Pata elimu juu ya afya hapa ukiwa na vitabu vyetu bila ya malipo yoyote
YANAYOATHIRI AFYA
Afya yamtu inaweza kuathiriwa kuwa njema au kuwa mbovu kwa kuzingatia mambo kadhaa wakadhaa. Hapa nimechagua mambo makuu matano ambayo nitakwenda kuyaangalia ambayo ni;-
A).vyakula
B)Mazingira
C)Shughuli za kila siku
D)Tabia na mazoea
E)Vizazi, familia ama kurithi.
1.VYAKULA
Vyakula ni katika sababu kubwa ambazo husaidia kwa kiwango kikubwa kuathiri afya za watu. Wataalamu wa afya leo wanaeleza na kutaja magonjwa mengi sana ambayoyo yanapatikana kwa kupitia vyakula. Pia yapo magonjwa ambayo huambukizwa kwa kupitia ulaji wa chakula. Hivyo magonjwa mengi na hatari zaidi yamekuwa na mahusiano na vyakula vyetu. Chakula kinaweza kuwa msaada kwako au kuwa ni chanzo cha matatizo ya afya yako.
Mfano mzuri ni kuwa leo wataalamu wa afya anaeleza kuwa mamilioni ya watu wanakufa kwa ugonjwa wa saratani kila mwaka. Tafiti zinaonesha kuwa miongoni mwa sababu za ugonjwa huu ni vyakula. Vyakula ambavyo tunavila leo sio rafiki kwa afya zetu. Tumekuwa tukila vyakula ambavyo vimejaa kemikali nyingi na matatizo kadha wakadha.
Mfano wa pili ni ugonjwa wa kisukari, huu ugonjwa umekuwa ukienea kwa kasi sana duniani leo. Kuanzia watoto, vijana wazee na wajawazito wote wapo hatarini kuapata maradhi haya. Wataalamu wa afya wanataja kuwa vyakula ni katika sababu mjawapo ya kupata maradhi haya. Kuongezeka kwa uzito nje ya uzito wa kawaidi ni katika sababu za kutokea kwa kisukari. Wataalamu wa afya wanaeleza kuwa vyakula ni sababu ya kuongezeka kwa uzito mwilini na kutofanya mazoezi ijapokuwa zipo sababu zingine.
Magonjwa ya moyo kama shinikizo la damu (presha) pamoja na shambulio la moyo (heart attack) ni katika magonjwa yanayowapata watu weng duniani na kusababisha vifo vingi sana. Wataalamu wa afya wanaeleza katika sababu kubwa za kutokea kwa maradhi haya ni vyakula. Hususan vyakula vyenye mchanganyiko mkubwa wa mafuta ya viwandani.
Maradhi ya utapiamlo kama matege, baadhi ya matatizo ya macho, unyafuzi na kwashiakoo pamoja na kudumaa ni katika maradhi ambayo husababishwa na vyakula. Majeraha kutokupona haraka, kuchelewa kupona kwa vidonda na makovu, ngozi kupasuka na kutokwa na vidonda kwenye mdomo ni katika baadhi ya matatizo yanayosababishwa na vyakula Kwa ufupi ni kuwa vyakula ni katika sababu kubwa sana ya maradhia mabayo tuanayapata. Tutazungumzia kwa undani zaidi somo hili kwenye kurasa zijazo na tutaona kwa undani vipi vyakula vinaweza kusababisha yote hayo.
Je! umeipenda hii post?
Ndio Hapana Save post
Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Topic: Jifunze Main: Post File: Download PDF Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 441
Sponsored links
👉1 Kitau cha Fiqh
👉2 Kitabu cha Afya
👉3 Simulizi za Hadithi Audio
👉4 Madrasa kiganjani
👉5 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)
👉6 kitabu cha Simulizi
Namna ya kuzuia dalili za hatari kwa aliyefanyiwa upasuaji
Posti hii inahusu zaidi namna ya kuzuia dalili za hatari kwa aliyefanyiwa upasuaji, ni mbinu mbalimbali ambazo utumika ili kujaribu kuepuka Dalili za hatari kwa aliyefanyiwa upasuaji. Soma Zaidi...
Kwanini najihisi mchovu alafu tumboni kunavitu navihisi vinacheza sielewi
Habari yako Dokta. Soma Zaidi...
MAZINGIRA
Pata elimu juu ya afya hapa ukiwa na vitabu vyetu bila ya malipo yoyote Soma Zaidi...
Sababu zinazopelekea kukosa Usingizi
Posti hii inazungumzia kuhusiana na Sababu zinazopelekea kukosa usingizi. Usingizi ni ugonjwa unaoendelea ambao unaweza kufanya iwe vigumu kusinzia, vigumu kubaki usingizini au vyote viwili, licha ya fursa ya kupata usingizi wa kutosha.Ukiwa na kukosa usi Soma Zaidi...
NYANJA ZA AFYA
Pata elimu juu ya afya hapa ukiwa na vitabu vyetu bila ya malipo yoyote Soma Zaidi...
Zijuwe faida za kiafya za kula Zabibu
Kula zabibubkina faida nyingi kwa afya yako. Soma Zaidi...
afya somo la 10
Pata elimu juu ya afya hapa ukiwa na vitabu vyetu bila ya malipo yoyote Soma Zaidi...
darasa la lishe
Jifunze mengi kuhusu afya na lishe, ujuwe utaratibu wa lishe Soma Zaidi...
NAMNA AMBAZO MWILI HUPAMBANA NA MARADHI
Pata elimu juu ya afya hapa ukiwa na vitabu vyetu bila ya malipo yoyote Soma Zaidi...
Dondoo za afya 21-40
Somo Hili linakwenda kukuletea dondoo mbalimbali za afya Soma Zaidi...
CHUKUWA TAHADHARI HIZI KWENYE MAZINGIRA ILI KULINDA AFYA YAKO
Pata elimu juu ya afya hapa ukiwa na vitabu vyetu bila ya malipo yoyote Soma Zaidi...
dondoo 100 za Afya
Basi tambua haya;- 21. Soma Zaidi...