Ni zipi hizo herufi saba, na ni vipi viraa saba katika usomaji wa Quran
Viraa saba na herufi saba.
Wataalamu wa tajwid wanaeleza kuhusu herufi saba za usomaji wa qurani. Itambulike kuwa qurani imeshuka kwa lugha ya kiarabu. Na pia itambulike kuwa waarabu wenyewe walitofautiana katika lahaja za lugha ya kiarabu. Lahaja hizi zilikuwa katika makabila saba ya kiarabu yaliyopo maka. Yaani ni kuwa waarabu walikuwa na makabila saba wakati ule. Na makabila haya ijapokuwa yalizungumza kiarabu lakini walikuwa wakitofautiana katika maneno, utamkaji na hata uandishi. Hivyo lahaja hizi zilijulikana kama herufi saba (za usomaji wa qurani).
Hivyo lahaja saba hizi ndizo chanzo za hizi herufi saba. Na hili linathibitika katika maneno ya Mtume (s.a.w) aliposema: ((Jibriyl alinisomea kwa herufi moja, nikaifanyia marudio mpaka akanifundisha nyingine, nikaendelea kumuomba nyinginezo mpaka mwishowe zikawa herufi (lahaja) saba)) (Bukhari na Ahmad).
Makabila haya yalikuwa Quraysh, Hudhayl, Thaqiyf, Hawaazin, Kinaanah, Tamiym na Yeman. Hivyo qurani ilishuka katika lahaja saba kulingana na makabila. Hivyo ikawa kila kabila linasoma qurani kwa namna ambavyo lahaja yao inawafanya waelewe. Wakawa watu wanaandika qurani kwa namna ambavyo wanaelewa wao. Kulingana na lahaja ya kabila lao. Hali hii ilifanya usomaji wa qurani utofautiaane. Mifano; “’alayhim” wengineo walitamka “’alayhimuw”, neno la “swiraatw” walitamka wengineo “zwiraatw” na wengine “siraatw”, “muumin” wengineo walitamka “muwmin”
Amesimulia ‘Umar Ibn Al-khatab kuwa: “Nilimsikia Hishaam ibn Hakiym akisoma Suwratul-Furqaan tofuati na vile ninavyoisoma na alivyonifundisha Mtume ( لى لله عليه وسلم B). Nilikaribia kumsimamisha (asiswalishe) lakini nikamvumilia mpaka akamaliza kisha nikamshika nguo yake shingoni na kumvuta mpaka kwa Mtume لى لله عليه وسلم) B) nikasema: “Nimesikia huyu mtu akisoma (Suwratul- Furqaan) kinyume na ulivyonifundisha”. Mtume ( لى لله عليه وسلم B) akasema: ((Mwachie!)) Akamwambia (Hishaam): ((Soma)). Akasoma. Akasema ((Hivi ndivyo ilivyoteremshwa)). Kisha akaniambia mimi: ((Soma)). Nikasoma. Akasema: ((Hivi ndivyo ilivyoteremshwa. Hakika Qur-aan imeteremshwa kwa herufi saba, hivyo someni iliyokuwa sahali kwenu)
Uislamu ulipoenea zaidi ikawepo haja ya kuiandika qurani katika lahaja moja ambayo itasomwa. Na hii ni kutokana na kuwepo makosa katika usomaji wa qurani. Hivyo katika utawala Kikundi cha Maswahaba, kilichoongozwa na Hudhayfah bin al-Yamaaniy ambaye alikuwa Iraq, kilikuja kwa ‘Uthmaan ( رضي لله عنه ) na wakamsihi "auokoe ummah wa Kiislamu kabla haujatofautiana juu ya Quraan." ‘Uthmaan ( رضي لله عنه ) akaamrisha chini ya uongozi wa Zayd bin Thaabit رضي لله عنه) ) nakala za Qur-aan ziandikwe na nakala zote zisizo rasmi zichomwe moto.
