(c) Hifadhi ya Mwanamke na Maadili ya JamiiKimaumbile wanaadam kama walivyo wanyama, wamejaaliwa kuwa na mvuto wa kimapenzi kati ya mume na mke ili kuwawezesha kutekeleza wajibu mkubwa wa kuzaana na kuendeleza kizazi.
(c) Hifadhi ya Mwanamke na Maadili ya Jamii
Kimaumbile wanaadam kama walivyo wanyama, wamejaaliwa kuwa na mvuto wa kimapenzi kati ya mume na mke ili kuwawezesha kutekeleza wajibu mkubwa wa kuzaana na kuendeleza kizazi. Wanyama, matamanio yao ya kukutana dume na jike yanakuwa juu kwa kipindi maalum, pale wanapokuwa tayari kuanzisha uzazi. Tofauti na wanyama, matamanio ya mwanadamu ya kukutana kimwii kati ya mwanamume na mwanamke yako juu siku zote alimradi tu vipatikane vishawishi. Kalika hali hii, endapo wanaume na wanawake wataachiwa huru kuchanganyika na kuingiliana pasina kuwekewa mipaka, watakidhi matamanio yao hadharani kama wanyama na pengine zaidi ya wanyama. Hali hii
tumeiona katika jamii za Ulaya na Marekani baada ya kutolewa uhuru kwa wanawake kuchanganyika na kubusiana na wanaume wependavyo na bila ya mipaka. Athari ya uhuru huu kwa jamii ya Ulaya na Marekani tumeiona katika kushamiri kwa umalaya, kuenea magonjwa ya zinaa, kuwa na watoto wa nje ya ndoa, kuvunjika kwa familia, n.k. Lakini aliyeathirika zaidi ni mwanamke ambaye uke wake umefanywa ni bidhaa ya kuuzwa na kununuliwa na urembo wake umefanywa ni chombo cha matangazo ya biashara.
Allah (s.w) hakujaaliwa mvuto wa mapenzi kati ya mwanamume na mwanamke, ili kumdhalilisha mwanamke na kuiangamiza jamii, bali amejaalia mvuto huu wa kimapenzi kati ya mume na mke ili wanadamu waweze kuendeleza kizazi na kuishi maisha ya kijamii yaliyojcngwa juu ya misingi imara ya upendo na ushirikiano;
Na katika ishara Zake ni kuwa amekuumbieni wake zenu katika jinsia yenu iii mpate utulivu kwao, naye amejaalia mapenzi 'na huruma baina yenu (30:21).
Ili tuweze kufikia lengo hili, Allah (s.w) ametuwekea utaratibu maalum wa mahusiano kati ya wanaume na wanawake. Allah (s.w) ameturuhusu, wanaume na wanawake, tukidhi matashi ya kimaumbile kati ya mwanamke kwa njia ya ndoa na ametuharamishia mahusiano yoyote kati ya mume na mke nje ya mipaka ya ndoa. Ili kurahisisha maisha ya ndoa na kuyafanya mahusiano kati ya mume na mke nje ya ndoa yawe magumu, Uislamu umeweka vipengele kadhaa vya kuihifadhi jamii na zinaa:
(i)Kujitakasa mtu binafsi (ucha-Mungu)
(ii)Kutoa adhabu kali kwa wazinifu
(iii)Kutokomeza vishawishi vya zinaa
(i) Kujitakasa Mtu binafsi (ucha-Mungu)
Ucha-Mungu ni kuishi kwa kuchunga mipaka ya Allah (s.w) kwa unyenyekevu. Imani thabiti ndio nyenzo kubwa ya kumuwezesha mja kuchunga mipaka ya Allah (s.w). Muumini wa kweli ni yule anayefuata kwa ukamilifu sheria ya Kiislamu katika maisha yake yote kwa kuhakikisha kuwa anafuata maamrisho yote ya Allah (s.w) na kuacha makatazo yake yote. Kwa Muumini huyu anachohitajia ni kujua tu Allah (s.w) na Mtume wake wamearisha nini na wamekataza nini. Muislamu mcha-Mungu atakapojua kuwa jambo fulani limekatazwa katika kitabu cha Allah (s.w) kama vile zinaa ilivyoharamishwa katika aya kadhaa (rejea Qur'an: 17:32), hatajiepusha na kulitenda tu bali hata pia kuliwaza.
