Aina za talaka zinazo rejewa

Aina za talaka zinazo rejewa

Ama za Talaka



Kuna ama nyingi za talaka ambazo ni vyema kila Muislamu akazifahamu. Kutojua talaka inavyopatikana, mtu anaweza kukaa na mke aliyekwisha achika kitambo. Kuna ama nyingi za talaka lakini tunaweza kuzigawanya kwenye makundi makuu mawili:
(1)Talaka Rejea.
(2)Talaka isiyorejewa.



I .Talaka Rejea
Talaka rejea ni ama yoyote ya talaka ambayo inampa mtu fursa ya kumrejea mkewe baada ya kumpa talaka na baada ya kuona kuwa kuna haja ya kusuluhishana na kurejeana. Kuna ama kubwa mbili za talaka rejea.
(a)Talaka moja. (Talaki-Ahsan).
(b)Talaka mbili (Talaki-Hasan).



(a)Talaka Moja:
Talaka moja hupatikana baada ya mume mwenye akili timamu kumtamkia mkewe akiwa katika twahara maneno ya kudhihirisha dhamira ya kumwacha kama vile: "Nimekuacha", baada ya eda kwisha mkewe huyo atakuwa ameachika kwa talaka moja.



(b)Talaka Mbili:
Katika ama hii ya talaka, mume baada ya kushindwa kufikia suluhu na mkewe, huamua kumuacha kwa talaka mbili kwa kumuandikia au kumtamkia kuwa amemuacha katika twahara ya kwanza (kama tulivyoona katika talaka moja), kisha kumtamkia tena kuwa amemuacha talaka ya pili katika twahara ya pili au ya tatu. Pia inahesabiwa talaka mbili kama baada ya kutoa talaka moja, wawili walipatana na kurejeana kabla ya kipindi cha eda kwisha,kisha wakakosana wakati mwingine kiasi cha kufikia hatua ya mume kutoa talaka nyingine. Vile vile kama wawili baada ya kuachana kwa talaka moja, watafikia maafikiano ya kuoana tena kisha wakagombana tena kiasi cha kupeana talaka, zitahesabika talaka mbili.



Utaratibu mwingine wa kuacha kwa talaka mbili ni sawa tu na ule wa kuacha kwa talaka moja tuliouona. Hii nayo ni talaka rejea, kwa maana ya kwamba mtu anaweza kumrejea mkewe kabla ya kipindi cha eda kwisha. Pia baada ya kuachana mwanamume anaruhusiwa kufunga tena ndoa na mke aliyemuacha endapo wataelewana na akiwa bado hajaolewa na mume mwingine. Mke aliyeachwa kwa talaka zaidi ya mbili harejewi tena kama inavyosisitizwa katika Qur-an:


Talaka (unazoweza kumrejea mwanamke) ni (zile zilizotolewa) mara mbili. Kisha kumuweka kwa wema au kumwacha kwa ihsani... (2:229).
Ama nyingine za talaka rejea ni hizi zifuatazo



(c)Talaka ya 'IIaa
Ama hii ya talaka inapatikana kwa mtu kuamua kujitenga na mkewe zaidi ya miezi mine. Katika jamii za kijahilia palikuwa na tabia ya wanaume, kwa sababu mbali mbali, kuapa kutofanya tendo Ia ndoa na wake zao kwa kipindi kisichojulikana. Uislamu unamruhusu mtu kutengana na mkewe kwa kipindi kisichozidi miezi mine.


Kwa wale wanaoapa kwamba watajitenga na wake zao (muda wao) ni kungojewa miezi mine. Na kama wakirejea (wakatangamana na wake zao) basi Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa kusamehe (na) mwingi wa kurehemu. (2:226).



Baada ya miezi mine kupita bila ya mume kumrejea mkewe, ndoa itavunjika, bila hata ya kutamka kuwa amemuacha. Kama atataka kumrejea tena mkewe itambidi afunge ndoa upya. Ni kwa mtazamo huu vile vile, mwanamke ana haki ya kudai talaka mbele ya kadhi endapo mumewe atakuwa amemsusa (amemuacha bila ya maagano yoyote) zaidi ya miezi mine. Mwanamke huyu atakuwa ameachika Kiislamu na atakuwa huru kuolewa na mume mwingine. Hekima ya hukumu hii ni kuwapa wanawake haki zao na uhuru wao wanaostahiki.



