JITIBU KWA TANGAIZI: faida za kiafya za tangaizi
Tangaizi ni katika mimea yenye asili na bara la asia hususan nchi ya China.
FAIDA ZA TANGAIZI
Tangaizi ni katika mimea yenye asili na bara la asia hususan nchi ya China. Mmea huu hutambulika kwa faida zake za kitiba toka zamani sana. Na karibia dunia nzima hutumia tangaizi kama tiba na kama kinywaji. Ndani ya tangaizi kuna chembechembe ziitwazo gingerol, hizi ndizo huipa tangaizi uwezo wake wa kitiba.
Unaweza kutumia tangaizi kwa kutafuna vipande vidogovidogo au kwa kutia kwenye mboga. Pia unaweza kuweka kwenye chai ikiwa vipande vidogo au ikiwa imekauchwa na kusagwa kama ungaunga. Zipo njia nyingi za kutumia tangaizi. Zifuatazo ni katika baadhi ya faida za tangaizi iafya:-
- Tangaizi ni mujarabu sana katika kutibu kichefuchefu. Hususani kichefuchefu cha mimba. Kwa ujumla kichefuchefu huwapata sana wajawazito, na watu walofanyiwa upasuaji wa ndani. Lakini kinaweza kumpata mtu yeyote. Unaweza kutumia tangaizi kwenye chai, ama kutafuna vipande vidogo. Hakikisha unakula japo gram moja.
- Hupunguza maumivu ya misuli
- Hupunguza maumivu ya viungo
- Husaidia katika kushusha kiwango cha sukari. Hususan kwa wenye kisukari type 2. kwa kufanya hivi pia hupunguza athari ya kupata maradhi ya moyo
- Husaidia kwa wenye tatizo la kutokupata choo na kukosa hamu ya kula.
- Hupunguza maumivu ya tumbo la chango kwa wanawake.
- Hupunguza hatari ya kupata ugonjwa wa saratani (cancer)
- Huimarisha afya ya ubongo
- Husaidia katika kuimarisha mfumo wa kinga za mwili.
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 ai web app 👉2 web hosting 👉3 Madrasa kiganjani 👉4 Kitabu cha Afya 👉5 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w) 👉6 Simulizi za Hadithi Audio
Post zinazofanana:
Faida za kiafya za mchaichai/lemongrass
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za mchaichai/lemongrass
Soma Zaidi...Faida za kula parachichi
Somo hili litakwenda kukueleza na kukuelimisha kuhusu umuhimu wa kula parachichi kiafya
Soma Zaidi...Vyakula vinavyosaidia kupunguza uzito
Posti hii inahusu vyakula ambavyo vinasaidia kupunguza uzito, ni baadhi ya vyakula ambavyo unaweza kutumia ili kuweza kuweka kwenye hali ya kawaida.
Soma Zaidi...Kazi ya Piriton
Posti hii inahusu zaidi kazi ya Piriton katika kutibu mzio au akeji ni dawa ambayo kwa lingine huitwa chlorpheniramine Maleate.
Soma Zaidi...