sababu za kondo la nyuma kuwa mbele ya mlango wa kizazi.
1. Kwanza kabisa tunapaswa kujua kuwa mtoto akija kuzaliwa utanguliza kichwa na kutoka kwenye tumbo la Mama ila Kuna wakati mwingine kondo la nyuma ndilo utangulia na kufuatia mtoto hii ni hatari kwa mtoto kwa Sababu hii kesi kama haijakutana na myaalamu wa kuzalisha mtoto anaweza kufia tumboni kwa hiyo ni vizuri kumtambua dalili na kumsaidia mama akaweza kujifungua salama.
2. Sababu ya kutanguliza kondo la nyuma badala ya mtoto pengine nikwa sababu ya kuwepo kwa maambukizi in kwenye mfuko wa kizazi kwa hiyo kondo la nyuma uweza kujishikisha sehemu ambayo Haina maambukizi na kusababisha kondo la nyuma kutangulia mapema wakati mtoto anapozaliwa.
3. Kuwepo kwa makovu kwenye mfuko wa uzazi.
Pengine kwenye mfuko wa kizazi panakuwepo na jeraha na jeraha hilo kwa wakati mwingine uwa kwenye sehemu ambayo kondo la nyuma linapasaw kujishikiza kwa hiyo ujishikiza sehemu yoyote ambayo ni tofauti na sehemu ya kawaida.
4. Kuwepo kwa upasuaji ambao umefanyika kabla ya mimba haijatungwa na yenyewe usababisha kuwepo kwa kitendo cha kondo la nyuma kujishikiza chini ya mlango wa kizazi na kusababisha madhara makubwa wakati wa kujifungua.
5. Mwonekano wa tumbo la uzazi kutokuwa la kawa, Kuna wakati mwingine tunaweza kumwona mtu yupo anatembea na ameumbika kawaida kwa nje ila ukija kuangalia kwa ndani mfuko wa uzazi ni tofauti na wengine kwa kitaalamu huitwa abnormally of uterus, kwa hiyo kama hauko kawaida usababisha kondo la nyuma kujishikiza sehemu yoyote isiyokuwa ya kawaida na kusababisha kondo la nyuma kutangulia mtoto.
6. Kwa kawaida kuja kumtambua kuwa Mama ana tatizo hili ni kufuatana na ujuzi wa muuguzi kwa sababu Mama anakuwa na uchungu kawaida na sifa zote za kujifungua ila shida kilichotangulia ndicho hakieleweki, kwa hiyo hali hii ikigundulika ni vizuri kumpeleka mama hospital Ili kuweza kumsaidia zaidi maana kama hakuna huduma mtoto anaweza kufia tumboni
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 Kitabu cha Afya 👉2 ai web app 👉3 Simulizi za Hadithi Audio 👉4 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w) 👉5 kitabu cha Simulizi 👉6 Tafasiri ya Riyadh Swalihina
Post zinazofanana:
Utaratibu wa kushiriki tendo la ndoa kwa wajawazito
Jifunze muda ambao mjamzito hatatkiwa kishiriki tendo la ndoa. je kuna madhara kwa mjamzito kushiriki tendo la ndoa.
Soma Zaidi...Hiv n kweli majivu hutoa mimb ya siku moja hadi wiki moja
Inashangaza sana, wakati wengine wanahangaika kutafutavijauzito kwa gharama yoyote ile, kuna wengine wanataka kutoa ujauzito kwa gharama yeyote ile. Unadhani njia za kienyeji sa kutoa mimba ni salama?
Soma Zaidi...Mtoto anaanz kucheza kwa mda gan
Kuna watoto wengine huanza kucheza mapema kuliko watoto wengine. Tunapozungumzia kucheza kwa mtoto aliye tumboni yaani mimba hapa inatubidi tuangalie kwa undani zaidi, je ni muda gani mtoto ataanza kucheza?
Soma Zaidi...Je chuchu zikiwa nyeusi Nini kinasababisha,, kando ya kuwa mjamzito? Na Kama sio mjamzito sababu ya chuchu kua nyeusi ni nini
Chuchu kubadilika range ni mojavkatika mabadiliko ambayo huwapa shoka wengi katika wasichana. Lucinda nikwambie tu kuwa katika hali ya kawaida hilo sio tatizo kiafya.
Soma Zaidi...Je, wajua sababu zinazopelekea maumivu ya Matiti kwa wanawake?
Maumivu ya matiti ni malalamiko ya kawaida miongoni mwa wanawake yanaweza kujumuisha uchungu wa matiti, maumivu makali ya kuungua au kubana kwenye tishu zako za matiti. Maumivu yanaweza kuwa ya mara kwa mara au yanaweza kutokea mara kwa mara tu. Maumiv
Soma Zaidi...