Haki na wajibu kwa mayatima

Haki na wajibu kwa mayatima

Wajibu kwa Mayatima



Yatima ni mtoto aliyefiwa na wazazi wake, hasa baba, kabla ya kufikia baleghe. Uislamu unatuhimiza kuwatendea wema yatima na kuwatunzia urithi wao kwa uadilifu mpaka wafikie baleghe yao na kuwa na akili ya kutunza mali.


"... Na wanakuulizajuu ya mayatima: Sema: Kuwatendea mema ndivyo vizuri. Na kama mkichanganyika nao (ndivyo vyema vile vile) ,kwani ni ndugu zenu..." (2:220)
Tunajifunza kutokana na aya hii kuwa tunatakiwa tuwatendee wema mayatima na tuishi nao katika familia kama tunavyoishi na watoto wetu. Kukaa nao pamoja kwa huruma na mapenzi kutawafariji na kuziba pengo Ia kufiwa na mzazi au wazazi wao. Si katika mwenendo wa Kiislamu kuwatenga mayatima kwenye makazi maalumu. Tuishi nao katika familia zetu na tuwasomeshe katika shule wanazosoma watoto wetu.



Kuwanyanyasa mayatima ni katika madhambi makubwa mbele ya Allah (s.w). Si muumini wa kweli yule anayemnyanyasa yatima kama tunavyojifunza katika Qur-an:


".Je, umemuona yule anayekadhibisha dini (asiyeamini malipo ya akhera)? Huyo ni yule anayemsukuma (anayemnyanyasa) yatima." (107:1-2)



Msisitizo wa kuwatendea wema mayatima pia tunaupata katika hadith zifuatazo:
Abu Hurairah (r.a) amesimulia kuwa Mtume wa Allah amesema: "Kaya (familia) bora kuliko zote ni ile ambamo anatendewa wema yatima; na kaya mbovu kuliko zote ni ile ambamo ananyanyaswa yatima." (Ibn Majah)



Sahl bin Sa 'ad (r.a) ameeleza kuwa Mtume wa Allah amesema: 'Mimi na yule anayemlea yatima (kwa wema), akiwa wa kwake au kwa wengine, tutakuwa naye peponi kama hivi - akionyesha kidole cha mwanzo (cha shahada) na kinachofuatia (cha kati) huku vikiwa vimeshikamana bila ya kuachana mwanya wowote ". (Bukhari)
Kuwatendea wema mayatima ni pamoja na kuwatunzia mali zao za urithi kwa uadilifu kama inavyosisitizwa katika Qur-an:


"Na wapeni mayatima mali zao. Wala msibadilishe kibaya kwa kizuri. Wala msile mali zao pamoja na mali zenu. Hakika (yote) hayo nijukumu kubwa." (4:2)



Na wajaribuni mayatima (wanapokuwa karibu ya kubaleghe kama wataweza kutumia fedha zao vizuri wakati watakapobaleghe. Wajaribuni kidogo kidogo) mpaka wafike wakati wa kuoa (kubaleghe). Kama mkiwaona wana akili njema, wapeni mali zao. Wala msizile kwa fujo na kwa haraka ya kwamba watakua (wazitake; hebu tuzile upesi). Na mwenye kuwa tajiri basi ajiepushe (na kuchukua ujira katika kuwafanyia kazi zao). Na atakayekuwa mhitaji basi ale kwa namna inayokubaliwa na Sharia. Na mtakapowapa mali zao, basi wawekeeni mashahidi (/uu ya kuwa Mwenyezi Mungu anatosha kuwa shahidi. (4:6)


Hakika wale ambao wanakula mali ya mayatima kwa dhuluma, bila shaka wanakula moto matumboni mwao; na wataungua katika huo Moto (wa Jahannam) uwakao. (4:10)
Kutokana na aya hizi tunahimizwa kutunza mali za mayatima mpaka watakapofikia umri stahiki ndio tuwakabidhi. Kama tuna uwezo tusitumie chochote kutokana na mali hiyo katika kuwalea. Kama hatuna uwezo tunaruhusiwa tuitumie katika kuwapa mahitaji ya lazima kama vile Elimu, mavazi, n.k; lakini vile vile kwa tahadhari na ungalifu.




                   


Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2018-08-01     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 115

Post zifazofanana:-

KULINDA AKAUNT YAKO YA FACEBOOK DHIDI YA WAHALIFU WA KIMTANDAO
Watu wengi wanalalamika kuwa akaunti zao za facebook zimehakiwa, yaani zimeshambuliwa na wahalifu wa kimtandano. Soma Zaidi...

Mafunzo ya Sura Zilizochaguliwa
Soma Zaidi...

Fahamu virutubisho vya wanga na kazi zake, vyakula vya wanga na athari za upungufu wake
Hapa tutaona kuhusu virutubisho vya wanga, kazi zake na athari za upungufu wake Soma Zaidi...

NAMNA YA KUGUNDUA VIDONDA VYA TUMBO
NAMNA YA KUGUNDUA VIDONDA VYA TUMBO Ili kugundua vidonda, daktari wako anaweza kwanza kuchukua historia ya matibabu na kufanya uchunguzi wa mwili. Soma Zaidi...

HADITHI YA NURDINI 02: mawaziri wa Mfalme
Alikuwepo mfalme aliyetambulika kwa jina la Muhammad Suleiman Azeyn. Soma Zaidi...

UTAMBUE UGNJWA WA UTI DALILI ZAKE, CHANZO NA TAHADHARI DHIDI YAKE
Pata elimu juu ya afya hapa ukiwa na vitabu vyetu bila ya malipo yoyote Soma Zaidi...

Swala ya ijumaa, nguzo zake na suna zae, namna ya kuswali swala ya ijumaa
Soma Zaidi...

Fangasi wa kwenye kucha: dalili zake, na kumbambana nao
Hawa ni fangasi ambao wanashambulia sana kwenye kucha za vidole vya mikonobna miguu. Soma Zaidi...

Kuporomoka kwa Dola ya Kiislamu
Soma Zaidi...

THE DIFFERENCE BETWEEN BIOLOGY LABORATORY AND OTHER SCHOOL FACILITIES
THE DIFFERENCE BETWEEN BIOLOGY LABORATORY AND OTHER SCHOOL FACILITIES School facilities these are materials designed to serve specific purposes in the school system, which facilitate teaching and learning. Soma Zaidi...

KUAMINI MALAIKA
Jifunze tawhid yaani kumpwekesha Allah subhaanah wata'aala Soma Zaidi...

TYPES OF FOOD
THIS IS WHAT YOU NEED TO KNOW ABOUT FOOD. Soma Zaidi...