Posti hii inahusu zaidi aina mbalimbali za Magonjwa ya moyo,kwa kawaida tunajua wazi kuwa kuna moyo mmoja lakini moyo huo unaweza kushambuliwa na magonjwa kwa kila aina kwa mfano kuna Maambukizi kwenye mishipa ya moyo,au kubadilika kwa mapigo ya moyo na m
1. Kuathirika kwa mishipa ya moyo.
Kwa wakati mwingine kuna kuathirika kwa mishipa ya moyo ambayo kwa kitaalamu huitwa coronary artery, mishipa hii inaweza kupata Maambukizi na kushindwa kusafilisha damu kutoka kwenye moyo na kupeleka sehemu mbalimbali za mwili. Pengine mishipa inaweza kushindwa kusafilisha damu kwa sababu ya kuwepo kwa uchafu na mafuta kwenye mishipa hali hii usababisha moyo kusukuma damu kwa nguvu ili kuweza kukidhi mahitaji ya mwili hali hii usababisha kuaribika kwa mishipa ya moyo.
Kwa hiyo tunapaswa kupunguza vyakula vyenye mafuta mengi na kuhakikisha kuachana na vyakula vyenye sumu ambavyo Usababisha kuwepo kwa mafuta kwenye mishipa na kuwepo kwa uchafu kwenye mishipa kwa kuepuka mambo hayo tutaweza kuruhusu damu kusafili zaidi na kuepuka na kuaribika kwa mishipa ya damu.
3.Aina nyingine ya ugonjwa wa moyo ni mapigo ya moyo kwenda tofauti.
Kwa wakati mwingine mapigo ya moyo uenda haraka na kusababisha mtu kuwa na jasho na pengine mtu anakuwa hatulii sehemu moja . Na pia kwa wakati mwingine kuna kipindi mapigo ya moyo yanaenda taratibu sana kwa hali hii umfanya mtu kupumua kwa shida . Na kuna kipindi kingine mapigo ya moyo uenda ovyoovyo bila mpangilio hali hii ni mbaya sana inaweza kusababisha matatizo mengine makubwa kama vile kupoteza maisha.
4.Kwa wahudumu na ndugu wa mgonjwa baada ya kuona dalili kama hizi wanapaswa kumpeleka mgonjwa hospitalini ili aweze kupata matibabu kwa sababu hali ya kubadilika ki mapigo huwa sio nzuri hasa kwa mgonjwa yule ambaye ni mara yake ya kwanza kwa sababu anaweza kupanic na kuona kuwa ndio mwisho basi tuwafariji na kuwa pamoja nao ili waweze kupata huduma za muhimu.
5. Aina nyingine ni ile ya moyo kushindwa kufanya kazi.
Kuna kipindi ambapo moyo unashindwa kufanya kazi kwa sababu mbalimbali kama vile kuwepo kwa kiasi kidogo cha damu kwenye mwili au Maambukizi kwenye valve za mishipa.kwa hiyo hali hii isipogunduliwa mapema Mgonjwa anaweza kupoteza maisha kwa watu wenye tatizo kama hili wanaweza kutumia kifaa maalum ambacho usaidia moyo ili uweze kufanya kazi na pia kifaa hicho kwa kawaida huwa kinabadilika mara kwa mara kadri ya maoni ya wataalamu wa afya.
6.Kuna wakati mwingine moyo ushindwa kufanya kazi kwa ghafla kwa sababu ya matukio mbalimbali na kuna huduma ambayo utolewa kwa ajili ya kushutua moyo huduma hiyo uitwa cardiopulmonary Resuscitation, hii huduma utolewa kwa wale wenye utamaalamu na mafunzo maalum kwa ajili ya kushutua moyo uliosimama ghafla.
7. Kuna aina nyingine t Magonjwa ya moyo ambayo huwapata watoto
Kwa wakati mwingine watoto wanaozaliwa na ugonjwa huo kwa sababu kuna kesi mbalimbali zinazoonyesha kuwa mtoto amezaliwa na tundu kwenye moyo, hali hii utokea kwa sababu ya mtindo wa maisha kwa Mama wajawazito kama vile uvutaji wa sigara, utumiaji wa madawa ya kulevya wakati wa ujauzito na pia kutumia vileo vikali wakati wa ujauzito hayo yote usababisha watoto kuzaliwa na matundu kwenye Aorta.
8.Kwa hiyo ili kuepuka na matatizo haya wanawake wakati wa ujauzito wanapaswa kufuata mashariti ya wataalamu wa afya na kuachana na vileo, madawa ya kulevya, pombe kali na mambo kama hayo ili kuweza kuepuka matatizo kama hayo wakati wa ujauzito, kwa hiyo akina Mama pia wahudhuria maudhurio yote ya kliniki ili kuweza kusikiliza mafundisho kwa sababu hayo mafundisho utolewa kila mwezi kipindi mama akiwa kwenye mahudhurio ya kawaida.
