image

UANDISHI WA HADITHI WAKATI WA MASWAHABA

Wakati wa Masahaba wa Mtume (s.

UANDISHI WA HADITHI WAKATI WA MASWAHABA

Wakati wa Masahaba wa Mtume (s.a.w)11-100. A.H
Kipindi hiki ambacho kimechukua kama karne moja hivi kuanzia pale alipotawafu Mtume (s.a.w) mpaka kutawafu kwa sahaba wa mwisho. Sahaba wa mwisho, Anas bin Malik alifariki 91 A.H. Hiki ni kipindi cha Makhalifa wanne waongofu na Masahaba mashuhuri wa Mtume (s.a.w).. Ni katika kipindi hiki ambapo Dola ya Kiislamu ilitanuka sana. Matatizo mengi ya wakati huu yalitatuliwa kwa kutegemea hukumu za Hadith zilizohifadhiwa vifuani mwa Masahaba. Kwa mfano, baada ya kutawafu Mtume (s.a.w),zilijitokeza kesi ambazo zilionesha umuhimu wa kuhifadhiwa Hadith kama vile: "Mtume azikwe wapi - Makka au Jerusalem?" Ikatolewa Hadith ya Mtume isemayo: "Mtume azikwe afiapo." Hadith ikamaliza tatizo.

Katika kipindi cha Makhalifa wanne waongofu kazi ya uandishi ilikuwepo, lakini haikuwa katika kiwango kikubwa. Kazi kubwa ya kwanza ya uandishi wa Hadith iliyoonekana katika kipimdi hiki ni ile ya kitabu cha Hadith - "Alqatadaya cha 'Ali (r.a) aliyefariki 40 A.H. Pia palikuwa na Juzuu (Pamphlet) ya Hadith ya Ibn 'Abbas (r.a) aliyoiandika muda mrefu baada tu ya kutawafu Mtume (s.a.w). Ibn 'Abbas (r.a) alifariki 61 A.H. Hazrat 'Ali na Ibn 'Abbas japo walikuwa wanazuoni wakubwa, kazi yao hii ndogo, haikuwa inatosheleza mahitaji ya wakati huo.

Katika kipindi hiki haja kubwa ya kuhifadhi Hadith katika maandishi ilijitokeza baada ya kutokea matatizo ya kisiasa, palipotokea makundi mawili: Kundi la 'Ali na kundi la Mu'awiayh. Hadith zilianza kutumiwa vibaya kwa maslahi ya kikundi. Kila kikundi kilikubaliana tu na Hadith zile zinazotetea upande wake. Vile vile kulizuka Hadith nyingi za uongo. 

Ikumbukwe pia katika wakati huu wa Historia, dola ya Kiislamu ilikuwa imepanuka sana na kwa hiyo ulikuwepo uwezekano mkubwa wa kuzusha Hadith za uongo. Hii ndio sababu iliyomsukuma kiongozi aliyekuja baadaye kabisa 'Umar bin 'Abdul-Azizi (101 A.H.) achukuwe dhima ya kuchuja na kuandika Hadith zilizo sahihi. Chini ya uongozi wake vitabu kadhaa viliandikwa na ziliwekwa sheria za kutambua asili ya Hadith na maisha ya wapokezi hasa kuhusu mwenendo na msimamo wao. Watu wawili walifanya kazi hii, Ibn Shihab Al-Zuberi na Abu Bakr al-Hazm.


                   





           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 105


Sponsored links
👉1 Kitabu cha Afya     👉2 Madrasa kiganjani     👉3 kitabu cha Simulizi     👉4 Kitau cha Fiqh    

Post zifazofanana:-