Dondoo za afya 41-60

Dondoo za afya 41-60

Somo Hili linakwenda kukuletea dondoo mbalimbali za afya

Download Post hii hapa

? DONDOO 41 - 60

Basi tambua haya;-

41.Njia ambazo ugonjwa wa manjano huambukizwa ni sawa na zile za kuambukiza UKIMWI.

42.Dalili za ugonjwa wa manjano huchelewa kuonekana, na huonekana pale mtu anapokuwa ameshaathirika. Dalili hizo ni kama kukojoa mkojo wa rangi nyeusi, macho na ngozi kuwa njano, kichefichefu cha mara kwa mara, kupungua uzuto, homa kali, mwili kuwa dhaifu, kupoteza hamu ya kula na maumivu makali ya tumbo karibu na ini.

43.Ugonjwa huu pia hauna tiba, ila mgonjwa akiwahi hospitali anaweza kupewa dawa za kupambana na virusi hawa. Pia anaweza kubadilishiwa ini.

44.Mgonjwa mwenye ugonjwa wa manyano anatakiwa asinye pombe, madawa ya kulevya n.k

45.Virusi vya ugonjwa huu wa homa ya manjano ni hatari kuliko vya ukimwi maana vinaweza kukaa nje ya mfumo wa damu mpaka siku saba, wakati vya ukimwi haviwezi kufika hata dakika moja.

46.Mbegu za maboga zinaweza kuwasaidia watu wanaoishi na kisukari. Mbegu hizi zimeonekana kuwa na uwezo wa kusaidia kurekebisha kiwango cha insulin.

47.Madini ya zinc yaliyomo kwenye mbegu za maboga husaidia kuboresha afya ya ubongo na utunzaji wa kumbukumbu.

48.Karanga pia husaidi afya ya ubongo na utunzaji wa kumbukumbu. Kuna vitamin E kwenye karanga, hivi ndivyo vina kazi hii.

49.Mshubiri ni katika tiba za asili sana. Husaidia kuondoa miwasho kwenye ngozi. Pia kuponesha vidonda na michubuko kwnye ngozi. Kata jani lake kisha jipake kwenye jeraha, mchubuko au muwasho.

50.Na muarobani nao pia hutibi maumivi ya sikio , maradhi ya macho na miwash ya ngozi. Changanya mwarobaini uliopondwa na asali kisha weka tone moja wenye sikio. Fanya hivyo kwa siku kadhaa utapona.

51.Tende ni katika matunda ya asili na ni katika matunda yanayoweza kuhifadhiwa kwa muda mrefu kwa njia za asili. Wataalamu wa afya wanazungumza kuwa karibia virutubisho vyote anavyohitajia mwanadamu kuishi vinaweza kupatikana kwenye tende. Pia wataalamu wanaongeza kuwa mtu anaweza kuishi kwa muda mrefu kwa kula tende kokwa chache tu na glas ya maziwa.

52.Maziwa ni katika vinywaji vya asili pia. Maziwa ya mama yanafahamika kwa ubora wake na umuhimu kwa watoto wachanga. Wataalamu wa afya qwanasisitiza kuwanyonyesha watoto kwa muda wa miaka miwili. Halikadhalika maziwa ya ng’ombe na wanyama wengine kama ngamia na mbuzi yamekuwa yakitumiwa sana na watu wazima. Watu wamekuwa wakinywa maziwa kwa ajili ya kuondoa sumu. Halikadhalika maziwa yana virutubisho mauhimu nambavyo mwanadamu anahitajia. Wagonjwa wa vidonda vya tumbo wanashauriwa sana kunywa maziwa.

53.Asali pia ni katika vyakula na vinywaji vya asili. Ukiachilia mbali virutubisho vingi sana vilivyomo kwenye asali, lakini asali pia huweza kutumika kama dawa. Kwa walioungua hupaka asali kwenye jeraha. Asali ina uwezo mkubwa wakuuwa bakteria kwenye kidonda.

54.Nyama ni katika vyakula vyenye protini. Watu wengi hupenda kula vyama. Wapishi wa nyama wanapashwa kuwa makini kwani vyama inatakiwa iiive na kama haitaiva walaji wanaweza kudhurika kama mnyama atakuwa na vijidudu. Vyama vyekundu kama ya ng’ombe na mbuzi zimekuwa zikipatikana zaidi. Lakini wataalamu wa afya wanapendelea zaidi uaji wa nyama nyeupe kama nyama ya samaki, kuku n.k.

