Haki za mwanamke katika Uislamu
Katika kuhakikisha kuwa mwanamke anapata haki zake Uislam umesisitiza mambo ya msingi yafuatayo:
Kwanza, Uislamu umeweka wazi kuwa uongozi aliopewa mwanamume juu ya familia yake asije akautumia vibaya na akawageuza watu wa familia yake kuwa "Watumwa" naye akawa "Bwana". Bali anatarajiwa kuiongoza familia na kufikia lengo tarajiwa.
Pili, Uislamu umesisitiza kuwa wanawake wapewe fursa zote zitakazo wawezesha kuendeleza vipawa vyao katika kiwango cha juu ili kuinua na kuiendeleza jamii, ila tu mipaka ya Uislamu ichungwe.
Tatu, Uislamu unasisitiza kumuendeleza mwanamke kiwango cha hali ya juu na kumbakisha katika hadhi ya mwanamke. Kuwa mwanamume au kumtayarisha kwa majukumu ya wanaume si katika haki zake wala Si jambo litakalo mletea maendeleo yeye binafsi na jamii nzima kwa ujumla.
Kwa kuzingatia vipengele hivi vya msingi Uislamu unampa mwanamke haki katika nyanja zote za kijamii kama ifuatavyo: