HADITHI YA 04

عَنْ أَبِي عَبْدِ الرَّحْمَنِ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ مَسْعُودٍ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ قَالَ: حَدَّثَنَا رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه و سلم -وَهُوَ الصَّادِقُ الْمَصْدُوقُ-: "إنَّ أَحَدَكُمْ يُجْمَعُ خَلْقُهُ فِي بَطْنِ أُمِّهِ أَرْبَعِينَ يَوْمًا نُطْفَةً، ثُمَّ يَكُونُ عَلَقَةً مِثْلَ ذَلِكَ، ثُمَّ يَكُونُ مُضْغَةً مِثْلَ ذَلِكَ، ثُمَّ يُرْسَلُ إلَيْهِ الْمَلَكُ فَيَنْفُخُ فِيهِ الرُّوحَ، وَيُؤْمَرُ بِأَرْبَعِ كَلِمَاتٍ: بِكَتْبِ رِزْقِهِ، وَأَجَلِهِ، وَعَمَلِهِ، وَشَقِيٍّ أَمْ سَعِيدٍ؛ فَوَاَللَّهِ الَّذِي لَا إلَهَ غَيْرُهُ إنَّ أَحَدَكُمْ لَيَعْمَلُ بِعَمَلِ أَهْلِ الْجَنَّةِ حَتَّى مَا يَكُونُ بَيْنَهُ وَبَيْنَهَا إلَّا ذِرَاعٌ فَيَسْبِقُ عَلَيْهِ الْكِتَابُ فَيَعْمَلُ بِعَمَلِ أَهْلِ النَّارِ فَيَدْخُلُهَا. وَإِنَّ أَحَدَكُمْ لَيَعْمَلُ بِعَمَلِ أَهْلِ النَّارِ حَتَّى مَا يَكُونُ بَيْنَهُ وَبَيْنَهَا إلَّا ذِرَاعٌ فَيَسْبِقُ عَلَيْهِ الْكِتَابُ فَيَعْمَلُ بِعَمَلِ أَهْلِ الْجَنَّةِ فَيَدْخُلُهَا".
[رَوَاهُ الْبُخَارِيُّ]

Kwa mapokezi ya Abdullah ibn Masood (ra), ambaye alisema:Mjumbe wa Allaah ((s.a.w)), na yeye ni mkweli, aliyeaminiwa, ametusimulia sisi kuwa, "Hakika uumbaji wa kila mmoja wenu unakusanywa katika tumbo la mama yake kwa siku arobaini katika umbo la nutfah (tone la manii).

kisha anakuwa alaqah (tone la damu) kwa kipindi kama hicho, kisha anakuwa mudgha (pande la nyama) kwa kipindi kama hicho, kisha hutumwa kwake malaika atakayempulizia roho yake ndani yake na ameamrishwa mambo manne : kuandika rizq yake (riziki), maisha ya muda wake, vitendo vyake, na ikiwa vya heri au vya shari (yaani, ikiwa ataingia Peponi).

Na ninaapa kwa yule, ambaye hakuna Muungu isipokuwa Yeye, kwa hakika mmoja wenu anatenda vitendo vya watu wa Peponi hadi kutakapokuwa na urefu wa dhiraa kati yake na hiyo pepo, na yale yaliyoandikwa yatamtangulia, na kwa hivyo atafanya. vitendo vya watu wa Motoni na kwa hivyo atauiingia; na kwa hakika mmoja wenu atatenda vitendo vya watu wa Motoni, mpaka itakuwa kati yake na pepo ni urefu wa dhiraa, na yale ambayo yameandikwa yatamtangulia na atafanya vitendo vya watu wa Peponi na atainaingia peponi"[Bukhari & Muslim]،