(d) Ulaya Wakati wa Mapinduzi ya ViwandaKatika karne ya 18, wanafalsafa na waandishi wa Ulaya walipaza sauti zao dhidi ya jamii iliyojengwa katika misingi ya Ukristo iliyochanganyika na ukabaila (feudalism), ambayo ilikuwa ikiwanyonya na kuwanyanyasa wanyonge. Ni katika wakati huo palitokea mapinduzi ya viwanda yaliyoipa Ulaya na Marekani sura mpya ya maendeleo ya kiuchumi na kijamii.Hatua za mwanzo zilizochukuliwa na jamii hii ya mapinduzi ni pamoja na kumkomboa mwanamke na kuinua hadhi yake kutoka kwenye hali ya kudunishwa na kumfikisha kwenye hali ya kuwa na heshima na haki sawa na wanamume katika jamii. Sheria za Ndoa na talaka zilirekebishwa. Haki ya kuchuma na kumiliki mali ilirejeshwa kwa mwanamke. Itikadi zote za kidini na mila zilizomdhalilisha mwanamke zilirakebishwa. Wanawake walipata fursa sawa na wanaume katika elimu na mafunzo ya juu. Marekebisho haya yaliamsha an na vipawa vya mwanake vilivyo kandamizwa hapo awali. Wanawake walizipamba nyumba na kuichangamsha jamii kwa kujiingiza katika shughuli mbali mbali za ustawi wa jamii. Matunda yaliyopatikana kutokana na kumpa mwanamke heshima yake na haki zake nyingine za msingi kupatikana kwa malezi na afya bora kwa jamii na ukuaji wa sayansi kimu ( Domestic Science).Pamoja na matunda haya, kwa upande mwingine, jamii ya Ulaya iliporomoka sana kimaadili kutokana na mtazamo wake juu ya demokrasia kati ya wanaume na wanawake. Katika kumtetea mwanake Ulaya Magharibi ilizingatia vipengele vifuatavyo:Usawa kati ya Mume na Mke bila kujali maumbile yao ya kijinsia. Kujitegemea kiuchumi kwa mwanamke. Uhuru wa kuchanganyika wanaume na wanawake. Je, jamii ya Ulaya iliyoundwa juu ya misingi hii ya demokrasia kati ya mwanamume na mwanamke, ilistawi na kumbakisha mwanamke katika hadhi yake? Hebu tuangalie matokeo ya utekelezaji wa Demokrasia hii:Kwanza, Uoni juu ya usawa kati ya mwanamke na mwanmume haukuishia kwenye kupata heshima na haki sawa kati yao, bali ilichukuliwa kuwa hata kimaumbile wako sawa. Hivyo mwanamke naye alidai kufanya shughuli zile zile anazofanya mwanamume. Wanawake walidai kuwa wawe huru katika kuchunga miiko ya maadili. Wawe huru kuvaa na kujistarehesha kama wanaume. Mtizamo huu wa usawa ulimfanya mwanamke aidharau nafasi yake kama miezi wa familia na badala yake akajiweka katika mashindano na wanaume katika uchumi, siasa na harakait nyinginezo za kijamii. Alijiingiza katika kampeni za kugombea uongozi wa kisiasa, alikimbilia kazi za Ofisini na viwandani, alishindana na wanaume katika biashara na viwanda, katika michezo na mazoezi ya kimwili, katika kuendesha vilabu vya michezo na upigaji wa muziki. Katika hali hii, kuwalea watoto na kuiweka familia katika utulivu, upendo na ushirikiano, ilikatika kuwa jukumu lake Ia asili. Kwa mtazamo huu wa usawa, maisha ya ndoa yalidharaulika na uzinifu katika jamii ukawa ni jambo Ia kawaida na kuigharimu jamii kiasi kikubwa (zingatia madhara ya uzinifu katika jamii) na kuzidi kumdunisha mwanamke.Pili, Kujitegemea kiuchumi kwa mwanamke kumemdanya asiwe na haja yak kuwajibika kwa mumewe na kuvunja utartibu wa asili wa "Man for the field and Woman for the hearth" yaani "Mwanamume ni wa shambani na mwanamke ni wa nyumbani". Katika mtazamo huu wa maendeleo ya Ulaya, mwanamume na mwanamke wote wana jukumu sawa Ia kuchuma na malezi ya familia yakakabidhiwa watumishi wa nyumbani (House girls/House boys), taasisi nyingine kama vile vituo vya watoto, shule n.k. Katika hali hii ya mwanamke kujitegemea kiuchumi, hapakuwa na kiungo chochote cha kumuunganisha mwanamume na mwanamke ila haja tu ya kutosheleza matamanio ya ngono.


