Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu vyakula vya minyoo
NI NINI CHAKULA CHA MINYOO?
Kama tulivyokwisha kuona aina za minyoo, bila shaka umetambua kidogo kuhusu nini wanakifanya wakiwa mwilini. Hivyo basi katika sehemu hii nitakwenda kukueleza chakula cha minyoo ndani ya mwili:-
Wanakula chakula tunachokula, katika aina hizi za minyoo wapo minyoo wanaishi kwenye utumbo mdogo. Hii ndiyo sehemu ambayo chakula kinameng’enywa na kuupa mwili nishati na afya yaani kuupatia mwili virutubisho. Lakini minyoo hawa wakati mwingine wanakula chakula alichokula mtu hata kabla ya kumeng’enywa. Hali hii inaweza kusababishia mtu kukosa virutubisho na hatimaye kukonda ama kupoteza usito.
Wanakunywa damu, wapo minyoo wengine wanaishi kwenye mfumo wa damu ama ameneo mengine na kuanza kunyonya damu. Minyoo hawa ni hatari sana kwani wanaweza kusababisha ugonjwa wa anaemia. Ugonjwa huu husababishwa na upungufu wa damu.
Wanakula viungo vya mwili, katika minyoo hawa kwa mfano liverfluke hawa wanaishi kwenye ini ama maeneo ya nyongo. Minyoo hawa wanakula ini, na kulisababishia vidonda. Pia ini linaweza kuvimba hatimaye kuleta madhara makubwa.
Wanakula tishu nyingine, tofauti na hayo tuliyotaja minyoo hawa wanaweza kula tishu nyingine ndani ya mwili. Kama tulivyoona kuna baadhi ya minyoo wanakaa kwenye ngozi, viungio, ini na sehemu nyingine
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetuUmeionaje Makala hii.. ?
Hii ni orodha ya vyakula salama na vizuri kwa mgonjwa wa vidonda vya tumbo
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukuletea faida za kiafya za kula kabichi
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi faida za kitunguu swaumu wakati wa ujauzito, kuna kipindi ambacho wanawake wakati wa ujauzito uchaguza vyakula mbalimbali kuna ambao wanaweza kutumia vitunguu saumu na kupata faida kubwa
Soma Zaidi...Posti hii inaonyesha Faida za kula papai.papai Ni tunda na Lina leta afya,nguvu na kuujenga mwili.
Soma Zaidi...Somo hili litakwenda kukueleza na kukuelimisha kuhusu umuhimu wa kula parachichi kiafya
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kula mayai
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi mboga mboga za majani ambazo zinaweza kuweka sukari kwenye kiwango cha kawaida.
Soma Zaidi...Post huu inakwenda kukupa orodha ya madini muhimu kwa ajili ya afya yako.
Soma Zaidi...