Lahaja iliyotumika kuandika Qur-aan ni ile ya ki-Quraysh na Msahafu ukajulikana kuwa ni ‘Msahafu wa ‘Uthmaan’. Nakala hizo zilisambazwa miji mikuu ya Waislamu zikiwa kama nuskhah (kopi) rasmi. Na nuskhah ya asili ikabakishwa kwa Mama wa Waumini Hafswah ( رضي لله عنها ). Alimwacha Zayd bin Thaabit Madiynah, ‘Abdullaah bin Swaa’ib alitumwa Makkah,Mughiyrah bin Shu’bah alitumwa Syria, Abu ‘Abdir-Rahmaan As-Sulamy alitumwa Kuwfah, ‘Aamir bin ‘Abdil-Qays alitumwa Baswrah. (www.al-hidaayah.com)
Baada ya msahafu huu kusambazwa katika dola ya kiislamu lahaja zote ambazo siorasmi zilipotea. Msahafu huu ndio chimbuko la misahafu tulionayo leo. Ijapokuwa kuna tofauti kubwa za kiuandishi kati ya misahafu ya leo na msahafu huu. Kwa m fano msahafu huu haukuwa na dot kwenye herufi za dot au irabu pia hazikuwepo. Hayo yato yalifanyika baadaye kadiri uislamu ulipoenea maeneo mbalimbali ya dunia na ikaonekana ugumu wa kutumia msahafu ule kwa watu wasiokuwa waarabu.
Viraa saba.
Viraa hivi saba ndivyo ambavyo vimetokana na lahaja ya kikurayshi ambayo ndio msahafu wa ‘Uthmani umeandikiwa. Viraa hivi wataalamu wa elimu ya tajwid wamevizungumzia katika vitabu vya elimu hii.
Je! umeipenda hii post?
Ndio Hapana Save post
Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Topic: Quran Main: Post File: Download PDF Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 2088
Sponsored links
👉1 Madrasa kiganjani
👉2 Kitabu cha Afya
👉3 kitabu cha Simulizi
👉4 Kitau cha Fiqh
👉5 Simulizi za Hadithi Audio
👉6 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)
Kukusanywa na kuhifadhiwa kwa quran
Quran (EDK form 3: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...
quran na sayansi
Soma Zaidi...
Mtume hakufundishwa quran na Jabir na Yasir
Soma Zaidi...
Sababu za kushuka surat at Takaathur
Kuwa na tamaa huhitaji vitu vya watu si jambo jema. Ila kama tamaa hii itakuhamasisha na wewe kutafuta kitu hicho, kwa uwezo ambao Allah amekupa bila ha kuvuka mipaka yake, hili sio tatizo. Sura hii itakufundisha mengi Soma Zaidi...
Qur-an Yenyewe Inajieleza kuwa ni Ufunuo Kutoka kwa Allah (s.w)
(ii)Qur-an Yenyewe Inajieleza kuwa ni Ufunuo Kutoka kwa Allah (s. Soma Zaidi...
Quran si njozi za mvurugano alizoota Mtume Muhammad
(ii)Dai kuwa Qur-an ni zao la njozi za Mtume (s. Soma Zaidi...
As-Sab nuzul
Sababu za kuteremshwa baadhi ya sura Katika darsa hii tutaangalia sababu za kushuka kwa aya na sura ndani ya quran. Soma Zaidi...
HUKUMU ZA MIIM YENYE SAKINA (MIIM SAKINA)
HUKUMU ZA MIYM YENYE SAKNA : Mym sakina ni miym ambayo haina i’rab ( مْ). Soma Zaidi...
HUKUMU ZA QALQALA
Jifunze namna ya kusoma quran, pata mafunzo ya tajwid hapa Soma Zaidi...
Madai ya makafiri dhidi ya quran na hoja zao
Soma Zaidi...
Sababu za kushuka sural Masad (tabat haraka)
Sura hii inazungumzia kuhusu hali ya Abulahab namke wake wakiwa kama Watu waovu. Ni moja katika sura ambazo zilishuka mwanzoni toka Mtume alipoamrishwa kulingana dini kwa uwazi. Soma Zaidi...