Faida za tangawizi

Faida za tangawizi

Somo Hili linakwenda kukuletea faida za tangawizi

FAIDA ZA TANGAIZI

Tangaizi ni katika mimea yenye asili na bara la asia hususan nchi ya China. Mmea huu hutambulika kwa faida zake za kitiba toka zamani sana. Na karibia dunia nzima hutumia tangaizi kama tiba na kama kinywaji. Ndani ya tangaizi kuna chembechembe ziitwazo gingerol, hizi ndizo huipa tangaizi uwezo wake wa kitiba.

 

Unaweza kutumia tangaizi kwa kutafuna vipande vidogovidogo au kwa kutia kwenye  mboga. Pia unaweza kuweka kwenye chai ikiwa vipande vidogo au ikiwa imekauchwa na kusagwa kama ungaunga. Zipo njia nyingi za kutumia tangaizi. Zifuatazo ni katika baadhi ya faida za tangaizi iafya:-

 

1. Tangaizi ni mujarabu sana katika kutibu kichefuchefu. Hususani kichefuchefu cha mimba. Kwa ujumla kichefuchefu huwapata sana wajawazito, na watu walofanyiwa upasuaji wa ndani. Lakini kinaweza kumpata mtu yeyote. Unaweza kutumia tangaizi kwenye chai, ama kutafuna vipande vidogo. Hakikisha unakula japo gram moja.

2. Hupunguza maumivu ya misuli

3. Hupunguza maumivu ya viungo

4. Husaidia katika kushusha kiwango cha sukari. Hususan kwa wenye kisukari type 2. kwa kufanya hivi pia hupunguza athari ya kupata maradhi ya moyo

5. Husaidia kwa wenye tatizo la kutokupata choo na kukosa hamu ya kula.

6. Hupunguza maumivu ya tumbo la chango kwa wanawake.

7. Hupunguza hatari ya kupata ugonjwa wa saratani (cancer)

8. Huimarisha afya ya ubongo

9. Husaidia katika kuimarisha mfumo wa kinga za mwili.

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

       
Author: Rajabu Rajabu
Tarehe: 2024-05-10 14:53:23 Topic: Vyakula Main: Post File: Download PDF Views: 4062

Share On:

Share follows: 0 | Unique share links followed: 0
Sponsored links
👉1 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)     👉2 web hosting     👉3 Bongolite - Game zone - Play free game     👉4 Kitabu cha Afya     👉5 Simulizi za Hadithi Audio     👉6 Tafasiri ya Riyadh Swalihina    

Post zinazofanana:

Vyakula vya kupunguza presha ya kupanda

Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu vyakula ambavyo vinaweza kupunguza presha ya kupanda

Soma Zaidi...
Kazi za tunda la papai katika kurekebisha homoni imbalance

Posti hii inahusu zaidi kazi za tunda la mpapai katika kurekebisha homoni.ni tunda ambalo ufanya kazi yake kwa sababu ya kuwepo kwa virutubisho muhimu ndani ya tunda hili.

Soma Zaidi...
Vyakula vya kuongeza nguvu za kiume.

Tatizo la nguvu za kiume linawwza kuzuiliwa ama kupunguzwa kwa kutumia muunganimo wa njiankadhaa kama kubaduki vyakula, kutumia dawa, kupata ushauri kwa wataalamu wa afya ya mahusiano ama kufanya nazoezi. Je na wewe unasumbuliwa na tatizo hili? Makala hii

Soma Zaidi...
Faida za kiafya za kula fenesi

Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kula fenesi

Soma Zaidi...