Hadithi Ya 35: Msioneane Choyo, Msizidishiane Bei, Msichukiane
Hadithi Ya 35: Msioneane Choyo, Msizidishiane Bei, Msichukiane
الحديث الخامس والثلاثون
"لا تحاسدوا ولا تناجشوا ولا تباغضوا"
عن أبي هُريرةَ رضي اللهُ عنه قال: قال رسوُل الله صلى الله عليه وسلم : ((لا تَحَاسَدُوا، ولا تَنَاجَشُوا، ولا تَباغَضُوا، ولا تَدَابَرُوا، ولا يَبعْ بَعْضُكُمْ على بَيْعِ بَعْضٍ، وكُونُوا عِبادَ اللهِ إخْوَاناً، المُسْلمُ أَخُو المُسْلمِ: لا يَظْلِمُهُ، ولا يَكْذِبُهُ، ولا يَحْقِرُهُ، التَّقْوَى هاهُنا - ويُشِيرُ إلى صَدْرِه ثَلاثَ مَرَّاتٍ , بِحَسْبِ امْرِىءٍ مِنَ الشَّرِّ أن يَحْقِرَ أخاهُ المُسْلِمَ، كُلُّ المُسْلِمِ على الْمسْلِم حَرَامٌ: دَمُهُ ومالُهُ وعِرْضُهُ))
رَوَاهُ مُسْلِمٌ
HADITHI YA 35 MSIONEANE CHOYO, MSIZIDISHIANE BEI, MSICHUKIANE
Kutoka kwa Abu Hurayra رضي الله عنه ambae amesema: Mtume صلى الله عليه وسلم kasema:
Msioneane choyo, wala msizidishiane bei (za vitu), wala msichukiane, wala msipigane mapande (msitengane), wala msishindane kwa kupunguza bei. Lakini kuweni ndugu, enyi waja wa Mwenyeezi Mungu, Muislamu ni ndugu wa Muislamu mwenzake, hamdhulumu wala hamvunji, hamwambii uongo wala hamdharau. Ucha Mungu uko hapa (huku akiashiria kifuani kwake kwa vidole vyake) mara tatu. Ni uovu wa kutosha kwa mtu kumdharau ndugu yake Muislamu. Muislamu ameharamishiwa kwa Muislamu mwenzake: damu yake, mali yake na heshima yake (Yaani haramu kuchukua mali ya mwenzako, kumuua na kumdhalilisha).
Imesimuliwa na Muslim
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 Simulizi za Hadithi Audio 👉2 Kitau cha Fiqh 👉3 kitabu cha Simulizi 👉4 Madrasa kiganjani 👉5 web hosting 👉6 Tafasiri ya Riyadh Swalihina
Post zinazofanana:
TANZU ZA HADITHI
Tanzu za Hadith(1) Tanzu ya UsahihiKulingana na kiwango cha usahihi wa Hadith, Hadith zimegawanywa katika makundi makuu manne:(a) Sahihi (b) Hasan/Nzuri.
Soma Zaidi...(ii)Hum cha Allah (s.w) kwa kutekeleza amri zake
Anapotajwa Mwenyezi Mungu au wanapokumbushwa juu ya maamrisho na makatazo ya Mwenyezi Mungu, nyoyo zao hunyenyekea na kufuata kama walivyokumbushwa.
Soma Zaidi...