Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu njia ambazo VVU huambukizwa
NJIA AMBAZO VVU HUAMBUKIZWA;
Kuna nadharia nyingi zinaelezea ni namna gani ambazo VVU huambukizwa. Katika hizo kuna mbazo ni Imani potofu kabisa na hazifai kukubaliwa. Hapa nitakuletea njia ambazo zinaambukiza VVU. Njia hizo ni:-
1.Kwa kufanya mapenzi (ngono). Unaweza kuambukizwa ikiwa unafanya ngono ya uke, ya mkundu au ya mdomo na mwenzi aliyeambukizwa VVU ambaye damu yake au shahawa zake au majimaji ya ukeni huingia mwilini mwako kwa kupitia michubuko midogo, ama vidonda ama mikato ama sehemu iliyowazi inayoruhusi kufikiwa damu kwa urahisi. Na hii ndiyo njiainayoongoza katika kuambukiza VVU
2. Kwa kuongezewa damu kutoka kwa aliye athirka. Katika namn nyingine, virusi vinaweza kuambukizwa kupitia kuongezewa damu. Kwa sasa si sana njia hii maana damu anayopatiwa mgonjwa itapitia uchunguzi wa kina kabla ya kuongezewa ijapokuwa madhaifu ya kibinadamu yanaweza kufanyika.
3. Kwa kushirikiana matumizi ya sindano na vitu vyenye ncha kali kama visu na viwembe. VVU vinaweza kuambukizwa kupitia sindano, inaweza kutokea wakatiwa matibabu yatakayofayika chini ya utaratibu. Inaweza pia kuwa watumiaji a madawa ya kulevya hushirikiana sana matumizi ya sindano. Endapo mtumiaji wa kwana ana VVU na akajidunga ama kujikata, kisha akachukuwa mtumiaji mwinine na kujidunga ama kujikata muda mfupi toka mtumiaji wenye VVU kutumia.
4. Wakati wa ujauzito au kujifungua au kupitia kunyonyesha. Mama walioambukizwa VVU wanaweza kuambukiza watoto wao endapo hwatakuwa makini. Mama mjamzito mwenye VVU anatakiwa atumie dozi haraka iwezekanavyo ili kuepushamaambukizi kwa mtoto. Hata hivypo inampasa azalie hospitali ili uangalifu zaidi ufanyike wakati a kujifunguwa.
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetuUmeionaje Makala hii.. ?
hapa utajifunza maradhi mbalimbali yanatopelekea kuwepo kwa maumivu ya tumbo
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi dalili za mtoto Mwenye UTI,ni dalili ambazo uwapata watoto wadogo chini ya umri wa miaka mitano.
Soma Zaidi...Posti hii inazungumzia sababu zinazopelekea kuumwa na kifua.
Soma Zaidi...mm nahis miguu pamoja na mikono kuishiwa nguvu ni mgongo kuuma ni dalili za ugonjwa gan ?
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi hatua mbalimbali za Ugonjwa wa Ukimwi, kawaida Ugonjwa huu huwa na hatua kuu nne ila kila hatua huwa na sifa zake kwa hiyo tunapaswa kujua hatua za Ugonjwa huu na kujaribu kuzuia maambukizi yasisambae kabisa.
Soma Zaidi...Mvurugiko katika mfumo wa chakula mwilinivunaweza kusababisha maumivu ya tumbo, kuharisha, kutapika na kuchoka pia. Lakini zipo sababu nyingine kama kuwana ujauzito. Nini ufanye endapo unasumbuliwana hali hii
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi tatizo la fizi kuachana, ni tatizo ambalo uwakumba watu wengi kwa wakati mwingine unakuta fizi zimeachana kutoka sehemu moja kwa nyingine kwa hiyo tunaweza kuona sababu kama ifuatavyo.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi dalili ambazo mtu anaweza kupata ikiwa Kuna maambukizi kwenye magoti, kwa sababu mbalimbali ambazo usababisha maumivu au maambukizi kwenye magoti Kuna dalili za mwanzo ambazo zinajitokeza kama tutakavyoona hapo chini
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi tatizo la kushindwa kushuka kwa makende kutoka kwenye tumbo kwenda kwenye skolatumu(scrotum).
Soma Zaidi...