Umuhimu wa uchumi katika uislamu

2.

Umuhimu wa uchumi katika uislamu

2. Umuhimu wa uchumi katika Uislamu
Mwanaadamu ameumbwa na mahitajio mengi ambayo hana budi kuyapata ili aweze kuishi kwa furaha na amani hapa ulimwenguni. Kwa kuwa mwanaadamu ni mchanganyiko wa mwili na roho, pia mahitajio yake yamegawanyika, ana mahitajio ya kiroho na kimwili. Mahitajio ya kiroho ambayo humuwezesha mwanaadamu kuishi maisha ya utulivu yenye furaha na amani, hupatikana kwa kufuata kwa utii na unyenyekevu mwongozo wa Allah (s.w).



Mahitajio ya kimwili kama vile chakula, mavazi, vipando na njia ya uchumi hupatikana kwa kuchapakazi chini ya mazingira yatokanayo na itikadi sahihi yenye kusimamiwa na viongozi wanaozingatia haki itokayo kwa Muumba. Katika Qur-an tunafahamishwa kuwa Allah (s.w) amejaalia mali anayoichuma mwanaadamu iwe ndiyo inayoboresha maisha yake: 'Wala msiw ape w apumbavu mali zenu ambazo Mw enyezi Mungu amezijaalia kwa ajili ya maisha yenu ' (4:5)


Kutokana na aya hii, kuchuma mali si jambo la hiari kwa mwanaadamu kwani kwa namna Allah (s.w) alivyokadiria, maisha ya mwanaadamu kwa hapa ulimwenguni hayawezekani pasi na kuchuma. Ni kweli kwamba vitu vyote vilivyomzunguka mwanaadamu katika ulimwengu huu vimeumbwa kwa ajili yake kwa ushahidi wa Qur-an: 'Yeye ndiye aliyekuumbieni vyote vilivyomo katika ardhi' (2:29).



Lakini mara nyingi vitu hivi haviko katika hali ya kutumiwa na mwanaadamu moja kwa moja. Bali mwanaadamu analazimika kutumia elimu yake, Maarifa yake, juhudi zake na vipawa vyake vingine ili ayabadilishe mazingira yake yaweze kumtumikia na kukidhi haja zake.
Kwa mtazamo huu Uislamu unatuamrisha kuchuma kama unavyotuamrisha kusimamisha Swala, kutoa Zakat na kutekeleza Ibada nyingine maalumu kama hizi:


Na itakapokwisha swala, tawanyikeni katika ardhi mtafute fadhila za Mwenyezi Mungu na mkumbukeni Mwenyezi Mungu kwa wingi, ili mpate kufaulu. (62:10)
Tunajifunza kutokana na aya hii kuwa, kuchuma ni wajibu unaompasa Muislamu mara tu baada ya kutekeleza Ibada maalum. Hili linabainishwa katika Hadithi ifuatayo:
'Abdullah bin Mus 'ud ameeleza kuwa Mtume (s.a.w) amesema: Kutafuta chumo la halali ni faradhi baada ya kutekeleza faradhi nyingine.' (Baihaqi).
Pia Mtume (s.a.w) amebainisha wazi ubora wa kujizatiti katika kutafuta chumo la halali kwenye Hadith ifuatayo:



'Miqdam bin Ma 'ad Yakrab ameeleza kuwa Mtume wa Allah amesema: Hapana mmoja wenu aliyekula chakula kizuri kuliko kile alichokula kutokana na kazi ya mkono wake mwenyewe. Na Daud, Mtume wa Allah, alikuwa anakula kutokana na kazi ya mikono yake.' (Bukhari)



Kwa upande mwingine Uislamu unalaani uvivu na kuwategemea wengine pasi na sababu au dharura maalum kama tunavyojifunza katika Hadith zifuatazo:
'Jubair bin Awam ameeleza kuwa Mtume wa Allah amesema: Mmoja wenu kuchukua kamba na kisha akaja na mzigo wa kuni akiwa amebeba mgongoni mwake na akauuza, na kwakufanya hivyo Allah akailinda hadhi yake, ni bora kwake kuliko kuomba omba watu, wakimpa chochote au wasimpe (Bukhari.)



Mpaka hapo tumejifunza kuwa kwa mtazamo wa Uislamu, uchumi ndio msingi wa maisha ya mwanadamu hapa ulimwenguni na Uislamu umewajibisha kuchuma kwa kila mwenye uwezo. Ni makosa katika Uislamu mtu mwenye uwezo na afya kubweteka na kuwategemea wengine katika kukidhi mahitaji yake.




                   




Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2018-08-01     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 164


Download our Apps
👉1 kitabu cha Simulizi     👉2 Kitabu cha Afya     👉3 Kitau cha Fiqh     👉4 Madrasa kiganjani    

Post zifazofanana:-

Quran si maneno ya shetani
Soma Zaidi...

DARSA ZA TAWHID
Jifunze tawhid yaani kumpwekesha Allah subhaanah wata'aala Soma Zaidi...

Faida za Kuwa mwenye Subira na Uvumilivu
29. Soma Zaidi...

Hadithi Ya 29: Muabudu Allaah Na Usimshirikishe Na Chochote
Soma Zaidi...

HIKUMU YA BASMALLAH YAANI KUSOMA BISMILLAH
Jifunze namna ya kusoma quran, pata mafunzo ya tajwid hapa Soma Zaidi...

Masharti ya swala
Sharti za SwalaSharti za Swala Sharti za swala ni yale mambo ya lazima anayotakiwa Muislamu ayachunge na kuyatekeleza kabla hajaanza kuswali. Soma Zaidi...

Mafunzo Yatokanayo na Historia ya Zakaria(a.s) na Yahya(a.s)
Kutokana na Historia ya Nabii Zakaria (a. Soma Zaidi...

Mtume hakufundishwa quran na Jabir na Yasir
Soma Zaidi...

Historia ya Mwanadamu
Soma Zaidi...

dharura
14. Soma Zaidi...

Usimamizi wa Haki na haki za binadamu Katika Dola ya Kiislamu
Soma Zaidi...

KAZI ALIZOFANYA MTUME MUHAMMAD (S.A.W) KABLA YA UTUME
KAZI ALIZOKUWA AKIFANYA MUHAMMAD (S. Soma Zaidi...