Haki za kiuchumi za mwanamke katika uislamu

Haki za UchumiKuwa imara kiuchumi ni sababu mojawapo kubwa ya kumpa mtu hadhi katika jamii.

Haki za kiuchumi za mwanamke katika uislamu

Haki za Uchumi
Kuwa imara kiuchumi ni sababu mojawapo kubwa ya kumpa mtu hadhi katika jamii. Kama tulivyoona jamii nyingi za kale, zilimnyima mwanamke haki ya kiuchumi na kumfanya kama mtumwa katika jamii. Wanawake walifanya kazi sana lakini hawakuwa na haki ya kumiliki kile walichokichuma, chochote walichokuwa nacho kilikuwa ni mali ya waume zao, hawakuwa na haki ya urithi bali wenyewe walirithi wa mume zao walipofariki. Kama tulivyoona wakati wa maendeleo ya viwanda,. nchi za Ulaya zilichukua jukumu Ia kumkomboa mwanamke kwa kumuingiza kazini ili naye ainuke kiuchumi. Ukombozi huu wa kumfanya mwanamke afanye kazi viwandani sawa na wanaume haukuwa ukombozi kitu kwani yalizuka matatizo mengine yaliyozidi kumdunisha mwanamke na kuidhoofisha jamii kimaadili.



Ni Uislamu pekee umemuinua mwanamke kiuchumi na maadili. Katika Sheria ya Kiislamu, mwanamke anayo haki ya kupata mahitaji yake yote ya maisha- chakula, nguo, makazi, n.k. kutoka kwa mumewe. Ni haki yake kupewa mahari na mumewe kabla ya kuolewa na ni haki yake pekee kumiliki mali hiyo inayotokana na mahari bila ya kuingiliwa na baba yake, mlezi wake, mum ewe au yeyote yule. Vile vile


mwanamke amepewa na sheria ya Kiislamu haki ya kuwarithi wazazi wake, mume wake, watoto wake na jamaa zake wengine wa karibu. Pia mwanamke amepewa uhuru kamili wa kuchuma na kumiliki alichokichuma. Ana uhuru kamili wa kuwa na hisa katika biashara au kampuni kwa jina lake mwenyewe.



Pamoja na uhuru huu aliopewa mwanamke wa kuchuma na kumiliki mwenyewe alichokichuma kwa mikono yake alimuradi tu anazingatia mipaka ya Allah (s.w) bado mumewe anawajibika kukidhi mahitajio yake yote muhimu ya maisha kama vile chakula, rnavazi makazi. Kwa hiyo hali ya kiuchurni kwa mwanamke imehif8dhiwa na Sheria ya Kiislamu kwa. kiasi kwamba mwanamke mara nyingi anakuwa tajiri kuliko mumewe.


Hata hivyo mwanamke anao uhuru kamili wa kumfanyia mumewe ihsani kwa kummegea kile alichokichuma au kumpunguzia majukumu kwa kujitosheleza yeye mwenyewe kwa mahitaji yake muhimu. Na wanaume nao wakifanyiwa ihasani na wake zao wapokee kwa furaha kama tunavyojifunza katika Qur'an: (Wake zenu) wakikupeni kwa radhi ya nafsi zao kitu katika hayo (mali yao) basi kuleni kwafuraha na kunufaika (4:4).



Ieleweke kuwa situ wanawake wanaruhusiwa kuchuma kwa kujiajiri tu wenyewe bali pia wanaweza kuajiriwa katika kazi yoyote ile inayoheshimu hadhi yake na kuchunga mipaka aliyoiweka Allah (s.w). Bali katika jamii ya Kiislamu baadhi ya wanawake wanalazimika waajiriwe kufanya kazi mahsusi. Kwa mfano katika Sheria ya Kiislamu ni . vizuri mgonjwa wa kike kuchunguza matatizo yake ya sin na daktari mwanamke. Vile vile mgonjwa mwanamke ni vyema auguzwe na muuguzi (Nurse) mwanamke. Ni vizuri zaidi pia watoto au wanafunzi wa kike kufundishwa na waalimu wa kike. Hii ma maana kuwa linahitajika kundi kubwa Ia wanawake watakao fanya kazi hizi. Kwa mujibu wa Sheria ya Kiislamu wan awake pia wanayo haki ya kupata malipo sawa na wanaume kulingana na sifa.


Pamoja na mwanamke kupewa uhuru wa kushiriki katika harakati za uchumi, ikumbukwe kuwa jukumu kubwa na muhimu kwa mwanamke ni kuilea familia kiafya na kimaadili. Kuna baadhi ya watu ambao wanadai kuwa katika jamii ya leo maendeleo yatapatikana tu iwapo wanaume na wanawake watafanya kazi za kuajiriwa. Kwa hoja hii inadaiwa kuwa kuwataka wanawake kushughulikia malezi ya watoto wao ni kurudisha nyuma maendeleo ya kijamii. Madai haya hayana msingi. Kwanza hatulijui ni jukumu gani kubwa na bora zaidi kuliko lile Ia mama kuwa miezi wa watoto wake. Swali Ia kujiuliza hapa ni je, tunayatafsiri vipi maendeleo ya jamii? Je, tunayatafsiri maendeleo kwa kiasi cha Dola ($) na Shilingi kilichomo nchini? Au tunazungumzia pia maendeleo ya kiroho na kimaadili? Ni dhahiri kuwa kama tutapanua upeo wetu wa tafsiri ya maendeleo tutaona kuwa jamii itanufaika sana siyo tu kwa kuwa na barabara zenye lami na mabasi mengi bali pia iwapo raia katika jamii hiyo watakuwa wamelelewa katika kuthamini uadilifu kuliko hata mali. Vinginevyo mabasi hayo yatakuwa kama majeneza yanayoelekea kwenye maangamizi kutokana na kuvamiwa na majambazi waporaji ambao hawasiti kuwaua binaadamu wenzao kama kuku. Tukipanua upeo wetu tutaona kuwa malezi bora ya watoto yatolewayo kwa mapenzi na huruma na mama ni hazina kubwa kwa jamii yoyote ile.



