Hapa nitakufindisha faida za kusoma quran kwa Tajwid.
Fadhila na umuhimu wa tajwid.
Kwa hakika tunatambuwa sasa kuwa elimu ya tajwid ina umuhimu mkubwa kwenye umma wetu wa kiislamu. Kwani msomaji kama hatachunga kisomo anaweza kubadilisha maana ya qurani kabisa. Hivyo elimu ya tajwid inaweza kuwa ni msingi wa kuchunga maana ya matamshi ya qurani katika usomaji.
Tunahitajia imamu mwenye kiraa kizuri kwa sauti pia awe anajuwa tajwid na anaitumia ipasavyo. Amesema Mtume (s.a.w): Kutoka kwa Abu Mas’uud Al-Answaariyy ( رضي لله عنه ) amesema: Mtume ( صلى لله عليه وسلم ) amesema: ((Awaswalishe watu yule mwenye kujua kusoma zaidi Kitabu cha Allaah na wakiwa katika kusoma wako sawa, basi mwenye ujuzi zaidi wa Sunnah, na wakiwa kwenye Sunnah wako sawa, basi aliyetangulia Hijrah, na wakiwa katika hijrah wako sawa, basi mkubwa wao kwa umri, wala asiswalishe mtu (mwengine) katika nyumba yake wala katika mamlaka yake wala asikae mahali pake pa heshima isipokuwa kwa idhini yake))
Halikadhalika watu hupenda kusikiliza kiraa cha mtu anayesoma vizuri kwa sauti na kuchunga hukumu za tajwid. Na hivi pia ndivyo Mtume (s.a.w0 anvyotuambia:Kutoka kwa Abu Muwsaa Al-’Ash’arriy ( رضي لله عنه ) kwamba Mtume kamwambia: ((Ungeliniona jana nilivyokuwa nakusikiliza kisomo chako. Hakika umepewea mizumari miongoni mwa mizumari ya aila ya (Daawuwd)
Msomaji wa qurani atakukuwa pamoja na malika wema wenye kuandika. Imetoka kwa ‘Aaishah ( رضي لله عنها ) kwamba Mtume ( صلى لله عليه وسلم ) amesema: ((Yule aliyekuwa hodari wa kusoma Qur-aan atakuwa pamoja na Malaika Waandishi [wa Allaah] watukufu wema, na yule ambaye anaisoma Qur-aan kwa mashaka na huku anajitahidi kwa kudodosa atapata ujira mara mbili)).
Umeionaje Makala hii.. ?
Nguzo za imani (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...Asbab nuzul surat al bayyinh. Sura hii imeteremka Madina na ina aya nane.
Soma Zaidi...Sura hii ni miongoni mwa Sura fupi sanya huwenda ndiosura yenye aya chache kuliko sura zote katika Quran.
Soma Zaidi...Sura hii inaonya vikali tabia ya kusengenya na kusambaza habari za uongo. Wameonywa vikali wenye tabia ya kujisifu kwa mali, kukusanya mali bila ya kuitolea zaka.
Soma Zaidi...3; Mchujo wa maji dhaliliKatika aya nyingine tunakuja kupata funzo kuwa maji aliyoumbiwa mwanadamu licha yakuwa na sifa zilizotajwa katika kurasa zilizopita ila pia maji haya yanasifa kuwa ni madhalilina pia na yamechujwa kama tunavyoelezwa katika quran??
Soma Zaidi...