55.Samaki ni katika vyakula vya asili pia. Wataalam wa afya wanaeleza kuwa ukuaji salalma wa ubongo kwa mtoto unaweza kuwa maradufu kama mtoto atakuala samaki. Wataalamu wa afya wanasisitika kula samaki akiwa katika supu ama namna ingine. Mafuta ya samaki ni katika sehemu muhimu inayopasa kuliwa kwenye samaki

56.Ni vyema kula matunda ukiwa una vyaa kabla ya kula chakula. Ulaji wa matunda ukiwa na njaa utapelekea mmeng’enyo wa lile tunda kukamilika wote na kuingia kwenye mfumo wa chakula.

57.Ijapokuwa watu wengi hawapendi pilipili ila itambulike kuwa tunda hili ni zuri na lina vitamini anbavyo vinasaidia katika ukuaji wa ubongo.

58.Matunda yenye rangi ya njano kama maembe na machungwa yana kiasi kikubwa cha vitamikni C. Wataalamu wa afya wanaeleza kuwa vitamini hivi ini mujarabu katika kuulinda mwili dhidi ya maradhi mablimbali.

59.Mimea yenye rangi a kijani yaani mboga ina vitamini A. Vitamini hivi pia via kazi ya kuulinda mwili na maradhi. Matatizo ya kutokuona usiku ni kutokana na upungufu wa vitamini hivi.

60.Ni vema kupiga mswaki kabla ya kulala. Ukilala na mabaki ya chakula mdomoni unaweza kukaribisha bakteria kuzaliana kwa kiasi kikubwa kwenye kinywa chako. Hali hii inaweza kuleta madhara katika afya ya meno yako.

Download Post hii hapa

Jiunge nasi WhatsApp
Upate Update zetu

Download App Yetu

Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.

Download Now Bongoclass Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 1970-01-01 03:33:44 Topic: Jifunze Main: Afya File: Download PDF Views 1387

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
👉1 Simulizi za Hadithi Audio    👉2 Kitabu cha Afya    👉3 Bongolite - Game zone - Play free game    👉4 Madrasa kiganjani    👉5 Kitau cha Fiqh    👉6 kitabu cha Simulizi   

Post zinazofanana:

AFYA NA MAGONJWA
AFYA NA MAGONJWA

Pata elimu juu ya afya hapa ukiwa na vitabu vyetu bila ya malipo yoyote

Soma Zaidi...
Namna ya kuzuia dalili za hatari kwa aliyefanyiwa upasuaji
Namna ya kuzuia dalili za hatari kwa aliyefanyiwa upasuaji

Posti hii inahusu zaidi namna ya kuzuia dalili za hatari kwa aliyefanyiwa upasuaji, ni mbinu mbalimbali ambazo utumika ili kujaribu kuepuka Dalili za hatari kwa aliyefanyiwa upasuaji.

Soma Zaidi...
MAANA YA AFYA
MAANA YA AFYA

Pata elimu juu ya afya hapa ukiwa na vitabu vyetu bila ya malipo yoyote

Soma Zaidi...
dondoo 100 za Afya
dondoo 100 za Afya

Basi tambua haya;- 61.

Soma Zaidi...
AINA ZA VYAKULA
AINA ZA VYAKULA

Pata elimu juu ya afya hapa ukiwa na vitabu vyetu bila ya malipo yoyote

Soma Zaidi...
Kitabu cha Afya 03
Kitabu cha Afya 03

Yajuwe mambo yanayoathiri afya ya miili yetu, jifunze mambo mengi kuhusu afya.

Soma Zaidi...
kitabu cha afya
kitabu cha afya

Jifunze sifa na aina za matunda, vijuwe viruturubisho

Soma Zaidi...
UPUNGUFU WA PROTINI NA FATI
UPUNGUFU WA PROTINI NA FATI

Pata elimu juu ya afya hapa ukiwa na vitabu vyetu bila ya malipo yoyote

Soma Zaidi...
Kitabu cha Afya 01
Kitabu cha Afya 01

Soma kitabu hiki cha afya sehemu ya kwanza upate kuijua afya yako.

Soma Zaidi...
DONDOO 100 ZA AFYA
DONDOO 100 ZA AFYA

Pata dondoo 100 za Afya

Soma Zaidi...