Na kwa nini hasa mwanamke akifanya kazi nje ya nyumba yake anahesabiwa anafanya kazi lakini akifanya kazi nyumbani mwake tangu alfajiri hadi usiku anahesabiwa hafanyi kazi? Tunaitafsiri vipi kazi? Je, kipimo ni kule kutoka nje ya nyumba au kufanya mbali na nyumbani? Na kwa nini katika jamii zetu za leo tunamhesabu mwanamke anayepika chakula hotelini kuwa anafaya kazi lakini akiwapikia awapendao nyumbani mwake anahesabiwa hafanyi kazi? Kwa nini mwanamke akishona nguo au kufuma sweta katika kiwanda anahesabiwa anafanya kazi lakini akiwashonea wanawe nyumbani anahesabiwa anakaa bure hafanyi kazi? Kwa nini akilea watoto wa mwenzake katika vituo vya watoto anahesabiwa yuko kazini lakini akiwalea watoto wake hafanyi kazi? Kwa nini mwanamke akiwa Sekretari anayepanga na kuratibu kazi za bosi wake anahesabiwa kuwa anafanya kazi lakini akipanga na kuratibu shughuli nyumbani mwake anahesabiwa kuwa hafanyi kazi?



Tatizo linalozikabili jamii nyingi hivi leo ni kudhani kuwa kuolewa na kulea watoto ni mambo ya kizamani, na kwa kuwa ni yakizamani basi ni mabaya na hayana faida yoyote. Lakini ukweli unabakia kuwa lau mume angalijaribu kuitathmini kazi anayoifanya mkewe katika mizani ya pesa na halafu akaamua kumlipa basi angalifilisika mara moja hata angalikuwa tajiri vipi. Mama kwa mfano, anaweza kujikuta halali usiku kucha kwa sababu ya kumuuguza mwanawe kwa huruma na mapenzi bila ya kusimamiwa na mtu na bila kutaraji malipo kwa mtu. Kazi hiyo yastahiki malipo kiasi gani?



Matokeo ya kupuuzia jukumu hili Ia mama kuwalea watoto wao wenyewe, ni kuwa baada ya mud a fulani jamii itajikuta inakabiliana na wimbi kubwa sana Ia wizi, ujambazi, uporaji na hata uuaji kama matunda ya kutowalea watoto ipasavyo au kwa kuwakabidhi watu amabo hawajali wala hawana habari juu ya makuzi ya kiroho na kimaadili ya mtoto.




                   




Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2018-08-01     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 149


Download our Apps
👉1 Kitabu cha Afya     👉2 Kitau cha Fiqh     👉3 kitabu cha Simulizi     👉4 Madrasa kiganjani    

Post zifazofanana:-

KUMUAMINI MWENYEZI MUNGU
Jifunze tawhid yaani kumpwekesha Allah subhaanah wata'aala Soma Zaidi...

Kuamini qadar na qudra katika uislamu
Kuamini Qadar ya Allah (s. Soma Zaidi...

Mafunzo Yatokanayo na Historia ya Nabii Ismail(a.s)
Kutokana na Historia ya Nabii Ismail(a. Soma Zaidi...

Dua sehemu 03
Zijuwe njia ambazo Allah hujibu Dua yako. Tambua kama umejibiwa dua yako au bodo, soma darsa za dua hapa. Soma Zaidi...

Hukumu ya Mtu asiyefunga kwa makusudi mwezi wa ramadhani
Soma Zaidi...

Maana ya Funga ya ramadhani kisheria na Aina za funga
Amesema mtume (s.a.w) kuwa Allah (s.w) amesema: kila amali ya mwanaadamu ni kwa ajili yake isipokuwa funga. Soma Zaidi...

Mtume hakufundishwa quran na Jabir na Yasir
Soma Zaidi...

Vituo vya kunuia ibada ya hija
Soma Zaidi...

Mambo gani ni Haramu kwa mwenye janaba?
Hadathi ya kati na kati (Janaba). Soma Zaidi...

Yunus(a.s) Kulingania Uislamu kwa Watu Wake
Nabii Yunus(a. Soma Zaidi...

sura ya 02
Jifunze namna ya kusoma quran, pata mafunzo ya tajwid hapa Soma Zaidi...

TANZU ZA HADITHI
Tanzu za Hadith(1) Tanzu ya UsahihiKulingana na kiwango cha usahihi wa Hadith, Hadith zimegawanywa katika makundi makuu manne:(a) Sahihi'(b) Hasan/Nzuri. Soma Zaidi...