(d)Talaka ya Zihaar
Katika jamii ya Waarabu wakati wa ujahili, palikuwa na ama nyingine ya kumsusa mke kwa kumwambia: "Ninakuona kama mgongo wa mama yangu". Baada ya mume kutamka maneno haya hakuwa tena anamuingilia mkewe na kumtekelezea vilivyo haki zake nyingine na wala hakuwa anamwacha ili apate kuolewa na mume mwingine. Uislamu umekataza desturi hii na kuwaadhibu vikali wale wanaofanya hivyo kama tunavyojifunza katika aya zifuatazo:


Mwenyezi Mungu amekwisha sikia usemi wa mwanamke yule anayejadiliana nawe sababu ya mumewe, na anashtaki mbele ya Mwenyezi Mungu; na Mwenyezi Mungu anayasikia majibizano yenu; hakika Mwenyezi Mungu ni mwenye kusikia, mwenye kuona. Wale miongoni mwenu wawaambiao wake zao kuwa wanawaona kama mama zao (kwa hivyo wakajiepusha nao wasiwaingilie, wala wasiwape ruhusa ya kuolewa na waume wengine); hao si mama zao. Hawakuwa mama zao ila wale walio wazaa wanasema neno baya na la uwongo. Na Mwenyezi Mungu ni mwenye msamaha, mwenye maghfirah. (58:1-2)



Na wale wawaitao wake zao mama zao, kisha wakarudia katika yale waliyoyasema (wakataka kuwarejea wake zao wakae kama mke na mume), basi wampe mtumwa uhuru kabla ya kugusana. Mnapewa maonyo kwa haya. Na Mwenyezi Mjungu anajua mnayoyatenda Na asiyepata (mtumwa) basi afunge saumu ya miezi miwili mfululizo kabla ya kugusana; na asiyeweza basi awalishe maskini sitini (kila maskini kibaba kimoja). (Mmeamrishwa) haya ili mumuamini Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na hiyo ni mipaka ya Mwenyezi Mungu; na kwa makafiri iko adhabu iumizayo. (58:3-4)



Tunajifunza katika aya hizi kuwa, mtu akimsusia mkewe kwa kumwambia kuwa anamuona kama mama yake anaharamishiwa mkewe na hawezi tena kumrejea kama mkewe mpaka atoe kafara kwa:


(a)Kumwacha mtumwa huru.
(b)Kama hana mtumwa, kufunga miezi miwili mfululizo (bila ya kupumzika katikati).
(c)Kama hana uwezo wa kufunga kwa sababu za kisheria zinazomruhusu mtu kutofunga Ramadhani, atalisha maskini sitini.



Kama mtu hatatekeleza adhabu hii kwa hiari yake, mahakama ya Kiislamu itaingilia kati na kumlazimisha kufanya hivyo, iii mkewe awe halali kwake. Muda wa miezi mine ukipita kabla hajatekeleza adhabu hii, mkewe atakuwa ameachika kama ilivyo katika talaka ya 'lila. Mkewe atakuwa hum kuolewa na mume yeyote aliye halali kwake. Pia mume anaweza kumrejea mkewe kwa ndoa mpya, endapo atamuwahi kabla hajaolewa na mwingine lakini pia kwa kutekeleza adhabu iliyotolewa, Qur'an 58:3-4).



(e)Talaka ya KhuI
Hii ni ama ya talaka ambayo inapatikana kwa mwanamke kudai aachwe. Kama mwanamke atakuwa hapati furaha na amani katika ndoa ya mume aliye naye, kwa sababu zake mwenyewe ana haki ya kudai talaka kwa mumewe na itabidi mumewe ampe talaka kwa kufuata utaratibu wa kawaida wa kutoa talaka, na baada ya kipindi cha eda, mwanamke atakuwa ameachika. Kama mke amedai apewe talaka kwa sababu zake mwenyewe bila ya mumewe kumnyima haki yake yeyote, atalazimika kumrudishia mumewe mahari, iii iwe kikomboleo kwake.Hata hivyo, wanaume wanaweza kusamehe mahari hayo. Ilivyo kawaida mwanamume haruhusiwi kudai mahari kama ndiye aliyetoa talaka, kama inavyobainishwa katika Qur-an:


