3; Mchujo wa maji dhaliliKatika aya nyingine tunakuja kupata funzo kuwa maji aliyoumbiwa mwanadamu licha yakuwa na sifa zilizotajwa katika kurasa zilizopita ila pia maji haya yanasifa kuwa ni madhalilina pia na yamechujwa kama tunavyoelezwa katika quran??
3; Mchujo wa maji dhalili
Katika aya nyingine tunakuja kupata funzo kuwa maji aliyoumbiwa mwanadamu licha ya
kuwa na sifa zilizotajwa katika kurasa zilizopita ila pia maji haya yanasifa kuwa ni madhalili
na pia na yamechujwa kama tunavyoelezwa katika quran
β βAmbaye ametengeneza umbo la kila kitu, na akaanzisha umbo la mwanadamukwa udongo.
Na kisha akakifanya kizazi chake kwa mchujo wa maji yaliyo madhalili β β[32:7-8]
βje ! hatukukuumbeni kwa maji yaliyo madhalili? β β [77:20]
kwa ufupi matumizi ya neno sulala kwenye aya hii yanatupa picha hilisi kuwa sio maji yote
yalitumika katika utungaji wa mimba bali kulifanyika mchujo wa majimaji hayo. Yaani ni
sawa na kusema kuwa sio mbegu zote zilizomo kwenye majimaji ya manii zilitumika katika
utungaji wa mimba bali mmajimaji haya ya manii yalichujwa na mengine kutumika na
mengine kuachwa.
Mchujo huu tukakuja uona vizuri hapo chini.
Uthibitisho wa sayansi
Sayansi inathibitisha kuwa sio kiasi chote cha mbegu za kiume yaan sperm hutumika katika
utungaji wa mimba bali kiwango kidogo sana ndo hutumika kama tutakavyoona;-
1; sayansi inathibitisha kuwa manii ni mchanganyiko wa majimaji yapatikanayo katika tezi na
mbegu za kiume zinazopatikana kwenye korodani. 95% ya manii ni majimaji hayo na 2%
ni mbegu yaani sperm. Lakini katika utungaji wa mimba mbegu pekeyake ndo hutumika
yaani katika kukutana kwa mbegu na yai majimaji mengine yanabakia pembeni na mbegu
pekee ndo huhitajika katika utungaji wa mimba. Hivyo huu ni mchujo wa majimaji hayo
2; sayansi imegunduwa pia katika ejaculationmoja mwanaume hutoa mbegu zifikazo milioni
250- 300 lakini katika utungaji wa mimba mbegu moja tuu ndo hutumika vinginevyo chance
ya kutumika mbili ipo lakini ni ndogo sana kwa baadhi ya mimba za mapacha. Huu bila shaka
nao ni mchujo wa majimaji hayo.
3; katika tumbo la mama sehemu inayohusika katika utungaji wa mimba huwa na hali ya asidi
hivyo hali hii huzifanya zile mbegu zilizo dhoofika kufa na kubakia zile zenye nguvu ambazo
ndo zitakwenda kuminyana katika utungaji wa mimba. Hivyo hali hii pia inatupa picha jinsi
mchujo huu unavyozidi kufanyika.
4; wakati mamilioni ya mbegu za kiume spermatozoansyanapokutana na yai
huminyanakulilainisha na kupata nafasi ya kuingia ndani ili nuclear ya mbegu ikakutane na ile
ya yai yaan ovum. Katika kiminyano hiki mbegu ya kwanza ikibahatika kuingia yai
linatengeneza utando mgumu ambao utazuia mbegu nyingine kuingia. Hivyo hapa tunazidi
kupatapicha zaidi jinsi mchujo huu unavyoendelea kufanyika.
Kwa kumalizia matumizi ya neno la kiarabu sulala limesaidia kutupa picha halisi ya kuwa
majimaji haya yalichujwa kwa namna mbalimbali na kupata sample moja.
Umeionaje Makala hii.. ?
Unazijua faida za kusoma Quran, na je ni faida gani utapata ukisoma Quran?
Soma Zaidi...surat Zalzalah ni sura ya 99 katika mpangilio wa Quran, na ina aya 8. Sura hii imeteremshwa Madina ila pia kuna kauli zinathibitisha kuwa ni ya Makkah. Katika hadithi iliyopewa daraja la hassan na Imam Tirmidh Mtume S.A.W amesema kuwa kusoa surat Zilzalah
Soma Zaidi...SURATUL-KAUTHAR Imeteremshwa maka, na sura hii imeshuka kwa sababu al-aAs ibn Waail.
Soma Zaidi...Quran (EDK form 3:dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...Jifunze namna ya kusoma quran, pata mafunzo ya tajwid hapa
Soma Zaidi...SURA YA NNE HUKUMU ZA MIYM YENYE SAKNA HUKUMU ZA MIYM SAKINA: Mym sakina ni miym ambayo haina iβrab ( Ω Ω).
Soma Zaidi...Asbsb nuzul surat al alaqa, sababu za kushuka surat alaqa. Sura hii imeshuka Makka na ina aya 19. Ni sura ya 96 katika mpangilio wa Quran.
Soma Zaidi...