Utangulizi
Tabii Tabiina ni wafuasi wa Tabiin au wafuasi wa wajukuu wa maswahaba.
Wanazuoni katika kipindi cha Tabiina, wakiwemo maimamu wanne wa Fiq-h, walijitahidi sana kukusanya Hadith za Mtume (s.a.w) lakini kazi zao hazikuweza kukidhi mahitaji yote ya kuendea kila kipengele cha maisha ya kibinafsi na kijamii. Kwa mfano kitabu cha Imamu Malik, Al-muwatta,kilichokuwa mashuhuri sana katika enzi hizo kiligusia baadhi ya mambo tu yakiwemo yale ya Ibada maalumu za swala,swaumu,Zakat na Hija. Pamoja na mapungufu haya pia iligundulika kuwa katika kipindi cha Tabiina zilizushwa Hadith za uwongo maelfu kwa maelfu.
Katika kupunguza mapungufu haya wanazuoni katika kipindi cha Tabii Tabiin walijishughulisha sana na kukusanya na kuandika Hadith kuhusu nyanja zote za maisha ya muiislamu. Pia ili kuhakikisha usahihi wa Hadith walizozikusanya na kuziandika walichukua tahadhari kubwa sana katika kuzichuja. Katika kipindi hiki walitokea maimamu mashuhuri sita waliojitahidi na kutumia sehemu kubwa ya maisha yao katika kukusanya,kuchuja na kuandika Hadith.
Maimamu hawa ni: Bukhari, Muslim, Abu Daud, Nasai, Ibn Majaha na Tirmidh. Walisafiri masafa marefu kwa ajili ya kazi hii ya ukusanyaji Hadith na ilibidi wajifunze tabia ya wapokezi kadhaa wa Hadith kabla hawajaiandika. Sio kila Hadith waliyoambiwa waliiandika bali kulikuwa na utaratibu wa kuchambua Hadith iliyo sahihi na isiyo sahihi kwa kuzingatia tabia za wasimulizi na vigezo vya matini ya Hadith. Kutokana na jitihada zao za uchujaji wa Hadith, vitabu vyao vilijulikana kwa jina la βSitta Sahihiβ. Kila Imamu wa Hadith alivyozidi kuwa muangalifu katika uchujaji wa Hadith zake alizozikusanya ndivyo kitabu chake kilivyopewa daraja ya juu ya usahihi. Vitabu sita mashuhuri vya Hadith sahihi vilivyoandikwa na maimamu hao ni:
Umeionaje Makala hii.. ?
Pamoja na utukufu na umadhubuti wa ufalme wake Nabii Sulaiman muda wake wa kuishi ulipokwisha aliondoka kama walivyoondoka Mitume,wafalme na wanaadamu wengine.
Soma Zaidi...KULELEWA NA BABA YAKE MDOGOBaada ya kufariki kwa mzee huyu, kiongozi mkubwa wa maquraysh na makkah, kiongozi ambaye jeshi la Abrah liliangamizwa ndani ya utawala wake.
Soma Zaidi...Historia na shida ya Mtume Muhammad S.A.W, sehemu ya 12. Hapa utajifunza kuhusu kutokea kwa vita vya al fijar.
Soma Zaidi...KULELEWA NA BABU YAKE:Mzee βAbdul Al-Muttalib alimchukuwa mjukuu wake na wakarejea Makkah na aliendelea kuishinae na kumlea kwa mapenzi makubwa sana.
Soma Zaidi...