9. Aina nyingine ya Magonjwa ya moyo ni pamoja na moyo kutanuka.
Kuna kipindi ambapo moyo unataka kusiko kwa kawaida kwa sababu ya kutanuka kwa misuli ambayo imeuzunguka moyo au kwa sababu ya kutanuka kwa kuta za moyo, kwa hiyo moyo unatumia nguvu sana kusukuma damu na kusababisha misuli yake kutanuka. Sababu kuu ambazo Usababisha moyo kutanuka ni kuwepo kwa presha kubwa juu. Kuwepo kwa Maambukizi kwenye mishipa ya moyo na mambo mengine kama hayo.
10. Aina nyingine ya magonjwa ya moyo ni kuwepo kwa Shinikizo la damu kwa kitaalamu huitwa blood pressure, ni hali ambayo utokea kama kuna presha iko juu kwa sababu ya moyo kutumia nguvu katika kusukuma damu au pengine kama mwili una Maambukizi vile usababisha kuwepo kwa shinikizo la damu au pengine ni kwa sababu ya kuwepo kwa mafuta kwenye mishipa ya damu ambapo damu kidogo uruhusiwe kupita na hapo mwili unahitaji kiwango kikubwa cha damu, kwa hiyo moyo usukuma damu kwa nguvu na kusababisha shinikizo la damu.
11. Chembe ya moyo. Pia hii nayo ni aina ya magonjwa ya moyo kwa kawaida mgonjwa uhisi maumivu kwenye kifua hali hii inaweza kutokea kama mtu anafanya kazi au amekataa, Maumivu pia uendana pamoja na kutokwa na jasho pia kukosa hewa safi, hasa hasa tatizo hili utokea kama mgonjwa hana damu ya kutosha mwilini.
12.Aina nyingine ni kufa kwa sehemu ya misuli ya moyo.
Kuna wakati mwingine sehemu za misuli ya moyo zinakufa hali ambayo Usababisha moyo kushinwa kufanya kazi zake za kila siku na tatizo kama halijulikana moyo unaweza kushindwa kufanya kazi zake kwa kila siku.
13. Aina nyingine ni damu kushindwa kusambaa.
Kuna kipindi moyo inasukuma damu na damu inashindwa kusambaa kwenye sehemu mbalimbali za mwili kwa sababu ya Maambukizi kwenye mishipa ya damu. Hali hii utokea kwa sababu ya kuwepo kwa mafuta kwenye sehemu mbalimbali za mishipa ya damu.
Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.
Download NowAnemia ya upungufu wa vitamini ni ukosefu wa seli nyekundu za damu zenye afya unaosababishwa na kiasi kidogo cha vitamini fulani kuliko kawaida.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu huduma kwa wanawake wenye mahitaji maalum, ni wanawake ambao wana shida ya akili, walionyanyaswa kijinsia, wakimbizi na wote wenye matatizo mbalimbali.
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu njia za kupambana na kisukari
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu watu walio hatarini kupata gonorrhea gonoria
Soma Zaidi...Posti hii inazungumzia kuhusiana na Ugonjwa wa Brucellosis ni maambukizi ya bakteria ambayo huenea kutoka kwa wanyama hadi kwa watu mara nyingi kupitia maziwa ambayo hayajasafishwa au kuchemshwa vizuri na bidhaa zingine za maziwa. Mara chache zaidi, ba
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi namna ya kuzuia maambukizi kwenye tumbo na utumbo mdogo, hizi ni njia ambazo zinapaswa kufuatwa ili kutokomeza kabisa maambukizi kwenye tumbo na utumbo mdogo.
Soma Zaidi...Watu wengi wamekuwa na mawazo kuwa ili nipate ukimwi ninatakiwa nishiriki ngono zembe na aliyeathirika mara ngapi? Majibu ya swali hili ni mafupi tu, ni kuwa unaweza kuathirika kwa ngono zembe ya siku moja tu ndani ya dakika chache. Lakini jambo la kuzing
Soma Zaidi...Posti hii inaelezea kuhusiana na Ugonjwa wa upungufu wa Adrenali ni ugonjwa ambao hutokea wakati mwili wako hutoa kiasi cha kutosha cha homoni fulani zinazozalishwa na tezi zako za adrenali. ugonjwa huu hutokea katika makundi yote ya umri na huathiri
Soma Zaidi...Posti hii inaelezea kuhusiana na dalili na sababu zinazopelekea Ugonjwa wa kuziba kwa Njia ya machozi yaani kukosa machozi ambayo husababishwa na maambukizi.
Soma Zaidi...Posti hii inazungumzia kuhusiana na maambukizi ya tishu ya matiti ambayo husababisha maumivu ya matiti, uvimbe, joto na uwekundu. Pia unaweza kuwa na Homa na baridi. Ugonjwa huu huwapata zaidi wanawake wanaonyonyesha ingawa wakati mwingine hali hi
Soma Zaidi...