Matunda ya zamani na ya asili, zijuwe faida za kiafya za tango
17.Tango (coccumber).
Tango ni katika mimea jamii ya matikiti na maboga. Tango ni katika matunda ambayo unatakiwa uyale sana kwenye maisha yako. Tafiti zinaonesha kuwa asilimia 95 ya tango ni maji. Tango lina vitamin K, B vitamins, copper, potassium, vitamin C, na madini ya manganese.
Tango lina anti-inflammatory flavonol ambayo huitwa fisetin. Hii husaidia katika kuimarisha afya ya ubongo. Hii husaidia katika kutunza kumbukumbu na kuimarisha afya ya mfumo wa fahamu pamoja na neva.
Tafiti zinaonesha kuwa tango lina polyphenols ambazo huitwa lignans (pinoresinol, lariciresinol, and secoisolariciresinol), husaidia katika kuzuia kupata aina mbalimbali za saratani (cancer) kama saratani ya kizazi kwa wanaume na wanawake.
Tango pia lina antioxidant flavonoids, kamavile quercetin, apigenin, luteolin, na kaempferol, ambazo husaidia katika kupambana na maradhi kama saratani na maradhi mengineyo.
Tango hupunguza joto tumboni, pia huondoa bajteria wanaoleta harufu mbaya mdomoni. Tafiti zinathibitisha kuwa tango husaidia katika kuondoa misongo ya mawazo na hii ni kutokana na uwepo wa vitamin B1, vitamin B5, and vitamin B7 (biotin) kwenye tango.
Tango huimarisha afya ya moyo na kupumguza shinikuizo la damu. Tanago husaidia mfumo wa kumengβenya chakula ufanye kazi kwa ufanisi. Tango husaidia katika kuthibiti uzito wa mwili.
Umeionaje Makala hii.. ?
Some Hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kula mihogo
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu vyakula ambavyo vinaweza kupunguza presha ya kupanda
Soma Zaidi...Posti hii inahusu vyakula ambavyo vinasaidia kupunguza uzito, ni baadhi ya vyakula ambavyo unaweza kutumia ili kuweza kuweka kwenye hali ya kawaida.
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kula bamia
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kula chungwa/orange
Soma Zaidi...Palachichi lina virutubisho vingi na vitamini, kula palachichi uiokoe afya yako
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kula mayai
Soma Zaidi...Nanasi ni katika matunda matamu lakini mazuri pia kiafya, je unazijuwa faida zake kiafya
Soma Zaidi...