Ria ni kinyume cha Ikhlas.
Ria ni kinyume cha Ikhlas. Kufanya ria ni kufanya jambo jema ili watu wakuone, wakusifu, wakupe shukurani, n.k. Mtu anayefanya ria hafanyi wema kwa kutarajia malipo kutoka kwa Allah (s.w) bali hufanya kwa kutarajia malipo ya hapa duniani tu, iwe ni mali au sifa au shukurani.
Mwenye kufanya ria hata akijiita Muislamu hana malipo yoyote mbele ya Alllah(s.w) katika siku ya Hukumu isipokuwa adhabu kali Motoni kama tunavyojifunza katika aya zifuatazo:-
“Wanaotaka maisha ya dunia na mapambo yake, tutawapa huku duniani (ujira wa) vitendo vyao kamili, humu wao hawatapunjwa. Hao ndio ambao hawatakuwa na kitu katika akhera ila moto na wataruka patupu waliyoyafanya katika dunia hii na yatakuwa bure waliyokuwa wakiyatenda.” (11:15-16)
Katika aya nyingine Allah (s.w) anatukamia:
“Basi adhabu (kali) itawathubutikia wanaoswali; ambao wanapuuza swala zao. Ambao hufanya riyaa ”. (107:4)
Katika Hadith tunafahamishwa kuwa Mtume (s.a.w) amesema:
“Katika siku ya hukumu, vitendo vyote vilivyofanywa hapa duniani vitahudhurishwa mbele ya Allah (s.w). Vitendo vilivyofanywa kwa ajili ya Allah (s.w) vitatengw a. Na vitendo vingine vilivyofanyw a kw a nia nyingine mbali mbali vitatupw a motoni”. (Baihaqi).
Umeionaje Makala hii.. ?
Hii ni historia ya uandishi wa hadithi wakati wa tabii tabiina. Yaani wafuasi wa wale wafuasi wa Masahaba
Soma Zaidi...Wajibu wa Wazazi kwa Watoto Wazazi wanawajibu kwa watoto wao.
Soma Zaidi...DUA ZA WAKATI WA SHIDA Dua ya wakati wa taabu βLAA ILAAHA ILLA-LLAHUL-βADHIMUL-HALIIMU.
Soma Zaidi...Kwenye Quran kuna duaambazo Allah ametufundisha tuziombe kwa ajili ya wazazi, familia na kwa ajili yetu wenyewe.
Soma Zaidi...Zijue fadhila za kuomba dua, tambua umuhimu na mahimizo juu ya kuomba dua?
Soma Zaidi...