Post hii inakwenda kukupa tahadhari juu ya mambo ya halali na mambo ya haramu.
عَنْ أبي عَبْد٠الله٠النّÙعْمَان٠بْن٠بَشÙير٠رَضÙÙŠÙŽ الله٠عَنْهÙما قَالَ : سمعت٠رَسÙولَ الله٠صلى الله عليه وسلم ÙŠÙŽÙ‚ÙولÙ: ((إن الْØَلالَ بَيّÙÙ†ÙŒ وَإنَّ الْØَرَامَ بَيّÙÙ†ÙŒ وَبَيْنَهÙما أمورٌ Ù…ÙشْتَبÙهَاتٌ لا يَعْلَمÙÙ‡Ùنَّ كَثيÙرٌ Ù…ÙÙ†ÙŽ الناسÙØŒ Ùَمَن٠اتَّقَى الشّÙبÙهَات٠Ùَقَد اسْتَبْرَأَ Ù„ÙدÙينÙه٠وَعÙرْضÙÙ‡ÙØŒ وَمَنْ وَقَعَ ÙÙŠ الشَّبÙهات٠وَقَعَ ÙÙŠ الْØَرَامÙØŒ كالرَّاعÙÙŠ يَرْعَى Øَوْلَ الْØÙÙ…ÙŽÙ‰ ÙŠÙوشÙك٠أَنْ يَرْتَعَ ÙÙيهÙØŒ أَلا وَإنَّ Ù„ÙÙƒÙلّ٠مَلÙÙƒÙ ØÙمىً أَلا وَإنَّ ØÙÙ…ÙŽÙ‰ الله Ù…ÙŽØَارÙÙ…Ùه، أَلا وَإنَّ ÙÙŠ الجَسَد٠مÙضْغَةً إذَا صَلَØَتْ صَلَØÙŽ الْجَسَد٠كÙلّÙه٠وإذَا Ùَسَدَتْ Ùَسَدَ الْجَسَد٠كÙلّÙÙ‡ÙØŒ أَلا ÙˆÙŽÙ‡ÙÙŠÙŽ الْقَلْبÙ)) رَوَاه٠الْبÙخَارÙيّ٠وَمÙسْلÙÙ…ÙŒ
Imepokelewa kutoka kwa Abuu ‘Abdillaah An-Nu’umaan bin Bashiyr (Radhwiya Allaahu 'anhu) ambaye alisema: Nimemsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: “Hakika halaal imebainika na haraam imebainika na baina ya mawili hayo mna yenye kutia shaka. Wengi miongoni mwa watu hawayajui. Basi atakayejiepusha yenye kutia shaka, atakuwa amejiepushia shaka katika Dini yake na heshima yake.
Na Atakayetumbukia katika yenye kutia shaka, ataingia kwenye haraam. Kama mchunga anayechunga kando ya mipaka, ni haraka kulisha humo (mpaka mwingine wa watu). Zindukeni! Kila mfalme ana mipaka. Zindukeni! Kwa yakini mipaka ya Allaah ni haraam Alizoziharamisha.
Zindukeni! Kwa yakini katika mwili mna kinofu cha nyama, kinapokuwa salama, mwili wote unakuwa salama. Kinapoharibika, mwili wote unaharibika. Zindukeni! Kinofu hicho ni moyo.” [Al-Bukhaariy na Muslim]
Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.
Download NowJe umeipenda post hii ?
Maana ya SunnahKilugha: Neno sunnah katika lugha ya Kiarabu lina maana ya mwenendo au mila.
Soma Zaidi...Wapo watu kadhaa ambao waliomba dua hazirudi. Hapa nitakueleza wawili ambao ni mzazi na msafiri.
Soma Zaidi...