Dondoo za afya 1-20

Somo Hili linakwenda kukuletea dondoo mbalimbali za afya

? DONDOO NAMBA 1 - 20

? Basi tambua haya;-

1.asilimia 50-90 ya mwili wa kiumbe hai ni maji. Hivyo mtu anaweza kupoteza uhai kwa haraka zaidi kwa upungufu wa maji.

2.Tende zina oxytocin hii husaidia katika kurahisisha mama wakati wa kujifungua. Hivyo ni vyema mjamzito kutumia tunda hili. Pia tende huongeza kiwango cha maziwa.

3.Hakuna madhara kwenye mafuta ya samaki, isipikuwa kunafaida kubwa. Katika mafuta haya kuna omega3 fat acidi. Hii hjulukana kwa uwezo wake wa kuupa mwili nguvu na uwezo wa kufanya kazi. Pia husaidia katika ichakato ya kikemikali mwilini.

4.Ulaji wa samaki hupunguza hatari ya kupata matatizo ya magonjwa ya moyo na shambulio la moyo.

5.Kufanya mazoezi ni jambo lililolazimishwa na wataalamu wa afya. Angalau kwa wiki mtu afanye mazoezi. Mazoezi huweza kuupa mwili afya na uwezo wa kupambana na maradhi.

6.Usinywe maji punde utokapo masoezini, subirika kidogo kama dakika kadhaa mwili kupoa.

7.Hakikisha unapofanya mazoezi jasho likaukie mwilini hasa kwa wale wenye track sut. Jasho husaidia kukausha mafuta yaliyoganya kwenye ngozi.

8.Kuoga pia ni lazima kwa mwanadamu, kuoga husaidia kuondoa stress yaani misongo ya mawazo.

9.Kuoga ni tiba ya matatizo ya kisaikilojia.

10.Kuna katika ulimi wa mwanadamu bakteria, hawa husaidia katika kuzuia hatari ya vyakula vyenye sumu hasa vile vyenye nitrate kama nyama.

11.Ni vyema kupata muda wa kutosha kwa ajili ya kulala. Mwuli huhitajia muda huo kwa ajili ya kurekebisha mifumo ya mwili na kupona kwa majeraha, pia na kupumzika.

12.Mtu anapolala huwa anageuka geuka, kitendo hiki ni muhimu kwa ajili ya afya. Kama mgonjwa hawezi kugeukageukja anatakiwa ageuzwe upande kila baada ya muda..

13.wakati wa usiku mwili hutoa homini iiitwayo melatonin. Hii husaidia katika kuuandaa mwili kulala. Mapigo ya miyo hushuka.

14.Kutokupata muda wa kutosha kulala lkunaweza kusabababisha mwili kupoteza uwezo wake wa kupambana na maradhi.

15.Kama mtu atakosa muda wa kulala kwa miusiku miwili anaweza kupoteza uwezo wa kufanya kazi kwa ufasaha na kuwa na uwezo mdogo wa kufikiri.

16.Mtu akikosa muda wa kulala kwa miusiku mitatu atapata matatizo ya kuona maluelue na atapoteza uwezo wa kufikiri vizuri.

17.Utafiti uliofanywa marekani umeonesha kuwa watu ambao hawana dini au imani ya mungu wapo hatarini kwa asilimia 60% kupata magonjwa ya moyo kuliko ambao wana imani.

18.Pia wataalamu hawa wa Saikolojia wakaongeza kuwa watu wasio na dini maisha yao ni mafupi sana kuliko qenye dini. Halikadhalika watu hawa wanasumbuliwa na maradhi mara kwa mara.

19.Pia tafiti nyingine zimeonesha kuwa watu ambao wanasamehe au wana uwezo wa kusamehe wanakuwa na afya njema ya mwili na akili kuliko ambao hawasamehe au hawana uwezo wa kusamehe. Hivyo ni vyema kujifunza kusamehe.

20.Pia wameongezea kuwa hasira ni hatari kwa afya ya moyo

Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 1970-01-01 03:33:44 Topic: Jifunze Main: Afya File: Download PDF Views 2890

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
👉1 Kitabu cha Afya    👉2 Tafasiri ya Riyadh Swalihina    👉3 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)    👉4 kitabu cha Simulizi    👉5 Madrasa kiganjani    👉6 Simulizi za Hadithi Audio   

Post zinazofanana:

Sababu zinazopelekea kukosa Usingizi

Posti hii inazungumzia kuhusiana na Sababu zinazopelekea kukosa usingizi. Usingizi ni ugonjwa unaoendelea ambao unaweza kufanya iwe vigumu kusinzia, vigumu kubaki usingizini au vyote viwili, licha ya fursa ya kupata usingizi wa kutosha.Ukiwa na kukosa usi

Soma Zaidi...
KITABU CHA MATUNDA

Jifunze sifa na aina za matunda, vijuwe viruturubisho

Soma Zaidi...
YANAYOATHIRI AFYA KUTOKANA NA VIZAZI, FAMILIA NA KURITHI

Pata elimu juu ya afya hapa ukiwa na vitabu vyetu bila ya malipo yoyote

Soma Zaidi...
Jinsi ya kuimarish afya ya meno

Katika post hii utajifunza namna ambavyo unaweza kuboresha afya ya meno yakom

Soma Zaidi...
afya somo la 10

Pata elimu juu ya afya hapa ukiwa na vitabu vyetu bila ya malipo yoyote

Soma Zaidi...
Madhara ya kutumia tissue au toilet paper

Post hii inahusu zaidi madhara ambayo tunaweza kuyapata katika matumizi ya toilet paper au tisu kwenye sehemu za siri.

Soma Zaidi...
VYAKULA

Pata elimu juu ya afya hapa ukiwa na vitabu vyetu bila ya malipo yoyote

Soma Zaidi...