Wala si halali kwenu kuchukua chochote mlichowapa (wake zenu), isipokuwa (wote wawili,) wakiogopa ya kwamba hawataweza kusimamisha mipaka ya Mwenyezi Mungu (yaani hawataweza kuishi kwa wema). Basi mkiogopa kwamba hawataweza kusimamisha mipaka ya Mwenyezi Mungu, hapo itakuwa hapana dhambi kwao (mwanamume wala mwanamke katika) kupokea (au kutoa) ajikomboleacho mwanamke. Hii ndiyo mipaka ya Mwenyezi Mungu; basi msiiruke. Na watakaoiruka mipaka ya Mwenyezi Mungu, hao ndio madhalimu. (2:229).



Ilivyo katika sheria ni kwamba kabla mwanamke hajafikia kuomba talaka, atamshitaki mumewe katika mahakama ya Kiislamu au kwa Kadhi, endapo atakuwa anamtesa au kumdhulumu haki zake. Mwanamume atashauriwa kutekeleza wajibu wake kwa mkewe. Mwanamume akizidi kukengeuka, itabidi mke adai talaka mbele ya mahakama, kama mume amekataa kutoa talaka kwa hiari yake. Kwa hali hii, kwa kuwa mwanamke ndiye aliyekosewa, hatalazimika kurudisha mahari au chochote alichopewa na mumewe. Na mwanamume naye hatalazimika kumpa kitoka nyumba.



Wanawake wanaodai talaka kwa sababu zao binafsi zisizo za msingi, kwa sababu tu eti wanataka kubadilisha mazingira, wajue kuwa mchezo huo ni mbaya sana mbele ya Mwenyezi Mungu (s.w) kama tunavyojifunza katika Hadith: Shaaban(r.a)ameeleza kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu amesema: Mwanamke yeyote atakaye dai talaka kwa mumewe bila kosa, hata harufu ya Pepo imeharamishwa kwake. (Ahmad, Tirmidh).



(f) Talaka ya Mubarat
Talaka hii inapatikana kwa makubaliano ya mume na mke kuachana kwa wema baada ya kuona kuwa hakuna maelewano katika ndoa.




                   




Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2018-08-01     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 692


Download our Apps
👉1 Kitabu cha Afya     👉2 kitabu cha Simulizi     👉3 Madrasa kiganjani     👉4 Kitau cha Fiqh    

Post zifazofanana:-

UHAKIKI WA HADITHI
Uhakiki wa Hadith za Mtume (s. Soma Zaidi...

Shukurani za Nabii Ibrahiim(a.s) kwa Allah(s.w)
Kwa neema hii ya kuruzukiwa watoto wawili - Ismail na Is- haqa(a. Soma Zaidi...

Kumuosha maiti hatua kwa hatua nguzo zake, na suna zake
Soma Zaidi...

KAMA HUNA HAYA BASI FAJA UNACHOTAKA
' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ': ' ' ' ' ' '?... Soma Zaidi...

Mkataba wa 'Aqabah na vipiengele vyake na mafunzo tunayoyapata katika mkataba wa aqaba
Mtume (s. Soma Zaidi...

swala za tahiyatu al masjid, qabliya na baadiya
Muislamu anapoingia Msikitini kabla hajakaa anatakiwa aswali rakaa mbili za maamkizi ya msikiti, Tahiyyatul-Masjid. Soma Zaidi...

Twahara na namna ya kujitwaharisha, nguzo zake na sunna zake
Soma Zaidi...

quran na sayansi
Soma Zaidi...

Matukio mbalimbali katika historia ya uislamu kabla na baada ya Mtume (s.a.w) na makhalifa wake wanne
1. Soma Zaidi...

NYAKATI AMBAZO DUA HUJIBIWA
NYAKATI AMBAZO DUA HUJUBIWA. Soma Zaidi...

SHUGHULI ZA KILA SIKU
Pata elimu juu ya afya hapa ukiwa na vitabu vyetu bila ya malipo yoyote Soma Zaidi...

DUA 51 - 60
51. Soma Zaidi...