haki ya kutaliki: kuacha na kuachwa katika ndoa ya kiislamu
Haki ya KutalikiKatika jamii nyingi za kjahili haki ya kutoa talaka iko kwa mwanamume tu na mwanamke hana haki yoyote ya kumtaliki mumee.
Haki ya Kutaliki
Katika jamii nyingi za kjahili haki ya kutoa talaka iko kwa mwanamume tu na mwanamke hana haki yoyote ya kumtaliki mumee. Kalika sheria ya Klislamu haki ya kutoa talaka iko kwa wote, mume na mke.
(a)Haki ya Mume kutoa talaka
Ilivyo katika kawaida ya maumbile mwanamume ndiye anayeanza kutoa posa au pendekezo Ia kuoana. Katika sheria ya Kiislamu, mwanamume pia ndiye anayepaswa kutoa mahari kumpa anayemtaka waoane, ndiye mwenye jukumu Ia kumlisha mkewe na kukidhi haja zake zote, na ndiye kiongozi wa familia. Kwa kuzingatia ukweli huu. Uislamu umempa haki ya kutoa talaka lakini iwe inapokuwa hapana budi na iwe ni kwa wema na kwa kutekeleza masharti yaliyowekwa na sheria.
(b)Haki ya mke kumwacha mumewe
Ndoa katika Qur-an imeelezwa kuwa lengo lake ni kuleta upendo na huruma kati ya mume na mke - (Rejea Qur-an, 30:21). Endapo mwanamke ataona sababu za msingi ambazo, zinaifanya ndoa yao isifikie lengo hili, mwanamke anapewa uhuru wa kudai talaka kwa mumewe. Mumewe akimkatalia, anaruhusiwa mwanamke kwenda mbele ya vyombo vya Sheria ya Kiislamu na kudai talaka. Itabidi mume alazimishwe kutoa talaka iwapo vyombo hivi vya sheria vitashindwa kuwasuluhisha. Wakati mwingine, mwanamke anaweza kumtaliki mumewe bila hata ya kukubaliana naye au kupitia mahakamani. Inawezekana hivi kwa namna mbili:
(i)Kama tangu mwanzo, katika kufunga mkataba wa ndoa mume alikubaliana na mkewe kuwa atakuwa na uhuru wa kuvunja ndoa, endapo mume atamfanyia au atafanya jambo fulani asilolipenda; basi atakapovunja ahadi hiyo, mkewe atakuwa na uhuru wa kumwacha bila ya kudai talaka kwake au mahakamani. Kwa maana nyingine mwanamume tangu mwanzo katika mkataba wao wa ndoa, amempa mkewe haki ya kumtalakisha, endapo atafanya au atamfanyia jambo fulani asilolipenda. Talaka ya ama hii huitwa "Khul".
(ii)Kama katika mkataba wa ndoa, mwanamume alitoa haki yake ya "kutamka" talaka na kumpa mkewe ili kumpa uhuru na uwezo zaidi wa kuvunja mkataba wa ndoa endapo ataona haifikii lengo lake.
(c)Kuvunja ndoa kwa makubaliano ya mume na mke:
Wakati mwingine, mume na mke wote baada ya kuona kuwa hawaishi kwa maelewano kama ilivyotarajiwa, wana uhuru wa kukubaliana kuachana kwa wema. Mahakama ya Kiislamu haitaingilia kati, labda itokee kuvunjwa kwa sheria nyingine kutokana na kuachana kwao huko. Ama hii ya Talaka huitwa "Mubarat".
(d)Haki ya Mahakama ya Kiislamu katika kuvunja Ndoa
Wakati mwingine, hata bila ya makubaliano ya mume na mke, mahakama ya Kiislamu ma uwezo wa kuvunja ndoa. Kwa mfano talaka ya ama ya "Li'aan" husimamiwa na serikali.
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
๐1 Bongolite - Game zone - Play free game ๐2 Kitabu cha Afya ๐3 Dua za Mitume na Manabii ๐4 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w) ๐5 web hosting ๐6 Madrasa kiganjani
Post zinazofanana:
Nafasi ya serikali katika ugawaji
Serikali ina nafasi katika kufanya mgawanyiko katika uchumi.
Soma Zaidi...Aina za Najisi na twahara katika uislamu
Post hii inakwenda kukufundisha aina za najis. Pia utajifunza aina za twahara katika uislamu
Soma Zaidi...Maana ya swala
Maana ya Swala Maana ya Swala kilugha(a) Kilugha Katika lugha ya Kiarabu neno ยSwalaatย lina maana ya ยombi au ยdua.
Soma Zaidi...MAANA YA ZAKA NA SADAKA KULUNGA NA KISHERIA PAMOJA NA TOFAUTI ZAO
MAANA YA ZAKA NA SADAKA KULUNGA NA KISHERIA PAMOJA NA TOFAUTI ZAO.
Soma Zaidi...