MAANA YA HADITHI SUNNAH

MAANA YA HADITHI SUNNAH

Maana ya SunnahKilugha: Neno sunnah katika lugha ya Kiarabu lina maana ya mwenendo au mila.

Download Post hii hapa

MAANA YA HADITHI SUNNAH

Maana ya Sunnah
Kilugha: Neno sunnah katika lugha ya Kiarabu lina maana ya mwenendo au mila. Hivyo ukisema "Sunnat Muhammad (s.a.w)" ina maana ya mwenendo au tabia au mila aliyokuwa akiifuata Mtume Muhammad (s.a.w) katika maisha yake ya kila siku. Na ikisemwa, "Sunnatullah" kama ilivyotumika katika Quran, ina maana ya desturi au kawaida au mila ya Allah (s.w) katika kufanya mambo ya Uungu wake kama tunavyojifunza katika aya ifuatayo: β€œHii ni kawaida (sunnah) ya Allah (ya kuwaadhibu wakorofi) iliyokuwa kwa waliopita zamani, hutapata mabadiliko katika kawaida (sunnah) ya Allah." (33:62)

Kisheria, sunnah ni mwenendo au matendo ya Mtume (s.a.w) ambayo ni sehemu ya Utume wake. Waislamu wanalazimika kuyaiga na kuyafuata katika uendeshaji wa maisha yao ya kila siku ili kupata radhi za Allah (s.w). Mwenendo wa Mtume (s.a.w) haukutokana na matashi yake bali ulikuwa ni wahyi kutoka kwa Allah (s.w) kama inavyothibitika katika Qur-an: β€œNa hazungumzi (Muhammad) kwa matamanio ya nafsi yake.Isipokuwa (anayozungumza ni) wahyi uliofunuliwa kwake." (53:3-4)Β 

Kiutendaji, sunnah ya Mtume (s.a.w) ni yale matendo ya msingi aliyoyafanya, aliyoyaagiza na yaliyofanywa mbele yake asiyakemee au kuyakataza.

Maana ya Hadith
Kilugha: maana ya Hadith katika lugha ya Kiarabu ni jambo jipya au kitu kipya", hutuba, taarifa, maelezo au mapokezi. Katika Qur-an neno "Hadith" limetumiwa kwa maana hizi kama ilivyo katika aya ifuatayo: Basi simulizi gani baada ya hizi (simulizi za Qur-an) wataziamini?" (77:50) Kisheria, Hadith za Mtume (s.a.w) ni simulizi (mapokeo) au taarifa juu ya yale yote aliyoyafanya Mtume (s.a.w) katika kuufundisha Uislamu kinadharia na kimatendo au juu ya yale yaliyotendwa mbele yake akayakataza au akayaridhia au maelezo juu ya mwenendo na tabia ya Mtume (s.a.w). Ifuatayo ni mifano ya Hadith za Mtume (s.a.w):

(i)Maelezo au maelekezo ya Mtume (s.a.w)
Amesema Mtume (s.a.w) "Mwenye kumueleza mwenzake jambo la kheri anapata malipo sawa na mtendaji wa kheri hiyo." (ii)Vitendo vya Mtume (s.a.w)
Amesema Bibi Aysha (r.a): "Mtume (s.a.w) alikuwa akiswali swala ya Dhuha rakaa nne na mara nyingine huzidisha atakazo." (iii) Kukubali (kuridhia)
Amesema Bibi Aysha (r.a): "Mtume (s.a.w) aliwapeleka askari kwenye vita, kiongozi wao alikuwa akipendelea sana kusoma suratul- Ikhlasi katika swala. Waliporejea waliripoti kwa Mtume (s.a.w) jinsi Imamu wao alivyokuwa anafanya, Mtume (s.a.w) akasema: "Muulizeni kwanini alifanya hivyo." Wakamuuliza naye akajibu kwamba suratul- Ikhlas ni sifa za Mwenyezi Mungu na yeye anapenda kuzisema. Mtume (s.a.w) akasema: "Mwambieni kwamba na yeye Mwenyezi Mungu anampenda." (iv) Sifa au Mwenendo wa Mtume (s.a.w)
"Amesema Sayidna Ali (r.a), Mtume (s.a.w) alikuwa mwenye elimu, mpole na mkarimu. Mwenye kumuona Mtume (s.a.w) huvutiwa naye na kumfuata."


                   

Download Post hii hapa

Jiunge nasi WhatsApp
Upate Update zetu

Download App Yetu

Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.

Download Now Bongoclass Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 1970-01-01 03:33:44 Topic: Main: Dini File: Download PDF Views 1001

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
πŸ‘‰1 Kitabu cha Afya    πŸ‘‰2 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)    πŸ‘‰3 Bongolite - Game zone - Play free game    πŸ‘‰4 Simulizi za Hadithi Audio    πŸ‘‰5 Madrasa kiganjani    πŸ‘‰6 kitabu cha Simulizi   

Post zinazofanana:

DARSA ZA TAWHID
DARSA ZA TAWHID

Jifunze tawhid yaani kumpwekesha Allah subhaanah wata'aala

Soma Zaidi...
mgawanyiko katika quran
mgawanyiko katika quran

MGAWANYIKO KATIKA QURAN Juzuu, Sura, Aya, Manzil, Qara Wataalamu wa elimu za Qurani katika fani za uandishi na usomaji wameigawanya Qurani katika mafungu ili kuwezesha urahisi kwa wasomaji wa qurani.

Soma Zaidi...
NDANI YA SHIMO LA KABURI
NDANI YA SHIMO LA KABURI

Download kitabu Hiki Bofya hapa NDANI YA PANGO LA MAKABURI Mmoja wapo akatowa kamba na kulifunga jeneza vizuri na kuanza kulishusha chini ya mapango kwa kamba ile.

Soma Zaidi...