Faida za vitamin C mwilini

Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za vitamini C mwilini

FAIDA ZA VITAMINI C MWILINI

 

Kama tulivyokwisha kuona vyakula vya vitamini C kama vile papai, machungwa, mananasi, maembe, malimao na ndimu. Pia tuliona baadhi ya kazi za vitamini C ambazo ni kusaidia katika kuuwa kemikali mbaya mwilini, kuipa nguvu miili yetu ya kupambana na maradhi. Katika makala hii nitakwenda kukujuza umuhimu wa vitamin C katuka mwili wa kila kiumbe akiwemo binadamu.

 

Faida na umuhimu wa vitamini C

1.Hulinda mwili dhidi ya maradhi ya kiseyeye (scurvy): Haya ni maradhi ambayo hufanya mwili uweze kutoa damu kwenye mafinzi, mwili kuchubuka kwa urahisi, kuchelewa kupona kwa majeraha. Kusoma zaidi kuhusu ugonjwa huu pitia zaidi makala zetu.

 

2.Kulinda mwili zidi ya maambukizi na mashambulizi:

Tafiti mbalimbali zilizofanya zinaonesha kuwa vitamini C inaweza kusaidia kupunguza nguvu za virusi waletao mafua na homa ya mafua. Baadhi ya tafiti zinadiriki kusema kuwa vitamini hivi kuponyesha mafua yaa kwa haraka, lakini ambalo halina shaka ni kuwa vitamini c vinaweza kupunguza kupata mafua ya mara kwa mara au kufanya mafua yaondoke kwa haraka.

 

3.Vitamini C ni muhimu sana katika mfumo wa kinga mwilini. Kwani vitamini C husaidia katika Antimicrobial yaani katika kuzuia vijidudu shambulizi mwilini kama bakteria na virusi, pia vitamini C husaidia katika Natural killer cell yaani katika kuuwa vijidudu shambulizi ama kuvizuia visiendelee kukua mwilini, pia vitamini C husaidia katika kuimarisha mfumo wa kinga kwa kuimarisha seli hai nyeupe ziitwazo lymphocyte hizi ndizo seli ambazo askari mkuu wa mwili dhidi ya vimelea vya maradhi kama virisi, fangasi, protozoa na bakteria.

 

4.Kulinda miili yetu dhidi ya saratani (cancer):

Tafiti mbalimbali zimefanywa kuhusu aina ya saratani na zinavyohusiana na vitamini C kama saratani ya matiti na mapafu. Ijapokuwa tafiti hizi hazikuweza kuthibitisha moja kwa moja kuwa vitamini C vinasaidia kuondoa saratani hizi kalaki kuna mambo ambayo tafiti hizi yametufungua mawazo:

A. Vitamini C husaidia kuborsha afya na kuishi vyema kwa wagonjwa wa saratani

B. Vitamini C inaweza kuuwa seli zinazotengeneza uvimbe wa saratani

 

5.Husaidia kulind miili yetu dhidi ya maradhi yanayohusu mishipa ya damu na moyo (cardiovascular)

 

6.Husaidia kulinda miili yetu dhidi ya maradhi ya ubongo na kusahasahau

Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 1970-01-01 03:33:44 Topic: Vyakula Main: Afya File: Download PDF Views 8022

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
👉1 Simulizi za Hadithi Audio    👉2 Bongolite - Game zone - Play free game    👉3 Madrasa kiganjani    👉4 Kitau cha Fiqh    👉5 Tafasiri ya Riyadh Swalihina    👉6 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)   

Post zinazofanana:

Faida za kula magimbi (taro roots)

Somo Hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kula magimbi

Soma Zaidi...
KITABU CHA MATUNDA

Jifunze sifa na aina za matunda, vijuwe viruturubisho

Soma Zaidi...
KITABU HA MATUNDA

Jifunze sifa na aina za matunda, vijuwe viruturubisho

Soma Zaidi...
Pilipili kali

Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za pilipili kali

Soma Zaidi...
Vijuwe vyakula vinavyoongeza damu kwa haraka

Post hii itakufundisha aina za vyakula ambavyo vinaweza kuongeza damu kwa haraka.

Soma Zaidi...
Faida za kiafya za kula pera

Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kula pera

Soma Zaidi...
Vyakula vya vitamin K

Some Hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za vyakula vya vitamin K

Soma Zaidi...