Sasa, kama mwanamke anajitegemea mwenyewe kwa chakula, mavazi, makazi, na kwa mahitajio yake yote mengine, kwa nini abakie kuwa mwaminifu kwa mume mmoja ambaye hamuhitajii kwa lolote ila kwa jimai tu? Kwa nini ajiingize katika maisha ya ndoa ambayo yamefungamana na kanuni za kimaadili na sheria? Kama, kwa mtazamo wa usawa tuliouona, umeshamuondolea vizingiti na kumpa uhuru kamili wa kuzini kwa nini asifuate njia hii nyepesi na ya haraka ya kutosheleza matamanio yake ya kimwili na badala yake achague njia ndefu ambayo si tu kuwa imeambatana na majukumu bali pia inataka kujitoa muhanga? Kwa hali hii umalaya katika jamii ulikuzwa na kutetewa kama haki nyingine zilivyotetewa. Mwanzoni walipatikana watoto wengi waliozaliwa nje ya ndoa, lakini sasa idadi hii imepunguzwa baada ya kubuniwa njia mbali mbali za kuzuia (kudhibiti) kizazi. Pia iii kujiepusha na kupata watoto, wanaume kwa wanawake walifikia kiwango cha kufanya jimai na mbwa. Hiki ndicho chanzo kikubwa cha magonjwa ya ya zinaa - kaswende, kisonono, AIDS n.k. Hata hivyo, hapakuwa na ubaya wowote katika jamii hii mwanamke kupata mtoto nje ya ndoa.Mamia kwa maelfu ya vijana wanawake katika nchi za Ulaya na Marekani wanapendelea kuishi maisha ya kutoolewa na wamefanya umalaya kuwa mtindo wa maisha. Wale wachache wanaoolewa, kwa kuwa kuna huo uhuru wa kujitegemea kiuchumi na kutomtegemea kabisa mume kwa mahitaji yoyote yale, ila kwa jimai tu, ndoa nyingi huwa ni zenye kuyumba. Panakosekana kiungo madhubuti cha unyumba wao. Mume na mke ambao kila mmoja anajitegemeakiuchumi, hujikuta hawana kitu madhubuti cha kuwaunganisha na kuwafanya wakubaliane na kuvumiliana katika mambo mbali mbali ya kiunyumba. Upendo wa kishabiki unaopatikana katika ule muda mfupi wa jimai hautoshi kuwafanya hawa wawili waishi maisha ya kuvumiliana. Kutoelewana katika jambo dogo tu hivi huwa ni sababu tosha ya kuvunja ndoa.Tatu,Uhuru wa kuchanganyika wanaume na wanawake umechangia sehemu kubwa ya kukuza umalaya katika nchi za Ulaya. Matamanio ya ngono hupata nguvu sana wanawake na wanaume wanapochanganyika pasi na mipaka. Katika kuukuza umalaya, na Marekani wanawake katika nchi nyingi za Ulaya na Marekani hujitahidi sana kujipodoa kwa vipodozi vya ama mbali mbali, kuvaa mavazi mafupi,yanayobana yanayoonyesha mwili(transparent). Wakati mwingine hutembea uchi wa nyama. Picha za wanawake walio uchi katika vitabu vya mapenzi, magazeti, sinema, n.k. ni vitu vya kawaida katika nchi nyingi za Ulaya na Marekani. Mazingira haya yamechochea wanaume kupatwa na kiu isiyokatika ya kutaka kutosheleza matamanio ya ngono. Kutokana na mazingira haya vijana wadogo huingizwa katika uzinzi hata kabla ya kufikia baleghe. Mabinti wadogo kuwa na marafiki wa kiumbe (boy friends) ni jambo Ia kawaida linaloshangiliwa na wazazi. Hii ndio jamii inayohesabika kuwa imeendelea katika kutetea haki na heshima ya mwanamke.