Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za ukwaju
. Faida za ukwaju (Tamarind)
Ukwajju ni katika mimea ambayo matunda yake yanatumika katika kutengenezea madawa ya hospitali. Kinywaji cha ukwaju hutumika katika kutibu kuharisha, kukosa choo, homa na aina za vidonda vya tumbo. Tofauti na matunda pia majani na maganda ya mti huu pia hutumika katika kutibu vidonda. Wataalamu wa afya bado wanaendelea kuuchunguza mti huu kwa ajili ya kupata tiba zaidi.
Antioxidant ambayo ipo kwenye ukwaju husaidia katika kudhibiti na kulinda mwili dhidi ya maradhi ya moyo, saratani na kisukari. Wataalamu wa afya wanaeleza kuwa ukwaju husaidia katika kushusha kiwango cha sukari kwenye damu. Pia kwa watu wenye kutaka kupunguza uzito, ukwaju pia husaidia.
Ukwaju una virutubisho vingi sana kama vile:- madini ya magnesium, potassium, chuma, calcium na phosphorous. Pia kuna vitamin B1 (thiamin), vitamin B2 (riboflavin), vitamin B3 (niacin). pia kuna vitamin C, k na B6 na B5. kwa ufupi ukwaju ni katika matunda ya asili yalotumiwa na watu toka zamani sana.
Katika ukwaju kuna polyphenols kama vile flavonoids ambayo husaidia katika kudhibiti kiwango cha cholesterol na triglycerides. Antioxidant zilizomo kwenye tunda hili husaidia katika kulinda mwili dhidi ya maradhi ya moyo. Pia ukwaju husaidia katika kutengeneza dawa za malaria.
Tafiti za kisayansi zinaonesha kuwa ukwaju husaidia katika kupunguza uzito. Itambulike kuwa kuzidi uzito mwilini kunahusianishwa sana na maradhi ya moyo, ini, na figo. Hivyo ukwaju husaidia katika kupunguza choloesterol mbaya (LDL) na husaidia katika kuongeza cholesterol nzuri (HDL).
Ukwaju una potassium bitartipate ambayo hii husaidia katika upatikanaji wa choo na kuzuia kuganda kwa choo. Mizizi na maganda ya mkwaju husaidia sana kwa maumivu ya tumbo. Uw.epo wa procyanidins kwenye ukwaju husaidia katika kulinda ini dhidi ya uharibifu. Pia ukwaju hutumika katika kutibu along’atwa na nyoka
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetuUmeionaje Makala hii.. ?
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kula fyulisi/ peach
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu aina za vyakula vya fati na umuhimu wake mwilini
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi namna nzuri ya kuandaa mchai chai kwa ajili ya matumizi mbalimbali, Ili kutumia mmea wa mchai chai zifuatazo ni mbinu za kuandaa mmea huu.
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu vyakula vya kuongeza damu
Soma Zaidi...