picha

MAAJABU YA MBU

7.

MAAJABU YA MBU

7.MBU (MOSQUITO)

Mbu ni katika wadudu wanaopatikana maeneo yenye joto hususan maeneo ynye hali ya hewa ya kitropik. Mbu anafahamika kwa kuwa ndiye msambazaji mkubwa wa malaria pamoja na matende na ngiri maji. Chakula cha mbu ni maji, bakteria pamoja na damu. Mbu dume huweza kumjua mwanamke kwa kutumia sauti ya mbawa. Mbu ni katika wadudu wadogo lakini wana maajabu makubwa. Katika mkala hii tutaangalia kwa ufupi mambo matano kuhusu mbu.

Tofauti na kuwa mbu ni mdogo lakini anaweza kunyonya damu iliyokuwa nzito kuliko mwili wake. Yaani sawa na mtu mwenye uzito wa kilo 70 kula chakula chenye uzito wa kili 100. mara mbu anaponyonya damu mwili wake huchukuwa mpaka siku tatu kuweza kuimengโ€™enya damu ile na kuimaliza. Baada ya hapo mbu atakwenda kunyonya damu tena. Itambulike kuwa chakula cha mbu ni bakteria, maji pamoja na damu. Mbu jike hula damu pindi anapotaka kutaga. Wataalamu wanaeleza kuwa kuna aina 2000 za mbu.

pic Kabla ya mbu kutaga mayai yake anaanza kupima ardhi kama ina majimaji pamoja na joto la kutosha kwa maisha ya mayai yake. Mbu hutaga mayai juu ya maji, ardhi, miti na nyasi pamoja na maeneo mengine yaliyo na majimaji. Pia mbu anaweza kutaga yai lake hata pakiwa na maji kiasi cha tone moja tu. Nayai ya mbu ni chakula kwa samaki pamoja na watutu wengine hivyo mbu huwa makini sana wakati wa kutaga mayai yake.

Tofauti na wadudu wengine na ndege mbu anaweza kulizuia yai lake tumboni kulitaga pindia anapohofia usalama wa yai lake. Kuku na ndege wengine yai linapofikia kutagwa hana namna lazima akalitage, lakini hii ni tofauti kwa mbu. Yai la mbu linaweza kukaa kwa muda wa miaka miwili bila ya kufa na ndo maana ni vigumu kutokomeza kabisa mbu.

Yai la mbu lina rangi ya njano, tangi hii ni rahisi kulifanya yai hili lionewe na maadui walao mayai ya mbu. Hivyo ifikapo usiku yai la mbu hubadilika rangi na kuwa jeusi. Hali hii husaidia kuliepusha yai la mbu kuliwa na maadua. Pia yai la mbu halizami ndani ya maji, na linaweza kuelea hewani, njia zote hizi husaidia ulinzi wa yai hili lisidhuriwe.

Ijapokuwa mbu anakula binadamu lakini na yeye ni chakula kwa viumbe vingine kama popo. Hivyo popo hutusaidia katika mapambano dhidi ya wadudu hawa hatari. mbu pia anaweza kujuwa wati mtu yupo kwa kutumia pumzi anayopumua mwanadamu.


                   

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

       
Author: Rajabu image Tarehe: 2024-05-10 14:53:23 Topic: Mengineyo Main: Post File: Download PDF Views 3226

Share On:

Share follows: 0 | Unique share links followed: 0
Sponsored links
๐Ÿ‘‰1 Kitabu cha Afya     ๐Ÿ‘‰2 Simulizi za Hadithi Audio     ๐Ÿ‘‰3 Bongolite - Game zone - Play free game     ๐Ÿ‘‰4 kitabu cha Simulizi     ๐Ÿ‘‰5 ai web app     ๐Ÿ‘‰6 Madrasa kiganjani    

Post zinazofanana:

Tembo

Posti hii inakwenda kukupa sifa za mnyama tembo

Soma Zaidi...
ZOEZI

Zoezi laย 1 (a) Ainisha maana ya sunnah kilugha na kisheria.

Soma Zaidi...
Njia za Kutatua Migogoro Katika Ndoa

igogoro katika ndoa ni jambo lisiloepukika kutokana na ukweli kuwa wanandoa wawili ni watu tofauti wenye malezi, fikra, na matarajio tofauti. Hata hivyo, tofauti kati ya ndoa zinazostawi na zile zinazoshindwa si ukosefu wa migogoro, bali ni jinsi wanandoa wanavyoitatua. Makala hii inaangazia mbinu za kivitendo za kutatua migogoro ili kudumisha upendo na heshima.

Soma Zaidi...
Maumivu ya Chini ya Tumbo kwa Mwanamke: Sababu na Tiba

โ€‹Maumivu ya chini ya tumbo (nyonga) ni hali inayowapata wanawake wengi katika vipindi tofauti vya maisha yao. Maumivu haya yanaweza kuwa ya ghafla (kali) au ya muda mrefu (sugu), na yanaweza kusababishwa na mifumo mbalimbali mwilini ikiwemo mfumo wa uzazi, mkojo, au mmeng'enyo wa chakula. Makala hii inaangazia sababu kuu za maumivu haya na jinsi ya kukabiliana nayo.

Soma Zaidi...
Ni kwa namna gani nyoka husikia ijapokuwa hana masikio

Ingawa nyoka hawana masikio ya nje kama binadamu na wanyama wengine, bado wana uwezo wa kusikia. Hutumia mifupa ya kichwa na viungo vya ndani kutambua mitetemo kutoka ardhini na mawimbi ya sauti yenye mzunguko mdogo.

Soma Zaidi...