picha

Dondoo za afya 21-40

Somo Hili linakwenda kukuletea dondoo mbalimbali za afya

? DONDOO NAMBA 21 - 40

Basi tambua haya;-

21.Maji hutumika kupooza ingini. Halikadhalika hutumika kupooza mwili pia.

22.Upungufu wa vitamini A hupelekea kukauka kwa ngozi, uoni hafifu na kuathirika kwa koo na ngozi

23.Upungufu wa vitamin B1 hupelekea kukosa hamu ya kula, udhaifu wa miguu, kupungua kwa hisia kwenye neva kudhoofu kwa misuli na kuathirika kwa akili.

24.Upungufu wa Vitamin B2 hupelekea kupata ugonjwa wa pellagra yaani vidonda vya mdomo na ulimi, ukuaji hafifu, kupasuka kwa nbgozi hasa sehemu za sikio na pua.

25.Upungufu wa Vitamin B12 husababisha matatizo katika uzalishaji wa seli hai nyekundu za damu. Na kusababisha aina ya ugonjwa wa anaemia

26.Upungufu wa vitamini C husababisha kutoka damu kwenye mafinzi, kuchelewa kupona kwa majeraha, maumivu ya viungo na kudhoofu kwa mishipa ya damu hasa kwenye ngozi.

27.Upungufu wa vitamin D husababisha kuleta matege.

28.Upungufu wa vitamin k husababisha kuchelewa kuganda kwa damu kwenye jeraha

29.Upungufu wa madini ya Iodine hupelekea kupata ugonjwa wa Goitre yaani kukuwa kwa tezi ya thyroid.

30.Upungufu wa madini ya potasium hupelekea udhaifu wa misuli kutokuweza kukunja kwa ufasaha.

31.Upungufu wa madini ya magnesium hupelekea utengenezwaji hafifu wa meno na mifupa na misuli hishindwa kukunja kwa ufasaha.

32.Upungufu wa madini ya sodium husababisha kukaza kwa misuli.

33.Upungufu wa madini ya clorine hupelekea mwili kushindwa kuzalisha asidi ya hydrocloric. Asidi hii husaidia katika mmeng’enyo wa chakula mwilini.

34.Upungufu wa madini ya phosphorous hupelekea udhaifu wa meno na mifupa na mwili kwa ujumla.

35.Madini ya calcium yakipungua mwilini husababisha udhaifu wa meno na mifupa.

36.Katika mabo yanayopunguza kinga ya mwili yaani uwezo wa mwili kupambana na maradhi ni misongo ya mawazo, utaratibu mmbovu wa lishe au kutopata lishe bora na mlo kamili, mazingira na madawa.

37.Upigapo chafya ziba mdomo kwa kitu kilicho safi.

38.Kwa mama anayenyonyesha ahakikishe ziwa lake halina kemikali yaani losheni au mafuta ili mtoto asije nyonya kemikali zile.

39.Ugonjwa wa mnjano yaani hepatitis B ni katika magonjwa yanayouwa watu wengi duniani. Karibia watu 620,000 hufa kila mwaka, na karibia watu milioni 350 wameathirika na ugonjwa huu. (WHO)

40.Ugonjwa wa manjano husababishwa na vitusi viitwavyo Hepatitia b (HBV) ambao hawa hushambulia ini na kusababishwa uvimbe. Uvimbe huu unapelekea kupata kansa ya ini.

Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu
Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

       
Author: Rajabu image Tarehe: 2024-05-10 14:53:23 Topic: Jifunze Main: Post File: Download PDF Views 2752

Share On:

Share follows: 0 | Unique share links followed: 0
Sponsored links
๐Ÿ‘‰1 kitabu cha Simulizi     ๐Ÿ‘‰2 Kitabu cha Afya     ๐Ÿ‘‰3 Dua za Mitume na Manabii     ๐Ÿ‘‰4 ai web app     ๐Ÿ‘‰5 Tafasiri ya Riyadh Swalihina     ๐Ÿ‘‰6 Simulizi za Hadithi Audio    

Post zinazofanana:

Jinsi ya kuimarish afya ya meno

Katika post hii utajifunza namna ambavyo unaweza kuboresha afya ya meno yakom

Soma Zaidi...
darasa la lishe

Jifunze mengi kuhusu afya na lishe, ujuwe utaratibu wa lishe

Soma Zaidi...
NAMNA YA KUTUNZA AFYA KUANZIA JIKONI

Pata elimu juu ya afya hapa ukiwa na vitabu vyetu bila ya malipo yoyote

Soma Zaidi...
Faida za kiafya za kufunga

Simulizi yetu ya leo tutajifunza kuhusu faida za kiafya za kufunga kwa mtazamo wa kitabibu, kama anavyoeleza daktari. Tutaangalia namna kufunga kunavyoathiri na kusaidia viungo na mifumo mbalimbali ya mwili. Somo letu la leo litahusuโ€ฆ faida za kiafya za kufunga katika figo, moyo, ini, mfumo wa kinga, kisukari, presha ya damu na mmengโ€™enyo wa chakula.

Soma Zaidi...