image

UANDISHI WA HADITHI WAKATI WA TABI'INA

Wakati wa Wafuasi wa masahaba (Tabi'ina)101-200 A.

UANDISHI WA HADITHI WAKATI WA TABI'INA

Wakati wa Wafuasi wa masahaba (Tabi'ina)101-200 A.H
Hiki ni kipindi cha wafuasi wa Masahaba wa Mtume (s.a.w) katika karne ya pili Hijiriyyah 101-200 A.H. Katika kipindi hiki walitokea wanazuoni wengi waliojizatiti katika kazi ya ukusanyaji wa Hadith kutoka katika vituo mbali mbali vya mafunzo (Centres of Learning). 

Wafuatao ni baadhi ya wanazuoni wa Hadith (Muhaddithina) waliojitokeza kutoka miji mbali mbali. Ma'mar bin Rashi wa Baghdadi; Said bin Abi Ubadah na Rabia bin Sabin wa Basra; Ibn Harith wa Baghdad; Abdul Malik bin Juraiji wa Makka; Walid bin Mubarrak wa Khurasan; Abu Bakr Shyaban wa Kufa na Sufyan bin Uyaina wa Madina.

Japo wanazuoni hawa walijitahidi sana katika hii kazi ya ukusanyaji Hadith, kazi zao bado hazikuwa zenye kutosheleza; isitoshe sehemu kubwa ya vitabu vyao ilihusu ripoti ya vituo vyao. Baada ya kazi hizi, kilitokea kitabu cha "al-Muwatta" cha Imam Malik bin Anas aliyeishi Madina kati ya 95 A.H na 179 A.H. Kazi ya Imam Malik ndiyo ya kwanza iliyowekwa katika mpango mzuri na kuwa kitabu cha kutegemewa na Umma. Imam Malik alifutu mas-ala ya Uislamu kwa kutegemea Qur-an na Hadith tu. Alianzisha umoja wa "Ahli Hadith" ambao kazi yake ilikuwa ni kukusanya Hadith na kuzitekeleza katika matendo.

Katika wakati huo huo alitokea Imam Abu Hanifa al-Numan bin Thabit (80-150) aliyefutu mas-ala mbali mbali ya Kiislamu kwa hoja na Qiyasi (deductions) baada ya kuzingatia Qur-an, Hadith na Ijma'i (makubaliano ya wanavyuoni). Hakuandika kitabu chochote cha Hadith lakini alikuwa mwanazuoni mkubwa wa "Qur-an na Hadith na alikuwa Muj-tahid na Mcha-Mungu.

Katika kipindi hiki hiki palitokea Maimamu wengine wawili mashuhuri. Imam Muhammad bin Idris al-Shafii (150-240 A.H.) aliyezaliwa Palestine mji wa Ghazza, na mwingine ni Imam Ahmad bin Hambal (164-241 A.H.) aliyezaliwa Baghdad na kujulikana sana kwa kitabu chake cha Isnad ya Ibn Hambali kilichokuwa na Hadith zaidi ya 30,000 alizokusanya.


                   





           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 91


Sponsored links
👉1 Madrasa kiganjani     👉2 Kitabu cha Afya     👉3 kitabu cha Simulizi     👉4 Kitau cha Fiqh    

Post zifazofanana:-