Hadithi Ya 25: Wenye Mali Wameondoka Na Fungu (jaza) Kubwa

Hadithi Ya 25: Wenye Mali Wameondoka Na Fungu (jaza) Kubwa

Hadithi Ya 25: Wenye Mali Wameondoka Na Fungu (jaza) Kubwa

Hadithi Ya 25: Wenye Mali Wameondoka Na Fungu (jaza) Kubwa

 

الحديث الخامس والعشرون

"ذهب أهل الدثور بالأجور "

 عن أبي ذَرٍّ رضي اللهُ عنه:  أَنَّ ناساً من أَصْحابِ رسول الله صلى الله عليه وسلم، قالوا لِلنَّبيِّ صلى الله عليه وسلم: يا رسولَ اللهِ، ذَهَب أَهْلُ الدُّثورِ بالأُجورِ، يُصَلُّونَ كما نُصَلِّي، ويَصُومُونَ كما نَصُومُ، وَيَتَصَدَّقُونَ بِفُضُولِ أَمْوَالِهِمْ. قَالَ: ((أوَ لَيْسَ قَدْ جَعَلَ اللهُ لَكُمْ مَا تَصَدَّقُونَ ؟ إنَّ  بكلِّ تَسْبيحَةٍ صَدَقَةً، وكُلِّ تَكْبِيرَةٍ صَدَقَةً، وكُلِّ تَحْمِيدَةٍ صَدَقَةً، وَكُلِّ تَهْلِيلَةٍ صَدَقَةً، وَأَمْرٍ بِالْمَعرُوفِ صَدَقَةً، وَنَهْيٍ عَنْ مُنْكَرٍ صَدَقَةً، وفي بُضْعِ أحَدِكُمْ صَدَقَةً)). قَالُوا: يَا رَسُولَ اللهِ، أَيَأْتي أحَدُنَا شَهْوَتَهُ وَيَكُونُ لَهُ فِيهَا أجرٌ ؟ قَالَ:

((أَرَأَيْتُمْ لَوْ وَضَعَها في حَرَامٍ، أَكَانَ عَليْهِ وزْرٌ ؟ فَكَذلِكَ إذَا وَضَعَها في الْحَلاَلِ كانَ لَهُ أَجْرٌ ))

رَوَاهُ مُسْلِمٌ   


 

HADITHI YA  25

WENYE MALI WAMEONDOKA NA FUNGU (JAZA) KUBWA

 

Kutoka kwa Abu Dharr رضي الله عنه  ambaye amesema:

Baadhi ya Maswahaba wa Mtume صلى الله عليه وسلم  walimuambia  Mtume صلى الله عليه وسلم  : Ewe Mjumbe wa Mwenyeezi Mungu, wenye mali wameondoka na fungu (jaza) kubwa, wanaswali kama sisi, wanafunga kama sisi, na wanatoa sadaka ya ziyada ya mali zao. Mtume صلى الله عليه وسلم  akasema:  Mwenyeezi Mungu hajakufanyieni vitu kwa ajili yenu kutoa sadaka?  (Basi jueni) Hakika kila Tasbihi (Subhana Allah) ni sadaka, kila Takbiri (Allahu Akbar) ni sadaka, kila Tahmidi (AlhamduliLlah) ni sadaka, na kila Tahlili (Laa ilaaha illa Allaah) ni sadaka, na kulingania jambo  jema ni sadaka, na kukataza mabaya ni sadaka na katika kujamii (wake zenu) kila mmoja katika nyinyi ni sadaka. Wakasema  (Maswahaba): Ewe Mtumeصلى الله عليه وسل mtu anapojitosheleza shahawa yake atapata malipo kwa ajili yake?  Akasema    صلى الله عليه وسلم  : Mnadhani ingekuwa anajitosheleza kwa njia ya haramu angelipata dhambi?  Na hivyo ikiwa kafanya kwa njia ya halali basi atapata thawabu.

 

Imesimuliwa na Muslim



                   

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

       
Author: Rajabu Rajabu
Tarehe: 2024-05-10 14:53:23 Topic: Sunnah Main: Post File: Download PDF Views: 2751

Share On:

Share follows: 0 | Unique share links followed: 0
Sponsored links
👉1 Madrasa kiganjani     👉2 Tafasiri ya Riyadh Swalihina     👉3 Kitau cha Fiqh     👉4 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)     👉5 Bongolite - Game zone - Play free game     👉6 Kitabu cha Afya    

Post zinazofanana:

Mambo yaliyo sunnah siku za Idi ('iyd) siku ya sikukuu

Makala hii inaelezea mambo mbalimbali yaliyothibiti katika Sunnah kuhusu namna ya kuadhimisha siku ya ‘Iyd kwa mujibu wa mafundisho ya Kiislamu. Miongoni mwa mambo hayo ni kuvaa mavazi mazuri, kula kabla ya Swalaah ya ‘Iydul-Fitwr, kuleta Takbira, kuswali kwenye Muswallaa, pamoja na adabu nyingine zinazopaswa kufuatwa na Waislamu katika siku ya Sikukuu.

Soma Zaidi...
Dua sehemu ya 04

Soma dua mbalimbali za kila siku ambazo unatakiwa uzijuwe. Dua 120 ambazo muislamu anatakiwa kuzijua

Soma Zaidi...
Hukumu ya kukusanyika kwenye dua na umuhimu wa dua ya watu wengi

Post hii inakwenda kukufundisha kuhusu umuhimu wa kukusanyika katika kuomba dua.

Soma Zaidi...