Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu maradhi ya cancer/saratani
SARATANI (CANCER)
Saratani ni ugonjwa unaotokana na kukuwa kwa seli ndani ya mwili bila ya mpangilio maalumu. Kukuwa huku kunashindwa kuthibitika ndani ya mwili. Seli hizi hukuwa na kusababisha kitu kinachoitwa kitaalamu tumor. Hii ni mkusanyiko wa hizi seli ambazo zimekuwa bila ya mpangilio maalumu ndani ya mwili. Hizi tumor husababisha kutokea kwa malignant tumor na hii ni mkusanyiko mkubwa wa hizi seli ambao huuwa seli nyingine za mwili na tishu. Hutokea wakati mwingine huu mkusanyiko ukawepo ila ukawa hauna madhara kwa seli nyingine, huu utaitwa benign tumor ila zikikuwa zaidi huweza kuathiri tishu za mwili. Hizi tumor zinaweza kuingia kwenye mfumo wa damu na kuenea sehemu zingine za mwili.
Seli za saratani ni hatari zaidi kwani zinaweza kuharibu tishu na viungo vingine vya mwili kama ubongo na maini. Kiti hatari zaidi kwenye seli hizi ni kuwa zinaweza kuhama sehemu moja ya mwili kwenda sehemu nyingine. Kwa mfano saratani ya maini inaweza kuenea kwenye ubongo na kusababisha saratani ya ubongo. Saratani ya matiti na korodani inaweza kuenea kwenye mifupa na kusababisha saratani ya mifupa.
Hali hii hufanya seli hizi ziwe hatari zaidi. Mchakato huu wa kuhama sehemu moja kwenda nyingine huitwa kitaalamu metastasisi.
Seli ya saratani ya kwanza hutokea pale gene zinapopata hitilafu. Gene ni chembechembe ambazo huhusika katika kutengenezwa kwa selimmpya. Mtu anaweza kurithi gene hizi ambazo zimeharibiwa toka kuzaliwa ama akawa anazo zimeharibiwa kwa sababi zingine. Ila mtu huyu aliyerithi gene ambazo zina hitilafu ni rahisi kwake kupata saratani zaidi kuliko huyu ambaye hajarithi. Kama tulivyoona juu kule kuna mawakala wa kueneza maradhi, hali kama hii kuna mawakala wa kusababisha saratani ambao huitwa carcinogens hawa pia huhusika katika kutia hitilafu kwenye genes. Mifano ya mawakala hawa (carcinogens ) ni ;-
1.Aina flani ya virusi kama vile papilloma virus (HPV)
2.Mionzi kama radio na ulteraviolent (UV) na mionzi mingineyo.
3.Kemikali zinazopatikana kwenye tumbaku kama arsenic, benzene na formaldehyde
4.Asbestos haya ni malighafi zinazotumika kutengezea vifaa vya umeme na vifaa vingine vya nyumba kama vya kuzuia moto.
Ni vigumu sana kuepukana na mawakala hawa kwenye maisha, kwani huweza kupatokana kwwenye vyakula vyetu, shuhuli zetukwenye maji na hewa. Ila tutakujaona kwamba unaweza kujiepusha na hatari za saratani kwani karibia mawakala walotajwa hapo juu hueneza saratani ila kwa uchache ila tumbaku ni kwa kiasi kikubwa sana.
Unaweza ukagunduwa saratani kwa kutumia vifaa vya kitaalamu kama MRI, x-rays, biospy, na DNA test. Pia unaweza ukajijua mwenyewe kama una tumor kwa kujishika sehemu husika na kuona kama kuna uvimbe wowote usio wa kawaida. Pia ijulikane kuwa zipo tiba za saratani ijapokuwa kuimaliza kabisa mwilini ni kazi mzito ila ukweli ni kuwa karibia aina zote za saratani zinaweza kutibiwa kama mtu atawahi kwa haraka.baadhi ya njia wanazotumia kupambana na saratani ni kama
A)kufanyiwa upasuaji, hufanyika kwa ufasaha zaidi kama saratani haijaenea zaidi
B)Kufanya chemotherapy ni matumizi ya dawa kwa ajili ya kuuwa seli za saratani, ila kwa bahati mbaya njia hii pia huuwa seli nyingine za mwili
C)Radiation therapy ni kutumia mionzi kwa ajili ya kuuwa seli za saratani
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetuUmeionaje Makala hii.. ?
Somo Hili linakwenda kukueleza kuhusu dalili za presha ya kushuka
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu namna ya kuishi na vidonda vya tumbo
Soma Zaidi...Post yetu inaenda kuzungumzia kuhusiana na Saratani ya Matiti ni Saratani ambayo hutokea katika seli za matiti. Baada ya Saratani ya Ngozi, Saratani ya matiti ndiyo Saratani inayojulikana zaidi hugunduliwa kwa wanawake Mara nyingi. Saratani yaÂ
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwenda kujifunz akuhusu ugonjwa wa Bawasiri na dalili zake. Pia utajifunza njia za kujilinda nao.
Soma Zaidi...Hapa utajifunza sababu zinzopelekea mdomo kubadilika ladha na kuwa mchungu, ama mchachu.
Soma Zaidi...Coma ni hali ya kupoteza fahamu kwa muda mrefu ambayo inaweza kusababishwa na matatizo mbalimbali Jeraha la Kichwa, Kiharusi, Uvimbe kwenye ubongo, ulevi wa dawa za kulevya au pombe, au hata ugonjwa wa msingi,
Soma Zaidi...kovu (Fibrosis) ya ini inayosababishwa na aina nyingi za magonjwa na hali ya ini, kama vile Homa ya Ini na unywaji pombe kupita kiasi. Ini hufanya kazi kadhaa muhimu, ikiwa ni pamoja na kuondoa vitu vyenye madhara katika mwili wako, kusafisha damu yako
Soma Zaidi...