Maumivu ya tumbo baada ya tendo la ndoa

Somo Hili linakwenda kukueleza kuhusu sababu za maumivu ya tumbo baada ya tendo la ndoa

 

MAUMIVU YA TUMBO BAADA YA TENDO LA NDOA

 

Mara nyingi maumivu ya tumbo baada ya tendo la ndoa sio tatizo sana kiasi cha kuogopa. Kwani hali hii husababishwa na gesi iliyoppntumboni mama kama uume ulikuwa ukiingia ndani sana, na hii hutokea endapo uume ni mrefu sana ama mtindo uliotumika katika tendo la ndoa. Tatizo la kupatwa na maumivu wakati wa tendo la ndoa ama baada hutambulika kama dyspareunia.

 

Inakadiriwa kuwa asilimia 10 mapka 20 ya wanawake huweza kusumbuliwa na tatizo hili. Ila pia tatizo hili si kwa wanawake tu hutokea pia kwa wanaume, ila kwa kiasi kidogo yapata lamda asilimia 5. lakini tatizo hili linatibika bila ya wasi hivyo si vyema kuendelea kuteseka.

 

Sababu za maumivu ya tumbo baada ya tendo la ndoa.Tofauti na sababu ya ya gesi ama uume kuingia ndani sana, tatizo hili linaweza kusababishwa na mambo yafuatayo:-

 

1.Fikra, hisia na mawazo ya mtu. Hii hutokea kama mtu ana misongo ya mawazo kibao, ama ana woga juu ya tendo la ndoa ama mahusianao yake na ya mwenzie sio mazuri lamada amembaka ama kumlazimisha, haya yote yanaweza kutengeneza mazingira ya kuumwa na tumbo baada ya tendo.

 

2.Endapo tendo la ndoa litafanyika kwa kiasi kuwa uume uliingia ndani sana. Hii inaweza kusababisha maumivu ya tumbo, ila ni ya muda mfupi na yataweza kuondoka baada ya kupumzika. Ni vyema kubadili mikao ama kupunguza kukandamiza sana uume.

 

3.Wakati mwingine hali huweza kutokea endapo mwanamke ameingia kileleni. Wakati wa kufika kileleni misuli inayozungukia mfumo wa uzazi, maeneo ya kiunoni na nyonga misuli hii kusinjaa na kujikaza na kusababisha maumivu ya chini ya tumbo. Hali jii kitaalamu hufahamika kama dysorgasmia.

 

Watu wanaosumbuliwa sana tatizo hili ni:-A.WajawazitoB.Wenye matatizo kwenye ovariC.wenye mashambulizi ya kwenye mfumo wa uzazi (PID)D.Wenye matatizo kwenye korodani.

 

4.Gesi; wakati wa kupushi uume ndani unaweza kupushi hewa kuingia ndani ya tumbo. Sasa kama hewa hii itanaswa sehmemu humo ndani inaweza kusababisha maumivu ya tumbo kwa juu ama kifuani. Mtu anaweza kuhisia kama gesi inatembea tumboni na maumivu haya yanaweza kuelekea maeneo mengine ya mwili.

 

5.Kama mtu anasumbuliwa na UTIUTI inaweza kuwa ni katika sababu za maumivu haya. Mtu pia anaweza kuhisi dalili kamaA.Maumivu wakati wa kukojoa kama anaunguaB.Kukojoa mara kwa maraC.Mkojo kuwa mchafuD.Kuwa na damu kwenye mkojoE.Maumivu ya mkundu.

 

6.Kuwa na maradhi ya ngono kama gonoria na chlamydia. Pia mtu anaweza kuona dalili kama:A.Kutoa harufu mbaya sehemu za siriB.Kutokwa na uchafu sehemu za siriC.Maumivu wakati wa kukojoa

 

7.Kama mfuko wa uzazi umeinama, hii inaweza kupelekea kuguswa kwa mfukowa uzazi wakati wa tendo la ndoa hivyo kupelekea maumivu

 

8.Kama kunashida kwenye ovari

 

9.Kama kuna uvimbe kwenye kizazi. Dalili zake ni kamaA.Kutokwa na damu nyingi wakati wa hedhiB.Hedhi kutokata ndani ya siki 7C.Kukosa chooD.Maumivu ya miguu ama mgongo

 

10.Kama mirija ya falopia imeziba.

 

11.Kama mwanaume ana maradhi kwenye mfumo wa uzazi.

 

?

Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 1970-01-01 03:33:44 Topic: Jifunze Main: Afya File: Download PDF Views 2888

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
👉1 web hosting    👉2 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)    👉3 Bongolite - Game zone - Play free game    👉4 Kitabu cha Afya    👉5 kitabu cha Simulizi    👉6 Dua za Mitume na Manabii   

Post zinazofanana:

ilinde Afya yako

Hiki ni kitabu kilichosheheni masomo zaidi kuhusu Afya yako, vyakula pamoja na maradhi sugu.

Soma Zaidi...
Zijue sehemu kuu nne za chumba cha upasuaji

Post hii inahusu zaidi sehemu kuu nne za chumba cha upasuaji, chumba cha upasuaji kina sehemu kuu nne na sehemu hizo ufanya kazi tofauti tofauti kama ifuatavyo.

Soma Zaidi...
kitabu cha matunda

Jifunze sifa na aina za matunda, vijuwe viruturubisho

Soma Zaidi...
Umuhimu wa kuvaa nguo za upasuaji.

Posti hii inahusu zaidi umuhimu wa nguo za upasuaji, tunajua wazi kuwa, wakati wa upasuaji tunapaswa kusafisha chumba na mazingira yake lengo ni kuhakikisha kuwa tunazuia wadudu wasisambae au kuingia kwenye mwili wa binadamu.

Soma Zaidi...
Dondoo za afya 61-80

Somo Hili linakwenda kukueleza kuhusu dondoo za afya

Soma Zaidi...
UGONJWA WA MALARIA NA TAKWIMU ZA ATHARI YAKE KIDUNIA

Malaria ni katika maradhi ambayo husambazwa na na mbu jike aina ya anopheles.

Soma Zaidi...
DARASA LA AFYA NA AFYA YA UZAZI

Jifunze mengi kuhusu Afya, kuwa nasi kwenye makala hii hadi mwisho.

Soma Zaidi...