Miongoni mwa nyenzo zilizowekwa na Uislamu ili kumuwezesha mtu binafsi kuepukana na tendo ovu Ia zinaa ni kuwasisitiza waumini kuwa na haya, kujiepusha na fikra mbaya juu ya wanawake/wanaume, kujiepusha na kutizama kwa matamanio na wanawake kujiepusha na kushawishi kwa sauti kali, kudhihirisha mapambo na kupaka manukato makali.
"Haya" ni msingi wa Imani na ngao ya kumkinga mtu na maovu. llivyo ni kwamba matendo maovu kama vile uzinifu, wizi, uwongo, n.k. ambavyo mwanaadam huyatenda kutokana na msukumo wa matashi ya unyama wake, yanampelekea kwenda kinyume na utu wake. Matendo yote maovu yameelezwa katika Qur'an kwa neno "Munkar" lenye maana "isiyojulikana" au "jambo geni". Vitendo hivi vimeitwa "Munkar' kwa sababu ni vigeni katika utu wa mwanaadam. Mwanaadam ameumbwa na nguvu ya kupigana ndani kwa ndani na maovu. Nguvu hii ni "haya".
Nguvu hii ipo kwa kila mtu lakini inahitaji kuamshwa kwa kupewa mara kwa mara mafundisho ya maadili ya Uislamu. Katika kuonesha nafasi ya "haya" katika maadili ya Uislamu Mtume (s.a.w) amesema: 'Kila dini ma maadili yake na maadili ya Uislam ni 'Haya ". "Haya" ndiyo inayomuwezesha mwanaadam kujiepusha na maovu bila ya nguvu za polisi. Kinyume chake mtu asiye na haya hufanya ovu lolote alitakalo. Mtume (s.a.w) kasema: 'Unapokuwa huna haya unaweza kufanya ulitakalo ".
Muislam katika kujiepusha na matendo maovu na machafu, hawaonei haya wanaadam wenziwe tu bali humuonea haya zaidi Mwenyezi Mungu ambaye yu karibu yake zaidi kuliko mshipa wake mkuu wa damu (Jugular vein). Mtume (s.a.w) amesema: <<Allah (s.w) anahaki zaidi ya kuonewa haya" (Tirmidh). Kama mtu anaona haya kutenda kitendo kiovu mbele ya watu, basi aone haya zaidi kutenda kitendo hicho mbele ya Allah (s.w).
Je! umeipenda hii post?
Ndio Hapana Save post
Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Topic: Fiqh Main: Post File: Download PDF Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 476
Sponsored links
👉1 Madrasa kiganjani
👉2 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)
👉3 Simulizi za Hadithi Audio
👉4 Kitabu cha Afya
👉5 Kitau cha Fiqh
👉6 kitabu cha Simulizi
Tathmini ya swala zetu, kwa nini swala zetu hazijibiwi?
Soma Zaidi...
Jinsi ya kuswali swala vitani
Post hii itakufundisha taratibu zinazofanyika ilibkuswalibukiwa vitani. Soma Zaidi...
Kusimamisha swala.
Kwenye kipengele hiki tutajifunza maana ya swala ni nin?. Na masharti ya swala. Soma Zaidi...
Haya ndio yanayobatilisha Hija
Soma Zaidi...
Namna ya Safari ya Hija inavyoanza
Soma Zaidi...
Ni mambo yapi hupunguza Swawabu na malipo yamwenye kufunga
Soma Zaidi...
MTAZAMO WA UISLAMU JUU YA ELIMU
Maana ya elimuElimu ni ujuzi ulioambatanishwa na utendaji. Soma Zaidi...
Ni yapi masharti ya Udhu na kujitwaharisha
Soma Zaidi...
Taratibi za malezi ya watoto wadogo baada ya talaka katika uislamu
Endapo mke na mume wameachana na hali ya kuwa mke ana watoto wachanga. Je uislamu unasemaje kuhusu taratibu za malezi? Soma Zaidi...
NAMNA YA KUSWALI: NIA YA SWWALA, NA KUPIGA TAKBIRA (yaani kusema Allah akbar)
Mtume (s. Soma Zaidi...